Base (Swahili) | English |
---|---|
Wanaharakati Wajadili Mchakato wa Katiba Mpya.Mchakato wa kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unazidi kushika kasi zaidi nchini baada ya wanaharakati wa mikoa saba kukutana Dodoma kujadili na kujifunza juu ya katiba ya sasa na mapungufu yake na jinsi ya kuelimisha wananchi umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Warsha hiyo ya sikun tatu inafanyika katika Hoteli ya Dodoma inahudhuriwa na wawakilishi wa Mitandao ya Asasi za Kiraia kutoka katika Mikoa ya Morogoro, Lindi, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Mbeya Dodoma na Tabora. Washiriki wa warsha hiyo wameeleza nia yao ya kuhakikisha kuwa watadumu katika kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanziba na kuahidi kuwa watajitahidi kuhakikisha katika mchakato huo watajitahidi kuziondoa kasoro zinazoonekana kuwa zinayumbisha Mungano huo. Wakichangia mada katika warsha hiyo inayoonekana kuwavuta wanaharakati ha ambao ni waumini wa Asasi za kiraia nchini wamesema kuwa kazi ya kuelimisha jamii juu ya uwepo wa Katiba Mpya ni ya muhimu inayohitaji kujituma na kuwa na moyo wa kujitolea kuisaidia jamii ili ielimke na kuwa na maamuzi yaliyo sahihi na yenye manufaa kwa Taifa. Naye Mkufunzi wa warsha hiyo Bw. Deus Kibamba (picha ndogo)kutoka Jukwaa la Katiba amesema watanzania watashiriki kwa mara ya kwanza kutunga katiba yao kwani katiba iliyopo kwa sasa hakutungwa na watanzania bali watanzania waliletewa katiba hiyo iliyotungwa na waingereza. Washiriki wa warsha hiyo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kukata kiu ya watanzania katika kudai katiba mpya. Wadau hao walisema kuwa kauli ya Rais aliyoitoa kwenye maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM mkoani Dodoma tarehe 5 Februari, 2011 ilimaliza utata uliokuwepo kutokana na kauli tata za baadhi ya watendaji wake kama Mwanacsheria Muu wa Serikali na Waziri wa Sheria na Katiba. Warsha hiyo inayoendeshwa kwa mtindo shirikishi kwalengo la kuwafanya washiriki wote wajisikie kuwa sehemu ya mchakato huo; imekuwa ya mafanikio makubwa hasa kutokana na wengi wa washiriki kuonekana kuwa makini na wasikivu katika kila hatua. Tanzania, Tanzania; nakupenda kwa moyo wote.... Wanaharakati waliimba wimbo huo kuonyesha mshikamano wao kwa Tanzania na nia yao njema ya kudumisha Muungano huo ambao wamesema ni wa kipekee duniani hivyo hauna budi kuendelea kuwepo ili kuiweka Tanzania katika historia hiyo. |
Activists discuss the process of constitutional line.The process of writing a new constitution of the United Republic of Tanzania continues to keep pace over the country after seven regional activists meet in Dodoma to discuss and learn about the current constitution and its limitations and how to educate the public importance of a new constitution. The workshop of a three-kun held in Dodoma Hotel inahudhuriwa and representatives of civil society networks from the regions of Morogoro, Lindi, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Dodoma and Tabora. Participants have expressed their intention to ensure that they remain in the Union of Tanganyika and secured Zanziba and promising that they will strive to ensure the process will work to remove defects visible zinayumbisha Compounds that time. Wakichangia topics in the workshop visible persuading activists ha who are members of civil society in the country have said that the task of educating the community about the presence of a new constitution is the key that requires commitment and a spirit of volunteerism to help the community to ielimke and making things right and highly beneficial to the nation. And Mr. Trainer's workshop. Deus Kibamba (small pictures) from the Constitutional Forum has said Tanzania will participate for the first time framing their constitution because the constitution is not currently available in Tanzania but composed and Tanzania were brought to the constitution made by the British. Participants have applauded the President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete of Tanzania cut the thirst in demanding a new constitution. Stakeholders were said to be statements of the President was made in celebration of the Feast of fulfilling 34 years of the birth of the CCM in Dodoma on February 5, 2011 ended the complexity of the existing due to statements the complex of some of its practitioners as Mwanacsheria Muu's Government and Minister of Justice and Constitutional . The workshop run by a collaborative fashion Goals of making all participants feel a part of the process, has been a great success especially since many of the participants appear to be sensitive and responsive in every step. Tanzania, Tanzania, I love you with all your heart .... The activists sang the song to show their solidarity for Tanzania and the good intentions of maintaining their alliance that they say is unique in the world so it should continue to exist to put it in Tanzania's history. |
Translation History
|