MATANGAZO
- MTWANGONET inawatangazia viongozi wote wa ASASI kuleta mipango kazi ya Asasi zao katika ofisi ya MTWANGONET ili iweze kujumuishwa na ya Manispaa, mwisho tarehe 10/8/2011. kwa maelezo zaidi fika ofisini MTWANGONET siku na saa za kazi.
- Pia MTWANGONET inawatangazia viongozi wa Asasi zote kuja na kusoma tangazo kutoka T-MACK lililo katika mfumo wa barua, tangazo linataka asasi zinazotaka kuwa asasi kiongozi wa mradi wa FAMILY MATTERS mkoa wa Mtwara na Luvuma waombe, tarehe ya mwisho ni 29/07/2011 kwa maelezo zaidi fika ofisini MTWANGONET siku na saa za kazi.
- Wanachama wote ambao bado hamjamaliza au mnadaiwa ada za uanachama mnakumbushwa kulipa kama katiba inavyotaka.
PATA MAMBO WALIYOJIFUNZA WASHIRIKI WA MAFUNZO HUKO MASASI KUANZIA TAREHE 15-20 JUNE 2011.MAMBO_TULIOJIFUNZA_KATIKA_SEMINA_YA_GIZ_MASASI.docx
CHAC wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi. Deo Mtitu na Katibu wa Mtwara women living with HIV/AIDS(mwoliha) Bi.Mwanahamisi Bakari wakisikiliza kwa makini katika Mafunzo yanayoendelea mjini MASASI MTWARA TANZANIA.
Wanachama wa MTWANGONET walio katika mradi wa Ukimwi na Jinsia wapo MASASI wakihudhulia mafunzo ya siku sita ya Uendeshaji wa Shirika(Organizational Deveopment Training)
Mafunzo hayo yanalenga kuboresha utunzaji mzuri wa kumbukumbu za shughuli na miradi, upangaji mipango na utunzaji wa kumbukumbu za Fedha ili waweze kutekeleza mradi huu wa utetezi maswala ya Ukimwi na Jinsia lakini pia miradi mingine ambayo wataitekeleza. Akihojiwa na Afisa habari wa Mtwangonet Mwanyekiti wa Mtwangonet Bw. Saidi Ally Nassoro amewashukuru sana GIZ kwa kuwezesha wanachama wa Mtwangonet katika mradi huu pia yeye mwenyewe kama mshiriki wa Mafunzo hayo amesema kwa kweli mafunzo haya ni muhimu sana kwa Asasi zetu ili ziweze kusimama zenyewe "Mafunzo ni mazuri na wawezeshaji ni wazuri pia nawasisitiza viongozi wote wa Asasi zilizo katika Mradi huu zizingatie fursa hii Adimu" Alisisitiza Bw. Nassoro. Mafunzo haya yanaendelea katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Masasi Mjini mkoa wa MTWARA, TANZANIA.
Mkutano wa wanachama wa MTWANGONET walio katika mradi wa Ushawishi na Utetezi maswala ya VVU/UKIMWI na JINSIA
Tusome Taarifa ya Utekelezaji ya Mtandao ya mwaka 2010RIPOTI_YA_UTEKELEZAJI_YA_MWAKA_2010_NA_MPANGOKAZI_WA_2011.doc
MTWANGONET imeanza kufanya Ufuatiliaji na Tathimini katika miradi yake kwa Azaki wanachama wa Mtwangonet, tunakaribisha maoni na mapendekezo ili kuboresha shughuli hii, Azaki wanachama mnaombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa wetu wa ufuatiliaji na Tathimini.
Mtwangonet inatoa mafunzo ya Afya ya Mama na Mtoto kwa ufadhili wa Amref Mtwara katika ukumbi wa COTC MTWARA, mafunzo ni ya siku tano kuanzia Tarehe 17-21 May 2011