June Mwaka 2016,Mpalano CDO kwa ruzuku kutoka Women Fund Tanzania (WFT) ilitekeleza mradi wa Kuwajengea uwezo Wanawake na Wasichana ili kukuza haki zao za kiuchumi na kisiasa Wilaya ya Mbozi, Songwe, Tanzania. Mradi huu uliwawezesha viongozi wanawake wa kuchaguliwa na wa vikundi vya kijamii wakiwemo wasanii kukuza sauti zao katika katika vyombo vya maamuzi. Vyombo hivyo ni pamoja na mahali wanapofanyia shughuli zao za kiuchumi na katika ngazi ya vijiji, mitaa na kata ili kuwa na ufanisi katika kuwasilisha na kuwakilisha sauti za wasichana na wanawake katika kudai haki kwenye ngazi husika za maamuzi katika wilaya ya Mbozi, mkoa mpya wa Songwe. Pichani ni sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo. Washiriki wanatoka katika kata 9 za Wilaya ya Mbozi: Ichenjezia, Nyambili, Iyula, Isanza, Ipunga, Ihanda, Mlowo, Ruanda na Isandula.
22 Aprili, 2017