Log in

/MEECO/history: English: WI000D7AB754795000028555:content

« Previous   ·   Next »
Base (Swahili) English

HISTORIA YA JUMUIYA

Kwa kutambua kuwa kila mtu analo jukumu kubwa la kuelimisha umma na kutayarisha Taifa bora lenye maendeleo ya kisasa kwa maisha ya leo na ya baadae.

Kwa kuwa kazi ya kuelimisha inahitaji elimu, ujuzi, ufahamu, uadilifu, uvumilivu na kujitolea kwa dhati.

Sisi Kama raia wengine tunayo haki ya kujiunga pamoja Kwa nia ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni katika kutatua matatizo ambayo yanaikumba jamii yetu yakiwemo:

  1. Mmong’onyoko wa Maadili.

 Nikweli kwamba asilimia kubwa ya vijana katika shehia hii wanaonekana kuwa ni vijana waliokosa maadili mema katika shuguli zao za kila siku. Sababu ambayo imepelekea mambo yafuatayo:

           i.         Kupungua na kutoweka heshima kwa wakubwa zao.

         ii.         Mwanaadamu kutothaminiwa utu wake kwa  kuongezeka kwa matusi, vitendo vya aibu, fedheha na kashfa mbalimbali kitu ambacho ni kinyume na haki za binaadamu.

        iii.         Kuanzishwa kwa vikundi viovu vya uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.

        iv.         Kuongezeka kwa vitendo vya uasharati.

         v.         Udhururaji ovyo kwa vijana bila ya shughuli maalumu.

        vi.         Kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu ukiwemo wizi na kadhalika.

Hali ambayo inapelekea madhara makubwa katika jamii yakiwemo:

  1. Vifo vya kutatanisha.
  2. Ulemavu wa maisha.
  3. Vijana kupoteza mtazamo wao sahihi wa maisha.
  4. Vijana kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu.
  1. Uharibifu wa Mazingira

Mazingira katika shehia yetu yanaonekana kutokuwa mazuri kwa namna moja au nyengine.Hii imesababishwa na wanajamii kufanya yafuatayo:

           i.         Ukataji wa  miti ovyo, bila ya mpango maalumu.

         ii.         Ujenzi usiokuwa wa mpango maalumu mwenye kuharibu vianzio vya maji na sehemu za mitaro ya kusafirishia maji.

        iii.         Kuvamiwa sehemu mbalimbali kwa uchimbaji wa mchanga, sehemu ambazo     zisizoruhusu shughuli hiyo.

        iv.         Tatizo kubwa la utupaji wa takataka sehemu zenye makaazi ya watu.

   Hali ambayo inapelekea madhara makubwa katika jamii yakiwemo:

  1. Kukosekana kwa mvua, vivuli na uvutaji wa hewa safi.
  2.   Kuweko uhaba wa maji katika shehia.
  3.   Kutuwama kwa maji machafu na madimbwi ya hapa na pale.
  4.   Kuzuka kwa maradhi ya kuambukiza na kuenea kwa harufu mbaya.
  1. Kupotea kwa Utamaduni wa Mzanzibari.

  Kwa upande wa utamaduni katika shehia yetu umeonekana kudharaulika, kwani vijana wanaonekana wenye kuthamini Utamaduni wa nchi za kigeni.Suala ambalo linaleta athari zikiwemo:

               i.         Kupoteza haiba ya nchi yetu.

              ii.         Kuikosesha mapato Serikali yetu.

Kwavile ,” mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe “. Serikali pamoja na asasi zisizo za kiserikali nazo pia zinalo jukumu kubwa la kuhakikisha maendeleo yanapatikana.Hivyo wakaazi wa M/Kwerekwe Zanzibar kwa pamoja tuliazimia kuungana na vijana wengine na kuunda jumuiya yetu itakayohakikisha kuwa tunajiletea maendeleo ya Taifa letu. Hivyo mnamo mwaka 2009 Jumuiya ya Mwanakwerekwe Environmental Ethics and Cultural Organization (MEEC0) imeanzishwa. Imesajiliwa kwa sheria za jumuiya zisizo za kiserikali (NGO's) mwaka 2011, yenye nambari ya usajili 919. Jumuiya hii imeanzishwa kwa kutatua matatizo yaliyoelezwa hapo juu.

MAFANIKIO MAKUBWA ILIYOPATA JUMUIYA

Jumuiya ya Mwanakwerekwe Environmental Ethics and Cultural Organization (MEECO) imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miongoni mwa mafanikio  hayo yakiwemo:

  1. Kukubalika katika jamii ya Zanzibar na vitongoji vyake
  2. Kuweka Mazingira safi baadhi ya Mitaa ya Mwanakwerekwe Zanzibar
  3. Kuzuia uharibifu wa mazingira uliokithiri kwa kuwapa elimu inayostahiki na kuwachukulia hatua waharibifu hao kwa kushirikiana na jeshi la Polisi.
  4. Kufukia shimo kubwa lililokuwa hatari kwa wakaazi wa mtaa wa Mwanakwerekwe.
  5. Kufanya dhiara mjini na vijijini za kuhamasisha jamii juu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
  6. Kuwakusanya vijana na kuunda timu mbalimbali za michezo. Ikiwemo sarakasi, mpira wa miguu ili wasiwe na mawazo mabovu ya kujiingiza katika vikundi viovu,kutumia madawa ya kulevya, kujiingiza katika vishawishi vinavyopelekea HIV/AIDS
  7.  Kuwapa elimu ya maadili vijana wa Mwanakwerekwe.
  8. Kuandika miradi mitatu ya maendeleo ikiwemo :
  • Mradi wa ushirikishwaji wa vijana katika maamuzi na mipango ya Maendeleo
  • Mradi wa kujengewa uwezo wa Asasi
  • Mradi wa kuzuia uharibifu wa mazingira wa uchimbaji wa mchanga kiholela

Lakini miradi yote hiyo tunasubiri majibu.

 

 

 

HISTORY OF THE COMMUNITY

Recognizing that each person only has a vital role to educate the public and make a better nation for the development of the modern life of today and the future.

Since the work of education requires knowledge, skill, knowledge, integrity, perseverance and dedication.

We as citizens have the right to join together in order to bring economic, social and cultural problems in our society which yanaikumba including:

  1. Mmong'onyoko of Ethics.

  Is true that a large percentage of youth in this shehia seem to be teenagers who lack moral principles in their daily activities. The reasons which led to the following:

i. The decline and disappearance of respect for their bosses.

ii. Man kutothaminiwa his personality to the increase in assault, acts of shame, humiliation and various scandals something that is contrary to human rights.

iii. The introduction of the smoking groups, omissions, or use of drugs.

iv. The increase in acts of wastefulness.

v. Udhururaji distraction for young people without activity.

vi. The increase in criminal acts including thefts and so on.

The situation which leads to serious consequences in the community including:

  1. Mortality confusing.
  2. Disability life.
  3. Young people lose correct their view of life.
  4. Young people lack their basic rights including education.
  1. Environmental Damage

Environment in our shehia seems no good in one way or nyengine.Hii caused to communities to do the following:

i. Both the deforestation of trees, disposal, without special arrangements.

ii. Building non-specific plan to destroy the sources of water and transporting part of the drainage water.

iii. Invasions parts for the extraction of sand, where zisizoruhusu activity.

iv. The main problem of waste disposal areas of residence.

The situation which leads to serious consequences in the community including:

  1. The lack of rain, shadows and smoking of fresh air.
  2. The presence of water shortage in shehia.
  3. Linger for filthy water and ponds here and there.
  4. Infectious disease outbreak and spread of odor.
  1. Loss of Zanzibari culture.

  In terms of culture have appeared in our shehia kudharaulika, because young people seem to appreciate the culture that makes kigeni.Suala effects including:

i. Loss personalities of our country.

ii. Kuikosesha Our government revenues.

Since, "the architect is a citizen himself." Government and NGOs are also zinalo role of ensuring the residents of the development yanapatikana.Hivyo M / Kwerekwe Zanzibar together we commit ourselves to connect with other youth and create itakayohakikisha our community that we brought our national development. So in 2009 Mwanakwerekwe Community Environmental Ethics and Cultural Organization (MEEC0) has been established. Registered by the law of non-governmental organizations (NGO's) in 2011, with registration number 919. This community has been established to solve the problems outlined above.

A highly successful Community

Community Mwanakwerekwe Environmental Ethics and Cultural Organization (MEECO) has made some progress since the inception of these achievements include:

  1. Acceptance in the community of Zanzibar and its surroundings
  2. Keeping the environment clean some streets Mwanakwerekwe Zanzibar
  3. Preventing damage to the environment by providing education extreme inayostahiki and consider them pests such measures in conjunction with military police.
  4. Bury large hole was dangerous for the residents of the estate of Mwanakwerekwe.
  5. Making dhiara promoting urban and rural communities on the preservation and conservation...

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register

Translation History

Google Translate
July 18, 2011
HISTORY OF THE COMMUNITY – Recognizing that each person only has a vital role to educate the public and make a better nation for the development of the modern life of today and the future. – Since the work of education requires knowledge, skill, knowledge, integrity, perseverance and dedication. – We as citizens have the right to join together in order to bring...