Fungua
MTWARA NON GOVERNMENTAL ORGANIZATION NETWORK

MTWARA NON GOVERNMENTAL ORGANIZATION NETWORK

Mtwara Mjini na Vijijini, Tanzania

Wanachama wa MTWANGONET walio katika mradi wa Ukimwi na Jinsia wapo MASASI wakihudhulia mafunzo ya siku sita ya  Uendeshaji wa Shirika(Organizational Deveopment Training)

Mafunzo hayo yanalenga kuboresha utunzaji mzuri wa kumbukumbu za shughuli na miradi, upangaji mipango na utunzaji wa kumbukumbu za Fedha ili waweze kutekeleza mradi huu wa utetezi maswala ya Ukimwi na Jinsia lakini pia miradi mingine ambayo wataitekeleza. Akihojiwa na Afisa habari wa Mtwangonet Mwanyekiti wa Mtwangonet Bw. Saidi Ally Nassoro amewashukuru sana GIZ kwa kuwezesha wanachama wa Mtwangonet katika mradi huu pia yeye mwenyewe kama mshiriki wa Mafunzo hayo amesema kwa kweli mafunzo haya ni muhimu sana kwa Asasi zetu ili ziweze kusimama zenyewe "Mafunzo ni mazuri na wawezeshaji ni wazuri pia nawasisitiza viongozi wote wa Asasi zilizo katika Mradi huu zizingatie fursa hii Adimu" Alisisitiza Bw. Nassoro. Mafunzo haya yanaendelea katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Masasi Mjini mkoa wa MTWARA, TANZANIA.

16 Juni, 2011
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

Makoti Deo (Dar es salaam) alisema:
Hakuna taarifa mpya hapa embu tuwekeeni up to date katika mtandao huu ili tupate taarifa nzuri mpya.
5 Novemba, 2013

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.