Envaya

/TEYODEN/post/115513: Kiswahili: WIfFz3dCCm5AX1gEuuecWKra:content

Asili (Kiswahili) Kiswahili

WASICHANA WALIOZAA CHINI YA UMRI WA MIAKA 20 NA AMBAO WAPO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI WAPATA NAFASI NYINGINE YA KUPEWA MAFUNZO NA MITAJI ILI WAWEZE KUJIENDESHA KIMAISHA.

TEYODEN imefanya shughuli ya utambuzi wa wasichana  walio katika mazingira hatarishi ambao pia wamezaa chini ya miaka 20 ili waweze kuwa wanufaika wa mradi wa mwaka mmoja utakao kuwa unawawezesha kusimama upya kama watu wengine katika jamii.Mradi huu unaoendelezwa baada ya kutekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja hapo 2011-2012.Moja kati ya matunda ya mradi kwa kipindi cha utekelezaji cha 2011-2012 ni kuwezesha wasichana (kinamama wadogo) 20 kuwa na miradi ya kiuchumi iliyochangia kujiwekea akiba ya sh 1,200,000 benki inayosubili kujenga uwezo wa wasichana wengine zaidi.

Wasichana (wamama wadogo) 8 na mratibu wa mradi wameuhudhuria mafunzo ya siku  6 jijini Arusha kupata mafunzo zaidi ya namna ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika kutekelezaji wa mradi huu kwa kipindi kilichopita.

Katika kipindi cha siku 10 zijazo wasichana 60 (20 wanaoendelea na 40 wapya) watapata nafasi ya kuwezesha mafunzo ya stadi za maisha na stadi za ujasiliamali kabla ya kupewa mitaji kwaajili ya kuanzisha  na kuendeleza biashara walizo/watakazoziibua katika maeneo yao kama hatua/shughuli  moja wapo ya mradi huu.

Katika kipindi cha utekelezaji cha 2013-2014 mradi huu utaendelea katika kata za Azimio,Mtoni na Kibada na unategemea kuwanufaisha wasichana wa waliofanya vizuri katika kipindi kilichopita na wasichana wengine wapya.

"Nawakaribisha sana wasichana ambao wamezaa chini ya miaka 20 kujiandikisha kwa wingi kwa watendaji wa mitaa na kata katika zilizotajwa hapo juu ili waweze kusailiwa na kuandikishwa katika orodha ya wanufaika wa mradi" anasema mratibu wa mradi bwana Yusuph Kutegwa.Walimu wa wasichana waliochaguliwa na wasichana wenyewe wakiwa kwenye mafunzo ya uongozi na uwezeshaji,Ukumbi wa Azimio la Arusha jijini Arusha.

 

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe