Log in
Mzizi Cultural Troup

Mzizi Cultural Troup

Iringa, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Afya ya uzazi ni haki ya kijana je? tutaweza kuitetea kwa kutumia mazingira yetu ya asili?

Mzizi Cultural Troup (Iringa)
April 22, 2012 at 4:21 PM EAT

Kila uchao vijana wanahangaika katika kujikwamua na changamoto mbalimbali zinazowahusu. vijana wanapambana na matumizi ya madawa ya kulevya, ukatili wa kijinsia, changamoto mbalimbali za kielimu katika shule zetu, kasi ya maambukizi ya vvu nk.

katika nchi yetu vijana wanaongoza kwa zaidi ya asilimia 60% kwa kasi ya ongezeko la maambukizi ya vvu. hii inasababishwa na vijana wengi kukosa nafasi ya kujifunza kuhusu haki za afya ya uzazi na ujinsia ikiwemo changamoto za kiutamaduni zinazo ruhusu wazazi/walimu kuona aibu kuzungumzia hata kufundisha katika mashule/majumbani ikiwa sera na sheria zimetoa mwongozo wa kutoa mafunzo hayo kwa vijana!

Hali ya wazazi kuona aibu inasababisha vijana kushindwa kujitambua na kupelekea kudanganyika kirahisi na hata kuambukizwa vvu. 

kinakwamisha nini ikiwa sera na sheria zipo? hakuna njia nyingine zaidi ya kusimama kwa pamoja kutetea utekelezwaji wa sera na sheria zilizopo, lakini pia kuwahamasisha vijana kutengeneza chaguzi sahihi katika uwajibikaji wao juu ya afya zao na kuwasaidia kutambua mahitaji yao yanayoweza kuleta mabadiliko na maendeleo kwao na jamii kwa ujumla.

Tunaamini kuwa "AFYA YA UZAZI NI HAKI YA KIJANA... na kwa pamoja tunaweza kuitetea na "TUITEEE" sasa!

Stella (Iringa)
April 23, 2012 at 10:27 AM EAT

Safi sana vijana wa Mzizi........

Hongereni sana kwa hatua hii, yaonyesha ni jinsi gani ambavyo mko makini katika kutetea Haki za Afya zya Uzazi na Ujinsia kwa vijana wenzenu

Sijawasahau, hata ninyi pia mwajitetea kwani mnahusika moja kwa moja......

 

Kila kitu chawezekana penye nia .......

 

Haki za AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KWA KIJANA KUTETEWA ni muhimu kama kweli twahitaji vijana wenye kujiamini na kusimamia malengo ya maisha yao katika jamii na taifa letu kwa ujumla.

LAKINI, tujiulize, nini maana ya Haki,  Afya ya Uzazi na Ujinsia kabla ya kwenda popote:-

HAKI

Haki ni kitu ambacho mtu au watu wanaweza kukidai kisheria.

Mfano, Mtu ana haki ya kuishi, itokeapo kutishiwa kutolewa uhai huo basi ana uwezo wa kumshitaki mhusika kisheria

 

AFYA YA UZAZI

Ni hali ya mtu kuwa katika hali nzuri kimwili, kiakili na kijamii katika maswala yote yahusianayo na mfumo wa uzazi

Kimwili: Hana tatizo katika viungo vya uzazi au madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya viungo hivyo.

Mfano, magonjwa ya ngono, mimba za utotoni na VVU/UKIMWI.

Kiakili: Hana tatizo katika mfumo wake wa kiakili kutokana na maswala ya uzazi.

Mfano, Matokeo ya matatizo ya afya ya uzazi kama kuchanganyikiwa kutokana na kuwa na msongo wa mawazo sababu ya mimba za utotoni, magonjwa ya ngono na VVU/UKIMWI hasa pale wanapotengwa na jamii kwa ujumla au kujiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya na uuzaji wa miili sababu ikiwa ni hizo hizo

 

Kijamii: Hana tatizo lakutengwa na jamii kutokana na tatizo lililoletwa na matumizi hatarishi ya viungo vya uzazi.

