Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
HISTORIA YA JUMUIYA Kwa kutambua kuwa kila mtu analo jukumu kubwa la kuelimisha umma na kutayarisha Taifa bora lenye maendeleo ya kisasa kwa maisha ya leo na ya baadae. Kwa kuwa kazi ya kuelimisha inahitaji elimu, ujuzi, ufahamu, uadilifu, uvumilivu na kujitolea kwa dhati. Sisi Kama raia wengine tunayo haki ya kujiunga pamoja Kwa nia ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni katika kutatua matatizo ambayo yanaikumba jamii yetu yakiwemo:
Nikweli kwamba asilimia kubwa ya vijana katika shehia hii wanaonekana kuwa ni vijana waliokosa maadili mema katika shuguli zao za kila siku. Sababu ambayo imepelekea mambo yafuatayo: i. Kupungua na kutoweka heshima kwa wakubwa zao. ii. Mwanaadamu kutothaminiwa utu wake kwa kuongezeka kwa matusi, vitendo vya aibu, fedheha na kashfa mbalimbali kitu ambacho ni kinyume na haki za binaadamu. iii. Kuanzishwa kwa vikundi viovu vya uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya. iv. Kuongezeka kwa vitendo vya uasharati. v. Udhururaji ovyo kwa vijana bila ya shughuli maalumu. vi. Kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu ukiwemo wizi na kadhalika. Hali ambayo inapelekea madhara makubwa katika jamii yakiwemo:
Mazingira katika shehia yetu yanaonekana kutokuwa mazuri kwa namna moja au nyengine.Hii imesababishwa na wanajamii kufanya yafuatayo: i. Ukataji wa miti ovyo, bila ya mpango maalumu. ii. Ujenzi usiokuwa wa mpango maalumu mwenye kuharibu vianzio vya maji na sehemu za mitaro ya kusafirishia maji. iii. Kuvamiwa sehemu mbalimbali kwa uchimbaji wa mchanga, sehemu ambazo zisizoruhusu shughuli hiyo. iv. Tatizo kubwa la utupaji wa takataka sehemu zenye makaazi ya watu. Hali ambayo inapelekea madhara makubwa katika jamii yakiwemo:
Kwa upande wa utamaduni katika shehia yetu umeonekana kudharaulika, kwani vijana wanaonekana wenye kuthamini Utamaduni wa nchi za kigeni.Suala ambalo linaleta athari zikiwemo: i. Kupoteza haiba ya nchi yetu. ii. Kuikosesha mapato Serikali yetu. Kwavile ,” mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe “. Serikali pamoja na asasi zisizo za kiserikali nazo pia zinalo jukumu kubwa la kuhakikisha maendeleo yanapatikana.Hivyo wakaazi wa M/Kwerekwe Zanzibar kwa pamoja tuliazimia kuungana na vijana wengine na kuunda jumuiya yetu itakayohakikisha kuwa tunajiletea maendeleo ya Taifa letu. Hivyo mnamo mwaka 2009 Jumuiya ya Mwanakwerekwe Environmental Ethics and Cultural Organization (MEEC0) imeanzishwa. Imesajiliwa kwa sheria za jumuiya zisizo za kiserikali (NGO's) mwaka 2011, yenye nambari ya usajili 919. Jumuiya hii imeanzishwa kwa kutatua matatizo yaliyoelezwa hapo juu. MAFANIKIO MAKUBWA ILIYOPATA JUMUIYA Jumuiya ya Mwanakwerekwe Environmental Ethics and Cultural Organization (MEECO) imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miongoni mwa mafanikio hayo yakiwemo:
Lakini miradi yote hiyo tunasubiri majibu.
|
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe