Base (Swahili) | English |
---|---|
WASICHANA WALIOZAA CHINI YA UMRI WA MIAKA 20 NA AMBAO WAPO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI WAPATA NAFASI NYINGINE YA KUPEWA MAFUNZO NA MITAJI ILI WAWEZE KUJIENDESHA KIMAISHA. TEYODEN imefanya shughuli ya utambuzi wa wasichana walio katika mazingira hatarishi ambao pia wamezaa chini ya miaka 20 ili waweze kuwa wanufaika wa mradi wa mwaka mmoja utakao kuwa unawawezesha kusimama upya kama watu wengine katika jamii.Mradi huu unaoendelezwa baada ya kutekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja hapo 2011-2012.Moja kati ya matunda ya mradi kwa kipindi cha utekelezaji cha 2011-2012 ni kuwezesha wasichana (kinamama wadogo) 20 kuwa na miradi ya kiuchumi iliyochangia kujiwekea akiba ya sh 1,200,000 benki inayosubili kujenga uwezo wa wasichana wengine zaidi. Wasichana (wamama wadogo) 8 na mratibu wa mradi wameuhudhuria mafunzo ya siku 6 jijini Arusha kupata mafunzo zaidi ya namna ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika kutekelezaji wa mradi huu kwa kipindi kilichopita. Katika kipindi cha siku 10 zijazo wasichana 60 (20 wanaoendelea na 40 wapya) watapata nafasi ya kuwezesha mafunzo ya stadi za maisha na stadi za ujasiliamali kabla ya kupewa mitaji kwaajili ya kuanzisha na kuendeleza biashara walizo/watakazoziibua katika maeneo yao kama hatua/shughuli moja wapo ya mradi huu. Katika kipindi cha utekelezaji cha 2013-2014 mradi huu utaendelea katika kata za Azimio,Mtoni na Kibada na unategemea kuwanufaisha wasichana wa waliofanya vizuri katika kipindi kilichopita na wasichana wengine wapya. "Nawakaribisha sana wasichana ambao wamezaa chini ya miaka 20 kujiandikisha kwa wingi kwa watendaji wa mitaa na kata katika zilizotajwa hapo juu ili waweze kusailiwa na kuandikishwa katika orodha ya wanufaika wa mradi" anasema mratibu wa mradi bwana Yusuph Kutegwa.
|
WALIOZAA GIRLS UNDER THE AGE OF 20 YEARS AND ENVIRONMENTAL who are in RISKY get another chance to be trained and capital so that they can sustain life. TEYODEN has cognitive activity of girls who are at risk who also have bear under the age of 20 so they can be beneficiaries of the project a year that will be enabled to stand revised as others in jamii.Mradi This developed after exercised for a period of one year when 2011-2012.Moja between the fruits of the project implementation period of 2011-2012 is to enable girls (young women) 20 have economic projects contributing savings bank shs 1,200,000 inayosubili build the capacity of most other girls. The girls (young women) 8 and coordinator of the project have recently attended training 6 days in Arusha to get more training on how to deal with the challenges faced in the implementation of this project for the previous period. In the past 10 days later girls 60 (20 who continued with 40 new) will have the opportunity to facilitate the learning of life skills and skills for entrepreneurship before receiving capital in favor of establishing and developing business what they / will kazoziibua in their areas as a step / activity one this project. In the period 2013-2014 the implementation of this project will continue in the county of the resolution, and both river and predominantly benefit girls who have done well in the past with other new girls. "I invite the girls who give birth under the age of 20 to register for the bulk of local and county officials in the above so that they questioned and registered in the list of beneficiaries of the project" says project coordinator Mr Yusuf tripped. |
Translation History
|