Log in
Sauti ya wakulima

Sauti ya wakulima

Bagamoyo, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

(English below)

Sauti ya wakulima, "The voice of farmers" (http://sautiyawakulima.net), ni msingi wa kuelimishana ulioundwa na wakulima wa eneo la Chambezi Wilayani Bagamoyo-Tanzania. Msingi huu wa kuelimishana umeundwa kwa kukusanya ushahidi wa picha za shughuli zinazofanywa na wakulima kila siku na rekodi za sauti zao kisha kurekodiwa kwa kutumia ‘smartphones’ na kuchapishwa kwenye mtandao.

Washiriki wa Sauti ya wakulima ni kundi la wanaume watano na wanawake watano ambao hukusanyika kila Jumatatu katika kituo cha kilimo kilichopo Chambezi. Wao hutumia kompyuta ndogo iliyounganishwa na mtandao wa mawasiliana wa 3G ili kuona picha na kusikiliza sauti zilizorekodiwa na kuchapishwa kwenye mtandao kwa kipindi cha wiki hiyo. Wao pia hukabidhi ‘smartphones’ mbili zilizopo katka kikundi toka kwa washiriki fulani kwenda kwa washiriki wengine, ili nao waweze kuzitumia kama zana za mawasiliano kati yao. Smartphones hizi zimeunganishwa na vifaa vingine kama vile viunzi huru vya GPS na vibandiko vingine ambavyo kwa pamoja hurahisisha utumaji wa picha na sauti kwenye mtandao. Wakulima hawa wa Chambezi huzitumia ‘smartphone’ hizi kurekodi/kuratibu shughuli zao za kila siku, kutoa taarifa juu ya masuala yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na pia kufanya mahojiano na wakulima wengine, hivyo kupanua mtandao wa mahusiano ya kijamii kati yao.

Mbali na kupambana na ubovu wa miundo mbinu/kutokuwa na miundo mbinu ya kutosha na na hali ya kutokuwa na masoko ya huhakika kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao, wakulima wa Chambezi pia wanakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. Pamoja na hayo, uhaba wa mvua, uhaba wa maji yanayopatikana chini ya ardhi na vitisho visivyo na kifani vivyosababishwa na wadudu na magonjwa ya mimea ni miongoni mwa masuala makubwa ambayo wakulima hawa wanalazimika kushughulikia. Hata hivyo, wakulima hawa wanatambua ya kuwa kwa kushirikishana maarifa wanayotumia katika kukabiliana na matatizo haya wanaweza kuwa na nguvu na kutafuta njia mbadala za kukabiliana nayo. Pia wakulima hawa wana matumaini kwamba, kwa kuwasilisha uchunguzi wao kwa maofisa ugani na watafiti wa kisayansi ambao wapo mbali nao wanaweza wakashirikiana nao katika kubuni mbinu mpya kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo. Wanataka sauti zao kusikika; wanayo mengi sana ya kuzungumza/kusema.

---

Sauti ya wakulima, "The voice of the farmers" (http://sautiyawakulima.net), is a collaborative knowledge base created by farmers from the Chambezi region of the Bagamoyo District in Tanzania by gathering audiovisual evidence of their practices using smartphones to publish images and voice recordings on the Internet.

The participants of Sauti ya wakulima, a group of five men and five women, gather every Monday at the agricultural station in Chambezi. They use a laptop computer and a 3G Internet connection to view the images and hear the voice recordings that they posted during the week. They also pass the two available smartphones on to other participants, turning the phones into shared tools for communication. The smartphones are equipped with GPS modules and an application that makes it easy to send pictures and sounds to the Internet. The farmers at Chambezi use them to document their daily practices, make reports about their observations regarding changes in climate and related issues, and also to interview other farmers, expanding thus their network of social relationships.

The farmers at Chambezi not only struggle because of insufficient infrastructure and unreliable markets for their products, but they are also facing the challenges of a changing local climate. Less rains, less underground water and unprecedented threats caused by pests and plant diseases are some of the pressing issues that they have to deal with. However, they know that by sharing their knowledge on how to cope with these problems, they can become stronger and find ways to overcome them. They hope that, by communicating their observations to extension officers and scientific researchers, who can be in remote locations, they can participate in the design of new strategies for adaptation. They want their voices to be heard: they have so much to say.

Latest Updates
Sauti ya wakulima added a News update.
October 10, 2011
Sauti ya wakulima created a Team page.
Shukrani kwa:Wakulima: Abdallah Jumanne, Mwinyimvua Mohamedi, Fatuma Ngomero, Rehema Maganga, Haeshi Shabani, Renada Msaki, Hamisi Rajabu, Ali Isha Salum, Imani Mlooka, Sina Rafael ... Read more
October 10, 2011
Sauti ya wakulima joined Envaya.
October 10, 2011
Sectors
Location
Bagamoyo, Pwani, Tanzania
See nearby organizations