Log in
kijogoo group for community development

kijogoo group for community development

morogoro, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Habari wadau,napenda kuchukua fursa hii ya kipekee kwa kutoa taarifa kwa wadau wote wapenda maendeleo nchini kwetu Tanzania.

ikumbukwe kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu,hivyo wadau yatuoasa tuwe mstari wa mbele kwa kuielimisha jamii iliyojiandikisha ijitokeze kupiga kura siku ya uchaguzi ambapo ni tarehe 25 oktoba 2015, na tuhamasishe wananchi kuwa uchaguzi huu uwe wa AMANI na HURU kwani amani ndio njia pekee ya kudumisha amani na utulivu Nchi yetu ya Tanzania.

wenzangu wana harakati tambueni kuwa sisi ni miongoni mwa wadau wakubwa tunoisaidia serikali kufika maeneo ambayo yenyewe serikali haijafika.

Ombi maalumu kwenu ni kuwa kusaidia kuelimisha wananchi wajitokeze kupiga kura kuongeza asilimia ya wananchi watakao shiriki kupiga kura kutoka 48.64% ya Mwaka 2010  hadi 86 au kuzidisha zile asilimia 86 za mwaka 2005.

Ndugu zangu wakati ni huu tusingoje kusukumwa ni wajibu kutekeleza majukumu haya lakini tuzingatie yafuatayo

1. Nchi ibaki kwenye utulivu na kuwepo kwa AMANI ya kudumu

2. Ulinzi na mali za wananchi bila kujali itikadi za vyama

3. Tutoe fursa kwa wananchi wenye ulemavu waweze kufika na na kushiriki kusikiliza sera za

    wagombea na vyama vyao na hatimae kushiriki kupiga kura siku ikifika.

Habari wadau wote wa maendeleo,kwanaza poleni sana na harakati za kila siku za kuleta maendeleo hapa nchini kwetu,

Asasi yetu inatekeleza mradi wa uwajibikaji wa jamii katika kufuatilia rasilimali za umma sekta ya afya wilaya ya ulanga tarafa ya vigoi kata za msogezi na nawenge,tulianza na shuguli ya kuendesha mafunzo kwa viongozi na watendaji wa serikali,wananchi wa kawaida na wajumbe wa kamati za afya kutoka vijiji vya kata husika za mradi na baada ya mafunzo hayo tumeendesha mafunzo ya kina kwa sam timu iliyoteuliwa na washiriki na baada ya nafunzo tupo katika hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi nayo ni kukusanya takwimu kutoka ngazi ya jamii,zahanati,vituo vya afya na kwa mganga mkuu wa wilaya.

Lakini chakusikitisha ni kwamba sehemu zote tumepata ushirikiano wa kutosha ila kikwazo kipo kwa mganga mkuu wa wilaya hataki kutoa taarifa na hana sababu yoyote ya kufanya hivyo, je kuna nini halmashauri ya wilaya ya ulanga kwenye sekta hiyo ya afya ? Tuna muomba mkaguzi wa hesabu za serikali kufanya ukaguzi maalumu kubaini kilichojificha ndani yake.

Kijogoo group for community development inatoa salam za sikuu ya pasaka kwa wadau wote mungu atubariki na tuisheherekee vema kwa amani

 

 

Habari wadau wa maendeleo,napenda kuwasilisha taarifa ya masikitiko juu ya hawa wenzetu waliopewa dhamana na serikali kwa ajili ya kutengeneza chombo kitachotuongoza sisi na vizazi vyeti ( WABUNGE WA KATIBA ) kwa kweli hawaoni ni kiasi gani wa Tanzania wanavyowachukulia kwa mitazamo tofauti kuhusu madai wanayosema ni muhimu kwao ya kudai posho zaidi ya ile iliyopangwa,Je wanatuchukuliaje sisi wa Tanzania wenzao tuliokosa fursa ya kushiriki bunge hilo kwa huo msimamo wao wa kudai posho kubwa angali bado kunachamgamoto kubwa za kimaendeleo zinazotusumbua ikiwa ni pamoja na Huduma duni za Afya,Miundo mbinu ya barabara.

 

Pia watambue kuwa kuna waajiliwa wengi mshara chini ya laki tatu kwa mwezi,wao wanapata laki tau kwa siku lakini hawatosheki  na kutaka ziada ya laki mbili ili iwe laki tano kwa siku je hao watu ni wazazlendo kweli wa nchi hii au wakimbizi ? tunaomba watafakari kwa kina juu ya msimamo wao. naomba tuwe wazalendo na nchi yetu.

Habari wana harakati,Kijogoo Group For Community Development ya Mjini Morogoro,inatoa taarifa kwa wadau juu ya mpango wake wa kutekeleza mradi wa SAM sekta ya Afya Tarafa ya Vigoi Wilaya ya Ulanga pindi tutakapoingiziwa fedha za Mfadhili.

Mradi huo utatekelezwa kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society ya Dar es Salaam nchini Tanzania.

Utekelezaji wa mradi huo utagharimu fedha kiasi cha Tsh,44,500,300/= shilingi milioni arobaini na nne laki tano na mia tatu za ki Tanzania.

Kata zitazohusika na mradi huu ni Kata za Nawenge na Msogezi, lengo ni kuwa na upatikanaji wa huduma bora zenye tija na ufanisi sekta ya Afya kwa wakazi wa kata hizo zilizoguswa na mradi.

ukiwa ni mdau wa maendeleo tunaomba ufuatilie hatua za utekelezaji wa mradi kwa kuzisoma kwa kuwa tutakuwa tukiziweka mara kwa mara kwenye mtandao.

 

Asante

wako katika maendeleo ya jamii

 

Ramadhan Said

Katibu - Kijogoo Group

 

large.jpg

Mh: Diwani wa kata ya Kibedya Tarafa ya Gairo Mze Mkunduge akichangia jambo wakati wa mdahalo ulifanyika Gairo 2011

large.jpg

Mratibu wa Mdahalo/Mradi wa Uwajibikaji wa Serikali kwa Umma wa Kijgooo Group Bw Ramadhani S. Omary akiteta jambo na Mh: Diwani wa kata ya Gairo Mjini wakati wa Mkutano/Mdahalo uliofanyika Gairo 2011

large.jpg

Mgeni rasmi afisa tarafa wa tarafa ya dumila, kwa niaba ya mku wa wilaya ya Kilosa akifunga Mdahalo wa wadau wa matumizi sahihi ya Vocha za Ruzuku za Pembejeo za kilimo. Ulioendeshwa na Kijogoo Group kwa Ufadhili wa The Foundation For Civil Society. L.T.D