1. Upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira katika maeneo tofauti ya Manispaa ya Lindi.
2. Utoaji wa Huduma kwa wagonjwa wa muda mrefu majumbani katika kata 13 za wilaya ya Lindi.
3. Utoaji wa Elimu ya afya ya msingi kwa jamii ili kupambana na magonjwa ya milipuko hasa Kipindupindu na malaria katika Manispaa ya Lindi.
4. Uchimbaji na ujenzi wa visima vifupi 4 vya maji katika kata 4 za; Jamhuri, Mitandi, Mtanda na Ndoro zilizopo manispaa ya Lindi.
5. Kujenga uwezo kwa waelimishaji rika 50 ngazi ya kata kwenye kata 5 kuhusu mbinu shirikishi jamii katika kupambana na VVU/UKIMWI katika Manispaa ya Lindi.
6. Kujenga uwezo kwa wakunga na waganga wa jadi 50 kuhusu jinsi ya kuandaa madawa ya asili yaliyo salama na jinsi ya kuwahudumia watu walioambukizwa VVU na wagonjwa wa UKIMIWI na magonjwa nyemelezi.
7. Kutoa lishe kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI wapatao 131 katika maeneo tofauti ya Manispaa ya Lindi.
8. Kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa unyonyeshaji maziwa mama watoto wa umri wa miaka 0-5 na akina mama wajawazito kuhudhuria kliniki na kupatiwa lishe bora katika vijiji 30 vya Lindi vijijini.
9. Kuelimisha na kuhamasisha wanaume kushiriki katika masuala ya uzazi wa mpango na mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa kuimarisha mahusiano katika familia kwenye kata 20 za Mikoa ya Lindi na Mtwara.
10. Kujenga uwezo kwa watoto ili kuwawezesha kufanya ushawishi na utetezi juu ya haki na usawa wa kiuchumi kwao kupitia mabaraza ya kata ya watoto kwenye kata 28 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini.
11. Kujenga uwezo kwa watu waishio na VVU/UKIMWI wapatao 180 katika kata 8 za Manispaa ya Lindi na Lindi vijijini ili kuelimisha na kuhamsisha jamii kupunguza unyanyapaa kwa watu waishio na VVU/UKIMWI.
12. Kuhakikisha usalama wa chakula kwa makundi ya watu walio katika hatari zaidi ya kuathirika na umaskini wapatao 18000 waliopo katika vijiji 10 vya kata 3 za Lindi vijijini.
13. Uelimishaji na uhamasishaji vijana kupiga vita UKIMWI na matumizi ya madawa ya kulevya katika kata 2 za Manispaa ya Lindi.
14. Kuboresha hali na afya za watu wanaoishi na VVU/UKIMWI katika kata 10 za Manispaa Lindi na Lindi vijijini.
15. Kuvijengea uwezo vikundi vya sanaa 2 vyenye jumla ya watu 30 ili kuhamasisha jamii kupambana na VVU/UKIMWI katika maeneo tofauti ya Lindi vijijini.