Fungua
Society for Women and AIDS in Africa

Society for Women and AIDS in Africa

Misufini mtaa wa police, Tanzania

large.jpg

Msichana huyu anaesoma katika Shule ya Sekondari ya Mziha kata ya MZIHA shule iliyopo Tarafa ya Turiani, ni mmoja wawasichana ambao alieleza viongozi wa shirika hili athari ya kukaa mbali na kuwa wapo hatarini, katika kubakwa kwani wanafika nyumbani kwao usiku na huwa wanondoka asubuhi sana nyumbani kwao na kufanya muda wao mwingi kuishia njiani kwa kutembea kwa miguu au kuomba lifti za pikipiki na baiskeli. Wanafunzi wengine wanatoka zaidi ya kilomita tano kwenda na kurudi shuleni.Mfano msichana huyu anatoka Difinga mwisho kijiji kilicho katika Msitu wa hifadhi kandokando ya MLIMA NGUU. Ushauri wao ni kuwa kama wangepata nyumba ya kulala Hostel wangesoma vizuri sana kutokana na kuwa shule yao ipo mahali pazuri kielimu.

8 Aprili, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.