
Fadeco Community Radio (100.8 FM) ni kituo cha redio cha jumuiya katika wilaya ya Karagwe, mkoa wa Kagera. Fadeco inafanya kazi ya kuleta maendeleo ya vijijini kwa kuboresha upatikanaji wa habari na teknolojia ya mawasiliano.

ANPPCAN ni mtandao wa Afrika ambayo umekuzania haki za watoto na ulinzi wa watoto. Sura yake ya Tanzania imeanzishwa mwaka wa 1990, na kwa sasa inafanya miradi mikuu miwili wilaya ya Kisarawe na Mkuranga katika mkoa wa Pwani.

Shirika la CFP linafanya kazi kuhamasisha jamii kutunza mazingira, na kundeleza misitu ya asili katika kisiwa cha Pemba. Tangu 2006, shirika hili limesaidia jumuiya 14 kupanda zaidi ya miti 300,000 kwa matunda na kuni, na jumuiya nyingi imeona faida za mazingira kutoka upandaji wa miti.

Kutoka Arusha, Tanzania, CWCD inasaidia kuhakikisha kuwa wanawake na watoto wana haki zao za msingi. CWCD ilianzisha Albehije Frankosea shule ya msingi ili kusaidia watoto walio katika mazingira magumu, ambayo kwa sasa inasaidia watoto 109: mayatima, walemavu, na watoto wa mitaani.

Nuru Halisi inaelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu UKIMWI, madawa ya kulevya, utunzaji wa mazingira, na elimu kwa vikundi vya vijana na kinamama, na inawatafuta msikwao na kuwakutanisha na ndugu zao na kuwapa mbinu za kujitegemea.

JEAN-media inaunganisha CBOs na NGOs ili kusababisha mawasiliano na mabadiliko katika jamii juu ya VVU/UKIMWI na masuala ya mazingira.
Kuhusu Mashirika Maalum