Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
Mwenye nyumba hii anahitaji kukutana na Tume ya Rais ya kukusanya maoni juu ya Marekebisho ya Katiba; wajumbe wa tume watamfikiaje huyu? taarifa za ujio wa Wajumbe wa Tume atazipataje?
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Wella iliyoko Manispaa ya Dodoma hutembea umbali wa zaidi ya Km 10 kwenda na kurudi shuleni kila siku. Shule hii ni ya Kata ya Kikuyu Kusini.
Mandhari ya Mji wa Singida.
Hizi ni picha za bafu na Choo kwa wavulana wa shule ya sekondari Mbabala
Hili ni Bweni la wavulana katika shule ya sekondari Mbabala! Humu ni ndani ya Bweni la wavulana katika shule ya Mbabala Sekondari Moja ya nyumba ambayo baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mbabala "GHETO" wamepangisha na kuishi humu. Kwa nyumba kama hii; tutarajie nini kwa wapangaji hawa? Wajasiriamali wa biashara ya Mkaa wakisaka wateja.
Kibao kinachokataza kutumia lugha ya kirangi na kusisitiza kutumia kiswahili katika shule ya sekondari Chagaa iliyoko Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma. Wanafunzi wa shule hiyo hutumia zaidi lugha ya Kirangi kuliko Kiswahili na Kiingereza kwao ni majaaliwa ya Muumba. Mlezi wa wanafunzi wa kiume katika shule a Kikuyu Sekondari Tumaini Wambura akitoa ushauri na rai kwa washiriki wa mjadala wa Club ya Marafiki kuzingatia maadili ili kutimiza ndoto yao ya kuhitimu Elimu ya Sekondari kwa mafanikio na kwenda kutumikia jamii.
Mwandishi wa Habari kutoka Kituo cha TV cha Chanel 10 akipiga picha wakati mwanafunzi Ruthilinda Egberth akichangia katika mjadala wa wanafunzi wa Club ya Marafiki wa Elimu Dodoma katika shule ya Sekondari Kikuyu ya Dodoma. Mchangiaji katika Mjadala wa katiba akisisitiza jambo wakati wa mjadala wa katiba uliofanuika Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wakazi wa mji huo zaidi ya 300.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bibi Betty Mkwasa akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mjadala wa Katiba ulioandaliwa na DUNGONET kwa ufadhili wa shirika la The Foundation for Civil Society la jijini Dar Es Salaam
Bweni la wavulana katika shule ya Sekondari Mbabala iliyoko Manispaa ya Dodoma. Kwa hali hii tutarajie matokeo gani kwa wanafunzi zaidi ya 43 wanaoishi katika ghala hili ambalo leo nimebadilishwa jina na matumizi hadi kuuwa Bweni bila marekebisho?
Choo chenye matundu mawili kinacho tumiwa na wavulana zaidi ya 43 wa Mbabala Sekondari Manispaa ya Dodoma Mkoani Dodoma.
Wanaharakati wa Warsha ya Jukwaa la Katiba Wakisikiliza michango ya washiriki.
Jenngo hili ni mfano wa moja ya majengo yaliyojengwa kwa fedha za Mpango wa Kuboresha Elimu ya Msingi (MMEM) katika shule ya Msingi Amani iliyoko Manispaa ya Dodoma mwaka 2005.
Mjini ni kazi na kilimo; utakula nini bila kushiriki kwenye uti wa mgongo wa Taifa hili? Acha uvivu wa kujifanya mtoto wa mjini; Shiriki kuzalisha shambani.
Mjumbe wa Bodi ya AFNET Mch. Kanyamala (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa AFNET Taifa Bi. Sarah Mwaga wakti wa maadhimisho ya kupinga ukatili wa wanawake Mkoani Singida.
Baadhi ya wanaharakati waliongana na wakazi wa mji wa Singida katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijisnia. Maadhimisho hayo yaliongozwa na ujumbe wa "Pinga Ukatili Imarisha Familia"
Mwakilishi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Bw. Ally Jumanne aliye simama katikati akichangia mada katika Mdahalo wa Wagombea Ubunge jimbo la Dodoma Mjini ulioandaliwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoani Dodoma (NGONEDO) 2010.
Wasanii wakitoa Elimu kwenye Moja ya Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010
Wadau wa Habari na wanaharakati wakizuru kaburi la Mtemi Mazengo katika Kijiji cha Mvumi Makulu Wilaa ya Chamwino Moani Dodoma.
Kaburi la Mtemi Daudi Salomona Mazengo Chalula aliyefariki Tarehe 17 Januari, 1967 anakadiriwa kuwa na Umri wa Miaka 106.
Pichani juu ni Fullgence Ngonyani akifurahia mchezo wa kuruka wakati picha ya chini ni Prince E. Kimaro .
Mchezo wa kuruka ni moja kati ya michezo inayojenga Afya na kuboresha uwezo wa Ubongo kufikiri na kutoa maamuzi kwa haraka. |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe