@NG'ONYE JOHN (Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Kitangari.):
Vizuri sana John;Nafikiri watu wanahamu kubwa ya kupata dawa ya ugonjwa huu;hasa wale ambao wameshaathirika ndio maana watu wengine (siyo babu wa loliondo) wanatumia njia ya kujipati fedha wakijua kwamba dawa haitibu lakini watu watanunua na pesa itapatikana kwa biashara hiyo.)angalia jinsi vikombe vilivyoongezeka hivi karibuni),mara cha bibi,mara cha nani;siwalaumu hii yote ni kwa sababu ya umasikini wa muda mrefu na bado wana hamu ya kufikia malengo yao au maisha bora.
Hivyo ni vizuri tufanye utafiti kwanza kabla ya kukubaliana na jambo nyeti kama hili la dawa ya ukimwi.
Kwa ujumla kwa maoni yangu maabukizi yamepungua hasa kutokana na watu kuhamasika kutumia kinga lakini kutoa taarifa kila mwezi inakuwa ngumu kwani watanzania wa sasa tumepoteza uzalendo kila mtu awe mtumishi wa uma au la anataka ajipatie kipato kwa lolote anlofanyo hajali wananchi wenzake.
Nashauri watu wenyewe pamoja na taarifa wajithamimi na kujilinda dhidi ya ugonjwa juu