Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

large.jpg

Wanafunzi wa Sekondari ya Mziha wakisikiliza mragibishi akitoa elimu ya usafi na Uzazi kwa wanafunzi wa kike na wakiume mwezi wa tatu mwaka 2012 kama mpango wa kuelimisha jamii.

large.jpg

Kikundi hiki kinaitwa Mbeta Group huwa kinafanya kazi ya kutoa mafunzo mbalimbali kwa njia ya sanaa na ngoma yao ya Mbeta. Ngoma hii ni asili ya Kabila la waluguru ambao huishi mlimani. vifaa anavyotumia ni mianzi ya kupuliza ambayo hutengenezwa kwa ustadi na kutoa sauti saba yaani DO RE MI FA SO LA TI DO. Shirika hili wanafanya nao kazi kwa kutoa elimu katika jamii hasa ya UKIMWI na kukemea mila potofu kama vile kuwaoza wasichana kabla ya umri.

large.jpg

Msichana huyu anaesoma katika Shule ya Sekondari ya Mziha kata ya MZIHA shule iliyopo Tarafa ya Turiani, ni mmoja wawasichana ambao alieleza viongozi wa shirika hili athari ya kukaa mbali na kuwa wapo hatarini, katika kubakwa kwani wanafika nyumbani kwao usiku na huwa wanondoka asubuhi sana nyumbani kwao na kufanya muda wao mwingi kuishia njiani kwa kutembea kwa miguu au kuomba lifti za pikipiki na baiskeli. Wanafunzi wengine wanatoka zaidi ya kilomita tano kwenda na kurudi shuleni.Mfano msichana huyu anatoka Difinga mwisho kijiji kilicho katika Msitu wa hifadhi kandokando ya MLIMA NGUU. Ushauri wao ni kuwa kama wangepata nyumba ya kulala Hostel wangesoma vizuri sana kutokana na kuwa shule yao ipo mahali pazuri kielimu.

large.jpg

Mr. kervin kutoka (The Faundation For Civil Society) akiwapa maelekezo wawakilishi wa asasi ya (SWAA-MO).

large.jpg

Mr. kervin kutoka (The Faundation for Civil Society) akiandika maelezo kutoka kwa viongozi wa (SWAA- MO).

large.jpg

picha ya pamoja ya viongizi, wajumbe wanachama na mwakilishi kutoka (The Faundation for Civil Society) baada ya mkutano.

large.jpg

Mwenyekiti wa SWAA akitoa mafunzo ya mada kuhusu elimu ya ukimwi na afya kwa mtoto wa kike katika shule ya sekondari Mnziha 2011.

large.jpg

Cheti usajili shilika la SWAA

large.jpg

watoto waliopata mavazi katika shule ya msingi kisaki kituoni wilaya ya morogoro vijijini kwa ufadhili wa TAKIAIDS 2008.