"SOMA KWA MALENGO" ,HII NI KAULI MBIU TULIYOANZA NAO KWA MWAKA HUU .PEACE AND HOPE FOR YOUTH DEVELOPMENT (PHY):MWAKA JANA 2012 TUMEJITAHIDI KUTEMBELEA SHULE MBALIMBALI HAPA WILAYANI KARAGWE, TULIBAINI WANAFUNZI WENGI WANASOMA BILA KUJIWEKEA MALENGO KWA UPANDE WA "ORDINARY LEVEL"( O`LEVEL ) KWA UPANDE WA A`LEVEL MAMBO YALIKUWA NI TOFAUTI KIDOGO MAANA HAWA WANAFUNZI WA "ADVANCED LEVEL(A`LEVEL) WAN ASEMA WANA`FOCUS` KWAMBA WANALENGA AU WANAANGALIA CHUO KIKUU MOJAKWAMOJA NA HALI YA KUVUNA WANACHOPANDA NI JAMBO LINALOWATIA NGUVU NA UJASIRI WA KUSOMA KWA BIDII ZAIDI ,KWAMBA HAWANA WASIWASI WANALO TUMAINI KWA LILE WALIFANYALO, PIA NA UMRI IMEONEKANA NI KIGEZO, KWAMBA HAWA WANAFUNZI WANAELEKEA UTU UZIMA HIVYO MAAMUZI WANAYOFANYA YA KUSOMA KWA BIDII WANAYASIMAMIA KIKAMILIFU NA KWA UJASIRI ILI WAFIKIE MALENGO YAO.
HALI HII NI TOFAUTI KWA VIJANA WANAOSOMA KIDATO CHA KWANZA HADI NNE,(O`LEVEL) WAO INAVYOONEKANA NA NDIVYO ILIVYO INAONESHA BADO HAWAJAJITAMBUA KIKAMILIFU HUSUSANI KUJUA KWA NINI WANASOMA ,HAWAJALITAMBUA JAMBO HILI KWA VITENDO ,BADO WANALO KWA NADHARIA , WANAJIKUTA WANACHANGANYA MAMBO MENGI NA WANAJIINGIZA KATIKA MAMBO MENGI NA MENGINE YA KUHARIBU MAISHA YAO.
ASASI MBALIMBALI ZINAZOHUSIKA NA ELIMU SHULENI KWA VIJANA KATIKA KUELIMISHA MAMBO YAFUATAYO YATILIWE MKAZO ILI KUFANIKISHA MALEZI NA HATIMAYE KUWAFANYA VIJANA KUFIKIA MALENGO YAO;
- KUWAJENGEA UWEZO KUTAMBUA UMUHIMU WA ELIMU
- UCHAMBUZI WA KITU GANI WASOME ILI KUAMUA USAHIHI WA MASOMO ATAKAYOSOMA AFIKAPO KIDATO CHA TANO
- AWAPO SHULENI ANAJUA NI KITU GANI ANATAKIWA KUSOMA? PAMOJA NA KUMTEGEMEA MWALI MU AMJULISHE HICHO KITU ,JE YEYE AMEWEKA JUHUDI GANI KUHAKIKISHA ANAKUWA NA UFAHAMU WA KITU HICHO KINACHOTAKIWA KWA DARASA
- MUDA WAKE ANAUTUMIA VIZURI AWPO SHULENI AU AMECHANGANYA MAMBO MENGINE KATIKA MUDA WA KUWA SHULENI
- AMEAMUA KIKAMILIFU KUSOMA KUTOKA MOYONI MWAKE NA KUWEKA NIA MOJA KATIKA HILOAMESHATAMBUA KWAMBA KATIKA ELIMU AMEWEKEZA ,HIVYO INAMPASA KUSOMA KWA MALENGO ILI AFANIKIWE MAANA HAKUNA ANAYETEGEMEA HASARA AFANYAPO KAZI YOYOTE.
- AMEHESABU GHARAMA,HAPA SIONGELEI GHARAMA YA KULIPIA ELIMU. LA! TUNATAMBUA MTU ANAPOTAKA KUJENGA NYUMBA UKAA CHINI AKAPIGA HESABU KUONA JE ANAYO FEDHA YA KUJENGA ASIJE ISHIA NJIANI WATU WAKAMCHEKA, KWAMBA ALIANZA KWA NGUVU ONA SASA AMESHINDWA KUTIMIZA LENGO LAKE,VIVYO HIVYO NA VIJANA WETU INAWAPASA KUTAMBUA ,JE WAMEHESABU GHARAMA. HII NI PAMOJA NA UVUMILIVU KWA KIPINDI CHA MIAKA YA KUWA SHULENI.
