Log in
Umoja wa Wawezeshaji Kioo

Umoja wa Wawezeshaji Kioo

Ilagala, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. View in English · Edit translations

Hivi karibuni shirika la KIOO lilifanya ufuatiliaji wa shughuli zake katika kata ambazo mradi wa ufuatiliji wa uwajibikaji kijamii unapofanyika. Katika ufuatiliaji huo ilibainika kuwa pamoja na kwamba serikali imeridhia suala la kupereka madaraka kwa umma kwa kutumia njia ya D by D bado hali ya watendaji huko chini inatia mashaka.Mfano katika kata ya Nguruka kijiji cha Nyangabo na Bweru havina ofisi za watendaji wa vijiji jambo ambalo limeperekea nyaraka mbalimbali za serikali kutunzwa nyumbani kwa mtu yaani nyumba aliyopanga mtendaji wa kijiji husika.

Hali hii imeperekea wanaokaimishwa kazi za utendaji wa kijiji kushindwa kuwa na nyaraka mhimu kwa ajili ya kijiji maana zinatunzwa nyumbani kwa mtu. Hali kama hiyo pia imejitokeza katika kijiji cha Mwamila kata ya Uvinza ambapo nyumba anayoishi mtendaji ndiyo ofisi ya kijiji na cha ajabu sana eneo hilo halina hata choo, hali inayotia shaka juu ya usalama wa watumishi hao wa serikali kiafya.

Kwa mjibu wa sheria ya serikali za mitaa Na 6 mtendaji  wa Kijiji ndiye kiongozi mkuu wa watendaji wengine wa idara za serikali kijijini, mtu huyu ambaye ni kiongozi wa wengine hana ofisi na wala hana cho hivi kweli ni rahisi kwake kuwaongoza wengine kutimiza wajibu wao?

July 30, 2011
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.