Asili (Kiswahili) | English |
---|---|
Hivi karibuni shirika la KIOO lilifanya ufuatiliaji wa shughuli zake katika kata ambazo mradi wa ufuatiliji wa uwajibikaji kijamii unapofanyika. Katika ufuatiliaji huo ilibainika kuwa pamoja na kwamba serikali imeridhia suala la kupereka madaraka kwa umma kwa kutumia njia ya D by D bado hali ya watendaji huko chini inatia mashaka.Mfano katika kata ya Nguruka kijiji cha Nyangabo na Bweru havina ofisi za watendaji wa vijiji jambo ambalo limeperekea nyaraka mbalimbali za serikali kutunzwa nyumbani kwa mtu yaani nyumba aliyopanga mtendaji wa kijiji husika. Hali hii imeperekea wanaokaimishwa kazi za utendaji wa kijiji kushindwa kuwa na nyaraka mhimu kwa ajili ya kijiji maana zinatunzwa nyumbani kwa mtu. Hali kama hiyo pia imejitokeza katika kijiji cha Mwamila kata ya Uvinza ambapo nyumba anayoishi mtendaji ndiyo ofisi ya kijiji na cha ajabu sana eneo hilo halina hata choo, hali inayotia shaka juu ya usalama wa watumishi hao wa serikali kiafya. Kwa mjibu wa sheria ya serikali za mitaa Na 6 mtendaji wa Kijiji ndiye kiongozi mkuu wa watendaji wengine wa idara za serikali kijijini, mtu huyu ambaye ni kiongozi wa wengine hana ofisi na wala hana cho hivi kweli ni rahisi kwake kuwaongoza wengine kutimiza wajibu wao? |
Recently KIOO organization was monitoring her activities carried out in the wards where the project of social accountability is conducted. During the monitoring it was found that although the government has ratified the issue of public power using the D by D state officials still at the bottom bolsters in the county and forexamples Nyangabo and Bweru villages in Nguruka are not having village executive offices of the villages which resulted into various government documents to be kept at home for a house plan that is managing the village concerned. This lead into poor performance and the village failed to document important for the village kept centrally at home for someone. A similar situation happened in the village of Mwamila Uvinza ward where the house in which he lives is the executive office of the village and a wonderful area it is even having no toilet, a worrisome situation on the security of the state health ministers. For him the law of the local village and six executive and head of the other actors of the village government departments, the man who is head of the office and not others does not have this really easy for him to lead others to fulfill their obligation? |
Historia ya tafsiri
|