Base (Swahili) | English |
---|---|
Sababu kuu nne ‘zinazowatafuna’ wakulima wa korosho nchini.
MKOA wa Mtwara umezungukwa na Bahari ya Hindi, na eneo la nchi kavu kuna miti ya mikorosho iliyopandwa tangu enzi ya wakoloni. Ni moja ya mikoa nchini inayowavutia watu wengi wakiwamo wawekezaji, hasa baada ya Serikali kuanza kuchimba gesi na kubadilisha mfumo wa kuuza zao la korosho na kuwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani. Korosho ndilo zao kuu la biashara katika mikoa ya Pwani, Lindi, Ruvuma na Mtwara. Kwa Mtwara, mkoa huo umekuwa maarufu zaidi baada ya wataalamu kueleza kwamba panapochimbwa gesi pia mafuta yanapatikana. Ndiyo maana hivi sasa ukifika katika mkoa huo, moja ya mambo yanayozungumzwa na wananchi, ni gesi kuhamishiwa mkoani Dar es Salaam na kuyumba kwa soko la korosho nchini. Msingi wa makala haya ni kuzungumzia mambo yanayosababisha kuyumba kwa soko la korosho. Kwa mfano, makala haya yanauliza, Kwa nini soko la korosho linayumba? Baadhi ya wakulima katika wilaya za mkoa huo kwa nyakati tofauti, wanasema soko la korosho linayumba kwa sababu mfumo wa stakabadhi ghalani umeingiliwa na watu wanaosimamia maslahi yao badala ya wakulima. Wanasema mambo yanayosababisha kuyumba kwa zao la korosho ni vyama vya msingi kutokuwa na mtaji wa kununua korosho kutoka kwa wakulima, baadhi ya wafanyakazi wa serikali kuhusika kuwakandamiza wakulima, mgomo baridi wa wafanyabiashara na madeni kutoka vyama vya msingi. Sababu hizo zimechangia wakulima wa korosho kutonufaika na kilimo hicho, na pia kusuasua kwa vyama vya ushirika ambavyo havina mtaji kwani navyo vinategemea fedha kutoka kwa wakulima hao Kwa mfano, chama cha ushirika cha msingi cha wilaya kinachukua Sh50 katika kila kilo moja ya mkulima ikiwa ni gharama za uendeshaji. Katika makato ya Sh50 kwa kila kilo, msimu wa korosho mwaka wa mwaka jana (2011/2012) wilaya ya Newala na Tandahimba waliuza kilo 64, 124, 110 kwa wanunuzi na kupata jumla ya Sh76.5 bilioni. Kwa hoja hiyo ikiwa utazidisha kilo za wilaya hizo zilizouzwa kwa Sh50, hakika vyama vya ushirika vilikusanya fedha nyingi. |
Four main reasons 'zinazowatafuna' cashew farmers in the country.Mtwara Region is surrounded by the Indian Ocean, with an area of land planted cashew trees since the days of the colonists. It is one of the regions in interesting way many people, including investors, especially after the government started drilling the gas and transform their system to sell the cashew and document storage system. Cashew is a staple business in coastal regions, Lindi, Ruvuma and Mtwara. In Mtwara, the region has become more popular after experts explain that panapochimbwa gas oil also available. That is why right now you come to the region, one of the things spoken by the people, it is transferred to the gas in Dar es Salaam and the cashew market instability in the country. Based on these articles are talking about things that cause instability in the cashew market. For example, this article asking, Why cashew market rates? Some farmers in the districts of the province at different times, say the cashew market rates for documents storage system was interrupted by people in charge of their own interests rather than farmers. They say things that cause instability in the cashew is their primary societies lack of capital to buy cashew nuts from farmers, some government employees involved oppressing peasants, cold strike of traders and liabilities from primary societies. These factors have contributed to the cashew farmers and agricultural kutonufaika period, and also sluggish for cooperatives that have no capital because they depend on money from the farmers For example, a cooperative association of the district's primary accounts Sh50 per kilogram of farmer as operating costs. In contributory Sh50 per kg, cashew season in the last year (2011/2012) and Tandahimba Newala district sold 64 kg, 124, 110 for buyers to get a total of Sh76.5 billion. By the same reasoning, if you multiply the district kilo sold for Sh50, certainly cooperative reassembled money. |
Translation History
|