1. Katika kuzuia wimbi la vijana kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ,Tosa inatoa elimu kwa vijana jinsi ya kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya madawa ya ikishirikiana na wadau mbalimbali.
2 Tosa inawasaidia watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi kuendelea na masomo kwa kuwapa sare za shule na vifaa vya shule mara 2 kwa mwaka
3.Kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajane, vijana na walezi wa watoto ili waweze kutumia raslimali walizonazo kuboresha maisha yao.
4.Tosa inatoa semina kwa waalimu wa shule za msingi ili kugundua mabadiliko ya tabia za watoto wanaishi katika mazingira hatarishi ili kuweza kwasaidia na kuwapa ushauri.
5.Tosa inafanya mradi wa mama na mtoto kwa kushirikiana na shirika la tandabui healthaccess Tanzania ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 katika kutoa elimu kwa jamii katika wilaya ya nyamagana kupitia kwenye zahanati na mikutano ya jamii.
6.Tosa inatoa elimu juu ya mabadiliko ya tabia katika vita dhidi ya malaria katika wilaya ya nyamagana kwa kushirikiana na shirika la tandabui la mwanza na mtandao wa kuthibiti malaria- tanam dar es salaam.
7. Tosa inatoa elimu ya makuzi kwa watoto ili kuwaanda ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya mwili kupitia vikundi vya watoto na michezo