Injira
TANZANIA SCIENCE JOURNALIST ASSOCIATION

TANZANIA SCIENCE JOURNALIST ASSOCIATION

DAR ES SALAAM, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations

Iran kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Sayansi

Elizabeth Mlay (kulia kwa waziri ) mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Dk. Mohammad Baqer Khorramshad

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu ICRO amesema ustawi wa kipekee wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa kisayansi ni mfano mzuri wa kuigwa na nchi za Kiafrika.

Dk. Mohammad Baqer Khorramshad alisema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Tanzania Profesa Makame Mbarawa,

Alisema ustawi wa kasi wa Iran katika uga wa sayansi na teknolojia ni natija ya juhudi na ubunifu wa wasomi na wanasayansi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha amesisitiza kuhusu azma ya ICRO ya kuimarisha uhusiano na Tanzania na kuongeza kuwa shirika hilo litatoa msaada wa masomo kwa wanafunzi 7 wa Tanzania bara na watatu kutoka Zanzibar.

Khorramshad aidha ameashiria uwezo wa Iran katika sekta kama vile utamaduni wa Kiislamu, ustaarabu, nano teknolojia, mawasiliano ya satalaiti na kilimo na kusema Iran iko tayari kubadilishana uzoefu wake huo na Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Tanzania Profesa Makame Mbarawa amesisitiza azma ya nchi yake ya kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Alisema kwa kuzingatia mahitajio mengi ya Tanzania katika sekta mbali mbali, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaweza kuwa chanzo kizuri cha kupata uwezo wa kisayansi.

 

large.jpg

Viongozi wa Kamati ya Utendaji ya TASJA wakiwa katika p;icha ya pamoja

TASJA yapata viongozi wapyaMgeni Rasmi akifungua Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Uchaguzi wa TASJA, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda, akitoa hotuba ya ufunguzi, kushoto ni Meneja Mkuu wa Biashara na uwakala wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kilala Sendama.Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TASJAMjumbe wa Mkutano Mkuu wa TASJA, na Katibu Mtendaji Mstaafu, David Ramadhan akichangia hoja katika mkutano wa uchaguzi.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Waandishi wa habari za Sayansi nchini (TASJA), kimepata viongozi wapya watakiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo

Waliochaguliwa ni Pamoja na Greyson Mutembei, ambaye ni Mwenyekiti mpya, Bakari Kimwanga Makamu Mwenyekiti, Benard Lugongo Katibu Mkuu na Nasra Abdallah Mweka hazina.

Mbali mkutano huo umewachagua wajumbe wa kamati ya utendaji ambao ni David Ramadhan, Asia Rweymamu, Gabriel Mushi, Restusta James, Jackob Nduye na Hamis Shimye.

Awali akifungua mkutano Mkuu huo wa mwaka, mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda, alisema ili nchi iweze kuendelea inahitaji wanasayansi na wabunifu wengi ambao wataleta maendeleo nchini.

“Tunajua TASJA kwa namna mlivyo mnaweza mkawa chachu ya maendeleo katika sekta ya Sayansi nchini, nasi kama wadau wakuu tunaamini waandishi wa habari mna mchango mkubwa katika wakuelimisha wananchi.

“Ahadi yangu kwenu TASJA kupitia COSTECH mnafika mbali sambamba na kuwaunganisha na taasisi zingine kimataifa,” alisema Dk. Mshinda

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Biashara na uwakala wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kilala Sendama, alisema kuwa hivi Maendeleo ya teknolojia za mawasiliano yamejkuwa yakichukua nafasi kubwa katika maendeleo ya Taifa.

“Kwetu TPC tumejiandaa katika kutoa huduma zatu ikiwemo EMS, Post Cargo na Inateranet ambayo imekuwa ikitumiwa na watanzania wetu nanyi TASJA ni moja ya wadau wetu,”alisema

large.jpg

Katibu Mktendaji mpya wa TASJA Bernard Lugonga, akikabidhiwa vifaa vya kazi na Katibu Mtendaji mstaafu David Ramadhan, wengine wanaoshudia ni baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ya TASJA

large.jpg

Timu ya Viongozi wa TASJA ikiwa katika picha ya pamoja, kulia ni Mwenyekiti wa TASJA Grayson Mutembei pamoja na Katibu Mtendaji wake Bernard Lugongo, waliosimama ni Makamu Mwenyekiti Bakari Kimwanga na Mweka hazina Nasra Abdallah

small.jpg

FEMALE STUDENTS WORKING ON THE MACHINERY EQUIPMENT

small.jpg

FEMALE STUDENT IN THE LAB