Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
4. UZINDUZI WA MAKTABA YA JAMII YA WEMA - MKALAPA Tarehe 11 Julai 2009 iliambatana na tukio muhimu na la kihistoria katika kijiji cha Mkalapa. Kijiji cha Mkalapa kipo katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Kikundi cha Wanaharakati wa Elimu, Mazingira na Afya-WEMA walizindua rasmi Maktaba yao ya Jamii ya WEMA ambayo ina vitabu na machapisho zaidi ya 750. Vitabu vilivyomo kwenye maktaba ya WEMA vimechangiwa na wafuatao; HakiElimu (machapisho na vitabu zaidi ya 150), Mratibu na mshauri wa kikundi Mr. Mussa P.M. Kamtande (amechangia vitabu na machapisho zaidi ya 450), pamoja na taasisi kama; Chuo cha Ualimu Mtwara (K), na Chuo cha Ualimu Mtwara (U), ambao kwa pamoja wamechangia machapisho yapatayo 150. Katika picha hapa chini anaonekana Mwenyekiti wa Kikundi cha WEMA Mr. Fidelis Milanzi akiwa na mgeni rasmi Mr. Richard Lucas wakiangalia vitabu kwenye maktaba hiyo. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe