Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

Kuna mapungufu gani hasa katika katiba ya sasa yanosababisha wananchi kutaka Katiba mpya?

Sango Kipozi (Dar-es-salaam)
6 Mei, 2011 22:12 EAT

Tunaomba Mchango wenu wa maoni na mapendekezo yenu Kuhusu nini kiongezwe na nini kipunguzwe ili kupata katiba mpya. Kuchangia na kujadiliana kuhusu mada muhimu kama hii ni wajibu wetu kama wana jamii. Tunatarajia ushiriki wenu. Karibuni sana.

Community Organization for Life and Development "COLD" (Buyange, Kahama, Tanzania)
8 Mei, 2011 19:06 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)
Mapungufu yaliyomo katika katiba ya sasa ni:- 1. Katiba hii ilitungwa katika mfumo wa chama kimoja hivyo ni dhahiri kuwa inakibeba chama hicho. 2. Katiba hii inampa raisi mamlaka makubwa mno, pamoja na vyombo vya kiutendaji; hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuhoji hasa katika mfumo wa vyama vingi. 3. Uteuzi wa watendaji wa taasisi za kiutendaji kama taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa (TAKUKURU) na tume ya maadili ya viongozi uko chini ya raisi hivyo kushindwa kutoa mwanya wa kuhoji. 4. Raisi akistaafu, inampa kinga ya kutoshtakiwa hata kama alitenda ndivyo sivyo.
Sango Kipozi (Dar-es-salaam)
10 Mei, 2011 14:28 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

Ahsante sana kwa mchango wako. Je unaonaje ikiwa kwamba Raisi bado abaki na kauli ya mwisho lakini taasisi nyingine kama Bunge zibaki kutoa ushauri na mapendekezo? kwasababu katika mfumo wa tawala mbali mbali duniani , kauli za mwisho huwanazo wafalme malkia waziri mkuu ama Raisi kutengemea na mifumo ya katiba za nchi zao.

Katika tawala zote hizo lazima kuwe na mtu mwenye kauli ya mwisho. Unalionaje hilo Bwana Julius na wengine wote watakao taka kuchangia mada hii inayo tugusa wote.

 

Sango Kipozi Mwenyekiti Mtendaji JEAN media (Dar-es-salaam)
10 Mei, 2011 15:31 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

@ COLD TZ

Kutokana na kmbukumbu ni kwamba Tanzania tumerithi katiba kutoka serikali ya kikoloni iotunngwa kwa mtazamo wa vyama vingi kala ya uhuru, lakini mara baada ya uhuru yakafanyika marekebisho mara mbili kwa msingi wa chama kimoja.Kwahiyo ni kweli lazima katiba ya sasa ishirikishe vyama vingi. Kuhusu madaraka makubwa aliokuwa nayo rahisi kwa mtazmo wa katiba hii ya sasa rejea kwenye majibu au maoni tuliyo ya toa kwa bwana julius, wa PELO, alafu utupatie mtazamo na maoni yako. ahsante kwa kuchangia mada hii.

Kisumva Mathew wa Community Organization for Life and Development "COLD" (Buyange, Kahama)
19 Mei, 2011 22:29 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)
Katiba ya sasa ishirikishe vyama vingi vya siasa, itakuwa rahisi kupata ushiriki wa watanzania. Kama Rais atabaki na kauli ya mwisho bado tu kutakuwa na mianya itakayokuwa uchochoro wa kupitisha maamuzi yasiyo sahihi ama kulingana na maslahi binafsi. Hivyo nashauri taasisi za kiutendaji zote ziwekwe chini ya bunge na uteuzi wao ufanyike bungeni, Rais awe ndiye mwenye kutoa ushauri au mapendekezo.
THOBA JOHN (DAR ES SALAAM)
8 Juni, 2011 12:10 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:06 EAT)

MAPUNGUFU NI MENGI, MOJA KUNA KIFUNGU CHA 46 , KINA TOA KATAZO L A RAIS KUTO SHITAKIWA NA MTU YEYOTE, BALI NI BUNGE TU, HIVI, FIKIRIA BUNGE HILO NDILO LILILOJAA WABUNGU WA CCM, JE WATAKUWA TAYARI KUMBULUZA MTU WAO, PIA KUNA HATUA NYINGI MPAKA KUFIKIA KUMSHITAKI RAIS, NDIO MAANA RAIS ANATAPANYE MALI ZA UMMA KWANI ANAJUA KATIBA ITAMLINDA, NA NDIO MAANA VIONGOZI WENGI WANAKUWA WABADHILIFU ZAIDI, WAKIWAACHA WANANCHI WAO WAKIWA MASIKINI WA KUTUPWA.

MWL.JOSEPH M. ABRAHAM (SHAKE HANDS YOUTH ORGANIZATION(TABATA))
19 Septemba, 2011 09:51 EAT (ilihaririwa 26 Machi, 2012 08:07 EAT)

MAPUNGUFU  YAPO NA  YENYE  KUWEZA  HATA  KUSABABISHA  MIGOGORO  MIKUBWA  KATIKA  NCHI  YETU AU  KUSABABISHA VITA  YA  WENYEWE  KWA  WENYEWE  HUSUSANI  KATIKA  MFUMO  WA  UTAWALA  KWA  MAPANA  YAKE,MFANO  MUINGILIANO WA  KIKATIBA  KTK  UTEKELEZAJI   WA  MAJUKUMU  KATI  YA  MKUU  WA  WILAYA, MEYA/MWENYEKITI WA  HALMASHAURI  NA  MKURUGENZI  WA  WILAYA. HAYA  MAENEO YANATAKIWA  KUTIZAMWA  UPYA  KWA  UMAKINI KATIKA  KATIBA  MPYA  IJAYO  ILI  KUONDOA  MIGOGORO  ISIYO  YA  LAZIMA KTK  NCHI  YETU,WATU  WAPEWE  ELIMU  YA  KUTOSHA  ILI  WAFANYE  MAAMUZI  SAHIHI  KTK  MFUMO  HUU  TATANISHI  KIUTAWALA.

Kwaang, Peter .L. (UDOM)
27 Mei, 2012 11:11 EAT
Katiba yetu, Zanzibar igawanye ktk mikoa. (muungano), Spika asitokee chama chochote. Katiba iweze kuzibiti muda wa wawekezaji kumiliki ardhi. Jaji mkuu asiteuliwe na rais, iwe sehemu ya ajira na watu kusomea nafasi hiyo. Katiba ijayo ikatae suala wastaafu kurudishwa makazini mf. Serikali ya JK.mawaziri-wakuu wa mikoa-wakuu wa wilaya.. Eti mstaafu Eng..... katiba ya Zanzibar isiingilie katiba na mamlaka ya serikali kuu, au serikali ya mseto. Nalia na madaraka ya rais yamezidi sana.
Dickson lukungu (Fray luis sec school. kigamboni)
23 Julai, 2014 09:13 EAT

katiba ya sasa inamnyima haki ya kujieleza bila mipaka kama katiba inavyosema katika kipengele cha muswada wa haki za binadamu kinavyosema, kwani baadhi ya taasisi za serikali zinafanya kazi chini ya ofisi ya rais hivyo watu hushindwa kuuliza kitu chochote juu ya utendaji wa taasisi hizo.mfano takukuru. hivyo suala hili litazamwe upyaaaa,


Ongeza Ujumbe Mpya (Ficha)

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.