Mfano, Kutengwa sababu ya kuwa na maambukizi ya magonjwa ya ngono, mimba za utotoni au VVU/UKIMWI.

 

UJINSIA

Mahusiano ya kijamii kati ya mwanaume na mwanamke au kijana na mtu mzima. Ni mahusiano yanayojengwa kutokana na utamaduni ambao umekubalika na jamii husika.

 

....... Siku nyingine ingekuwa vyema kama tutaweza kujadiliana juu ya Haki hizo za Afya ya Uzazi kwa vijana tukizichambua moja baada ya nyingine tukioanisha na mazingiraa yetu ya Kitanzania/kiasili....

Asante kwa nafasi....... Siku nyingine tena.....

 

 

 

 

 

 

AGENCY FOR BETTER HOPE AND SOCIAL UNITY[ABHASU]
April 30, 2012 at 1:56 PM EAT

@Mzizi Cultural Troup (Iringa): 

HAKI NA WAJIBU

Kijana anaye taka kupata haki ya afya ya uzazi ni lazima akumbuke kuwa ni wajibu wake kulinda afya pia. Wajibu wa kulinda afya ni wa kila mmoja wetu.

Dr Clifford Majan

ABHASU

Mzizi Cultural Troup (Iringa)
May 6, 2012 at 12:12 AM EAT

Naomba msaada kwenu wadau wa maendeleo na Afya hususani Afya ya uzazi na haki kwa vijana.

Vijana tupo katika hali mbaya ambayo mara nyingi hupelekea mimba za utotoni,watoto wasio tarajiwa na hata wengi wao kuishia kuwa watoto wa mitaani. ikumbukwe kuwa si wote wanaopata mimba wamekusudia kupata mimba.

Ulimwenguni kote kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Women Global Network for Reproductive Health (WGNRR) Makadirio ya zaidi ya mimba 41.6 milion duniani zinatolewa kila mwaka, katika hizo 21.6 milion hazitolewi kwa njia salama na kupelekea vifo kwa wasichana wadogo wasio na hatia. 95% ya utoaji mimba huu hufanyika katika nchi zinazoendelea. wasichana zaidi ya 47,000, hfa kutokana na utoaji mimba usio wa kisheria na salama.

 kwa hali hii katika nchi yetu . Ninajitoa muhanga kutetea Utoaji mimba salama iruhusiwe katika nchi yetu kisheria (tuipitishe kama inafaa)

Gasper Nsanye (IMC)
June 1, 2012 at 4:43 PM EAT

Haya bwana,tumeaona ila serikali yawezekana haiwatambui!Au mmefanya juhudi /nini kuijulisha serikali

Gasper Nsanye (IMC)
June 1, 2012 at 4:49 PM EAT

Karibu kwenye kilele cha siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16/06/2012? Hii pia itatangaza kazi zenu kwa umma hasa vijana au vipi? Unakaribishwa kushiriki kikao cha tarehe 4/06/2012 kwa ajili ya maandalizi ya siku ya mtoto wa Afrika.

martin salila-DACC (IMC)
June 1, 2012 at 4:58 PM EAT

Hongereni sana, pamoja na matatizo mliyo nayo njia pekee ya mafanikio msikate tamaa endeleeni kujitangaza na kushirikiana na asasi mbalimbali pamoja na mamlaka husika

Sezaria Andrew -RCHCCO (IMC)
June 1, 2012 at 5:05 PM EAT

Hongera mwanangu report yako ni nzuri sana nimeipenda, tupo pamoja tutasaidiana Ahsante sana

deo kipalile (iringa ilula)
January 19, 2015 at 12:38 PM EAT
hongela dr vijana tunapotea

Add New Message

Invite people to participate