Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UHAMASISHAJI WA KUPIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO, BONDE LA NGORONGORO NA TUKIO LA KUHAMA WANYAMA KATIKA HIFADHI YA SERENGETI KATIKA SHINDANO LA MAAJABU SABA YA ASILI KATIKA BARA LA AFRIKA Hivi karibuni pamekuwa na shindano jipya lijulikanalo kama seven Natural Wonders linaloshindanisha vivutio mbalimbali vya asili vinavyopatikana katika kila bara. Shindano hilo linaloendeshwa kwa kupiga kura kupitia tovuti ya http://sevennaturalwonders.org linashindanisha vivutio vya utalii kumi na viwili (12) katika bara la Afrika. Tanzania ni nchi pekee yenye vivutio vingi katika orodha hiyo. Vivutio vya Tanzania ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na hifadhi ya Serengeti. Watanzania na watu wote duniani wanahamasishwa kuvipigiakura vivutio hivyo vitatu Shindano hili linaweza kuwa fursa nzuri kwa Tanzania kujitambulisha pamoja na kuitangazia dunia kuwa Mlima Kilimanjaro, ambao ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika; Hifadhi ya Serengeti, ambapo tukio la kuhama wanyama hutokea kila mwaka; na eneo la Ngorongoro, ambalo ni urithi wa dunia wa asili na utamaduni (natural and cultural World Heritage Site), vyote ni vivutio vilivyopo hapa kwetu Tanzania. Imetolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe