Parts of this page are in Swahili. Edit translations
UTAMBULISHO
MASAYODENni shikalisilo la kiserikali na lipo wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara.Shirika lilianzishwa rasmi tarehe 18/5/2002 liliundwa na vikundi 34 vya vijana toka kila kata za wilaya ya Masasi. Masayoden ilisajiliwa tarehe 13/6/2003. namba ya usajili ni S .O.NO 11980 .Shirika linafanya shughuli za vijana ngazi ya wilaya. Lengo kuu ni kupambana na umasikini na vvu/ukimwi wilaya ya masasi.
MASAYODEN ni mwanachama wa shirika Mwamvuli la NGOs Masasi (MANGONET). Masayoden inamahusiano mazuri na vijana, watoto jamii wa jinsia zote. Vilevile serikali Halmashauri ya wilaya ya Masasi na mashirika mengine ya ndani na nje ya wilaya ya masasi. Masayoden imewahi kufanya kazi na UNICEF, 2002-2006 UNDP 2005 CONCERN 2006-2007.
MUHTASARI
Masasi ni Wilaya yenye eneo la mraba KM.4429.9 Wilaya hii ni karibu asilimia 23% ya eneo la Mkoa wa Mtwara ina tarafa 5 kata 34 vijiji 156 na vitongoji 905. Kutokana na sensa ya 2002 ina wakazi 304211. ikiwa na KE 159142 na ME148069. Inakadiriwa kuwa na kiwango cha 2.1% ya ukuaji wa uzazi.
TATIZO
Kuongezeka kwa kikwazo vinavyo kwamisha upatikanaji wa mitaji ya kuanzisha na kuendesha Biashara hasa zile ndogo na za vijijini wilaya ya Masasi.
UHAKIKA WA TATIZO
Wilaya ya Masasi ni kati ya Wilaya zenye idadi kubwa sana ya vijana wasiokuwa na shughuli maalumu na vijana wanayoishi katika mazingira magumu. Kuongezeka kwa tatizo la vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa mitaji ya kuanzisha na kuendesha Biashara .Imeleta athari kwa vijana kama zifuatazo:
(i) kupungua kwa ustawi wa vijana
(ii) Kuongezeka kwa vijana wanayoishi mitaani na vijiweni
(iii) Kuongezeka kwa uvutaji bangi na unywaji wa pombe
(iv) Kuongezeka kwa maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa vijana
(v) Kuongezeka kwa watoto yatima na wanayoishi katika mazingira magumu
(vi) Kuongezeka kwa utegemezi katika familia
LENGO KUU:
Kutokana na malengo ya kitaifa 2025 na mpango wa kitaifa wa mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini Tanzania (MKUKUTA) wenye vipengere vitatu (3) . Shirika la Masayoden likishirikisha na chama cha kuweka na kukopa Masasi vijana SACCOS kuchangia katika kipengele cha kwanza (i) cha kukuza uchumi na kuondoa umasikini wa kipato kwa watanzania.
LENGO LA MAHUSUSI
Kupunguza vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa mitaji ya kuanzisha na kuendesha Biashara hasa zile ndogo na za vijijini kwa vijana wilaya ya Masasi ifikapo Dec 2015.
WALENGWA
VIJANA
MIKAKATI
Kutoa mafunzo ya ujasiliamali
Kuendesha majukwaa ya vijana
Kuboresha ofisi ya Masayoden/Masasi Vijana Saccos
MATOKEO
Kuongezeka kwa uelewa juu ya mbinu, ubunifu uboreshaji wa bidhaa na ufuatiliaji wa masoko
Kuongezeka kwa kipato kwa vijana
Kupungua kwa vijana wanaoishi mitaani na vijiweni
SHUGHULI
Kuendesha mafunzo ya elimu ya ujasilamali kwa vijana
Kuendesha majukwaa ya vijana kila kata
Kuboresha ofisi ya Masayoden na Masasi Vijana Saccos
MAFANIKIO
Kuongezeka kwa ajira katika sekta binafsi
Kuongezeka kwa mapato katika serikali za mitaa kwa kukusanya kodi kutokana ongezeko la uzalishaji mali.
Kuongezeka kwa ustawi wa vijana
Vijana wengi kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo
MUDA WA UTEKELEZAJI
JULLAY…..........SEPTEMBER 2011
ENEO LA UTEKELEZAJI
WILAYANI NA KWENYE KATA
NJIA ZIKAZOTUMIKA
Majadiliano
Kazi za vikundi
WALENGWA WENGINE
Serikali
Jamii
CBOS
MAHITAJI
Vijana
Wataalamu
Fedha
May 26, 2011
Comments (5)
kuimarisha mfumo wa mawasiliano ya vijana kwa kuhusu ukimwi
kuwa mtetezi wa vikndi vya vijana masasi ili vipate kuwakilishwa katika nyanja zote na hoja zote za maendeleo
kuratibu ushirikiano na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi
kulinda na kudumisha utamaduni wa watu wa masasi kwa faida ya vizazi vijavyo
kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za shughuli za utamaduni zinazofanywa na vikundi wanachama.
kubuni miundombinu ya kiuchumi kwa maendeleo ya viajana
kuwa shirika mama au shirika mwamvuli la vikundi vya vijana katika wilaya ya masasi na kurtibu mambo ambayo yanavihusu vikundi hivyo kiwilaya.
Umaskini katika wilaya ya masasi unapigwa vita na unatoweka
KAULI MBIU YA MASAYODEN
Ajira kwa vijana, ambapo vijana katika wilaya ya masasi wanahamasishwa kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali ambavyo vitaanzisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi sambasamba na kuupiga vita ukimwi