- UVUMILIVU ULIOJAA TUMAINI ,TUMEONA WENGINE WANAKUWA NA UVUMILIVU USIO NA TUMAINI NDANI YAKE, MFANO UNAWEZA KUKUTA KIJANA AMBAYE AKUENDELEA NA MASOMO AMEMUA KIJIINGIZA KWENYE BIASHARA AU KILIMO ENDELEVU KWA KIASI FULANI AKAPATA VIJISENTI KWA NJIA HIYO AU NYINGINEYO, SASA HUYU MWANAFUNZI KWA KUONA MWENZAKE ALIYEMALIZA NAYE KUMWONA JINSI ALIVYOMILIKI BAADHI YA VITU, ANAANZA KUWAKA TAMAA NA KUPUNGUZA SPIDI KATIKA MASOMO ILI ATAFUTE LKIDOGOKIDOGO ILI NAYE AMILIKI BAADHI YA VITU, KUPITA HAPO UNAKUTA TAYARI AMEHARIBU MFUMO WAKE WA KUSOMA,ANAWEZA KUSHINDWA KABISA AU KUWA NA UFAULU HAFIFU KATIKA ELIMU YAKE.
- UCHAGUZI WA MARAFIKI PIA NI KITU KINGINE AMBACHO KIMEPOTEZA WANAFUNZI WETU, MCHANYIKO WA WATU KATIKA JAMII KWA TABIA TOFAUTI NA KAZI MBALIMBALI ,WAHUSIKA WAMEKOSA NIDHAMU KWA MFUMO WA MAISHA YAO .
- MFUMO TULIO NAO WA MAISHA KWA SASA NI TOFAUTI NA MIAKI 10 ILIYOPITA, MFUMO WA DUNIA KUWA KIJIJI UMECHANGIA WATU WA RIKA ZOTE KUANGALIA NA KUFAHAMU MAMBO MENGI KWA WEPESI, YPO YALIYO MAZURI YANAYOJENGA LAKINI YAPO MENGINE YANAYOBOMOA ,KUHARIBU NA KUHATARISHA MAISHA YA MHUSIKA MMOJAMMOJA. MFANO LEO HII TUMEONA WATOTO WADOGO WANAJIINGIZA KWENYE UHUSIANO WA KINGONO KWA UASHERATI NA UZINZI NA UMRI MDOGO,WAKITAKA KUJARIBU MAMBO MBALIMBALI YAWEZEKANA WAMESHAWISHIWA NA WENZAO AU WAMEONA MOJAKWAMOJA, KATIKA HILI VIJANA WENGI WAMEKOSA MAJIBU SAHIHI NA UKWELI WA MAMBO JAMBO AMBALO WAMETUMIA AKILI ZAO KUUTAFUTA UKWELI ,NA WAMEFIKIRI WAMEUPATA UKWELI KUMBE SI SAHIHI NI UONGO ,HATIMAYE WAMEHARIBU UFAHAMU WAO WA KUFIKIRI,MTAZAMO WA MAISHA YAO YA BAADAE NA WENGINE KUHARIBU MIILI YAO KWA UONGO WALIOUONA NA KUDHANIA NI UKWELI KWA AKILI YAO YA CHANGA. ASASI NA NGO NA WALEZI WENGINE KATIKA HILI MSIWE KIMYA ,NYAKATI HIZI NI TOFAUTI NA ZAMANI,EBU ONGEA UKWELI NA ATHARI ZILIZOPO KWA MAMBO AMBAYO WANAYAANGALIA WATOTO WETU NA KUWAFANYA WAHARIBIKIWE MIFUMO YAO.
- WANAFUNZI KUJENGEWA UWEZO WA KUWA NA UAMUZI SAHIHI KATIKA SUALA LA UHUSIANO HASA WA KINGONO (UASHERATI NA UZINZI) SIWEZI KUYAITA MAPENZI KUTOKANA NA MFUMO WAKE. TUMEONA SUALA LA TAMAA KWA WANAFUNZI WETU LAKINI PIA NA KUTAKA KUJARIBU MAMBO WANAYOYAONA KUTOKANA NA UTANDAWAZI, WAJUE NA WATAMBUE WAO WENYEWE MAPEMA ISJE KUWA SIKUJA , HIVYO ELIMU ITOLEWE KWA USAHIHI BILA KUFICHA WALA KULEMBA,TAFSIDA ITUMIKE LAKINI UJMBE UENDE MOJAKWAMOJA KWA WALENGWA.
Comments (1)