Injira

/jeanmedia/news: Kinyarwanda: WI0000C9C806B33000011021:content

« Inyuma   ·   Ahakurikira »
Base (Igiswayire) Kinyarwanda

Mtweve: Kujitolea damu hakuna madhara.

Na ASIA KILAMBWANDA, Mtwara Community media

Meneja wa mpango wa uchangiaji damu salama kanda ya kusini, Mtweve Vincent amesema kuwa hakuna madhara yeyote yanoyoweza kutokea endapo mtu atachangia au kutoa damu kwa njia iliyo salama.

Mtweve amesema hayo wakati akiongea na mwandishi wa habari hii ofisini kwake juu ya tathmini ya mwamko wa jamii katika uchangiaji wa damu kwa hiari katika mikoa ya kusini inayaojumuisha mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na maeneo machache ya mikoa ya nyanda za juu kusini (BIG FOUR) ambayo ni maeneo ya Namtumbo na Tunduru.

“Hali ya hamasa ya uchangiaji wa damu kwa wananchi wa mikoa ya kusini imeshuka kutoka asilimia 60 hadi kufikia asilimia hamsini kwa mahitaji ya kanda na asilimia 65 hadi asilimia 35 kwa mahitaji ya lengo la kitaifa kutokana na imani iliyojengeka kwa jamii kuwa ukitoa au kuchangia damu unaweza kupata madhara ikiwa pamoja na magonjwa na kuongezeka kwa damu mara kwa mara”,Mtweve alisema.

Mbali na hali hiyo ya ushukaji wa uchangiaji wa damu salama lakini mpango huu umeonesha faida na hatua zilizofikiwa katika kupunguza idadi ya vifo vya kina mama na watoto katika kanda ya kusini na Taifa kwa ujumla.

Aidha kutokana na harakati zinazofanya na mpango huu,Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula hospitali) imeripotiwa kutokuwa na idadi ya vifo vinavyotokana na wagonjwa wa upungufu wa damu kutokana na kupewa asilimia mia moja(100%) ya damu zinazochangiwa na jamii chini ya usimamizi wa Mpango wa uhamasishaji uchangiaji Damu salama kanda ya kusini.

Akielezea changamoto zinazosababisha kiwango cha uchangiaji damu katika mikoa ya kusini Mtweve amesema, hali ya makusanyo ya damu katika mikoa ya kusini imeshuka kutokana na asilimia kubwa ya wachangiaji kuwa wanafunzi ambao mara nyingi wengi wao hawana makazi ya kudumu jambo ambalo linasababisha kutofikia lengo.

“Kuanzia Januari hadi machi mwaka huu ni asilimia 35 tu za makusanyo ya damu yaliyopatikana katika mikoa ya kusini(Southern zone), makusanyo ambayo ni chini ya lengo la ukusanyaji wa damu lililowekwa kitaifa, hali hii inatokana na wachangiaji wakubwa kuwa ni wanafunzi,uelewa mdogo wa lengo la uchangiaji damu, mila potofu na umasikini hasa katika maeneo ya vijijini”,Mtweve aliongeza.

Kwa upande wa vikwazo vilivyoko mashuleni ni pamoja na wanafunzi wengi kutofikia vigezo vya utoaji wa damu ambavyo ni kuwa chini ya umri uliopangwa yaani miaka 18 na kuwa chini ya uzito wa kilogramu hamsini(50) ambapo mlinganyo wa waliofikia vigezo kuwa wachachezaidi ya wasio na vigezo.

Mbali na changamoto zinazoukabili uchangiaji wa damu kanda ya kusini, mpango huo umepanga kuhuisha uchangiaji damu kwa kujenga kituo kidogo(Satelite Centre) katika mkoa wa Lindi ambacho kitafanya makusanyo katika wilaya ya Lindi Mjini, pia umeanzisha Vikundi 35 vya vijana(Clubs) vinavyolenga kuhamasisha vijana katika uchangiaji wa damu.

Kwa upande wa taarifa iliyotolewa na Afisa Utawala wa mpango wa uhamasishaji uchangiaji damu salama Kanda ya kusini, Baraka Mfunguo Novemba 11, 2009 alitaja changamoto zilizopo mahospitalini kuwa ni pamoja na wagonjwa kuuziwa damu jambo ambalo ni kinyume na taratibu na lengo la mpango huo.

Hivyo kutokana na hali hiyo Mfunguo amewaomba baadhi ya watumishi wanaouza damu mahospitalini kutambua haki za watu wanaochangia damu kwa kutoa ushirikiano ili kazi ziende kwa ufanisi na kutoa hamasa kwa wananchi ili ongezeko la uchangiaji damu lipande.

Aidha aliwataka wananchi watakaoombwa rushwa ama kuuziwa damu kutoa taarifa katika vyombo vya sheria , taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(PCCB), uongozi wa Hospitali na hata ofisi za uchangiaji damu salama watasaidiwa kwa kuwa kuongezewa damu bila malipo ni haki yao.

Mpango wa uchangiaji damu salama kanda ya kusini ulizinduliwa mnamo June 14, 2007 ambapo hivi sasa umeweza kupiga hatua ya kuokoa maisha ya watu waliokuwa wakipoteza maisha kutokana na upungufu wa damu hasa kinamama wajawazito na watoto jambo ambalo mwanzoni ilikuwa hadi ndugu wachangie damu tofauti na sasa.

(Not translated)

Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe