Tunapo jadili swala la maadili sitahiki katika jamii, ili kuboreha/kustawisha maendeleo ya binadamu lazima tuelewe kuwa kuna mambo mengi yanayo simamia ujenzi wake. katika hali yoyote iwayo sirahisi kudumisha maaddili katika jamii yoyote ambayo hakuna usawa na haki katika mambo mbalimbali.Aidha ni shida kubwa kusimamia maadili katika jamii, jamii ambayo haitambui kazi kuwa ni jambo la lazima. kwani kupitia kazi ndiko ustaarabu wa binadamu hupatikana, kwa kuwa kazi ndiyo hufanya uwepo wa mambo mazuri.Mtazamo wangu jamii ichukue hatua katika kuhakikisha watu wanafanya kazi kwa bidii kwa kuwa kazi itasadia katika kudumisha maadili.Mahali penye shida mbalimbali ni vigumu kusimamia maadili, katika nchi yetu sasa tunashuhudia nguvu kazi kubwa ikipotelea barabarani na kwenye vijiwe kwa shughuli zisizo na tija, kama nchi sasa ni lazima tuchukue hatua za dhati kukabiliana na hali hii, vinginevyo tutaendelea kulalamika kuwa hakuna maadili katika nchi.'TUSIWAONEE AIBU WATU WASIO THAMINI NA KUFANYA KAZI'