Napenda kueleza machahche kuhusiana na Hali ilivyo kuhusu HIV/AIDS kwenye shule za Sekondari na Vyuo mbalimbali vya Ualimu hapa nchini Tanzania.
Nazungumzia jambo hili kwa sababu msisitizo kwa Vijana hawa upo kwenye Elimu ya Compyuta na Masomo ya Sayansi, lakini HIV/AIDS haihusishwi. Kutohusishwa inaonekana hawajengewi moyo wa Maisha ya Baadae,jambo ambalo mara wanapofuzu Taaluma yao wanaonekana tayari wana VVU lakini pia hawapendi kupangiwa kazi maeneo ya Mbali na mjini kwani wengine wanajihisi vibaya na hali wakiyonayo. Hii ipo sambamba na magonjwa ya zinaa kwani KITU MAPENZI kinawasumbua sana vijana hawa.
Ninachoshauri Mashirika mbalimbali, Walimu wa Ushauri nasaha na Wataalamu wengine wa Afya fanyeni juhudi za Makusudi ili Rika hili wawe na Subira ya Mapenzi kwani kila jambo lipo mbele yao.