MAZINGIRA HATARISHI KWA WAKAZI WA BONDE LA MTO MZINGA.
Baada ya mafuriko kulikumba jiji la Dar es salaam hapo tarehe 20/12/2011 na kuacha hasara kubwa kwa wakazi wa jiji hili,serikali ilichukua hatua za dharura kuhakikisha kuwa huduma za chakula,malazi na mavazi zinaendelea zinaendelea kupatikana kwa waathirika wa mafuriko hayo.
Ukubwa wa tatizo hili umesababisha baadhi ya familia kuwa na hali ngumu ya kimaisha kutokana na ukweli kwamba nyingi za familia zilipoteza mali zote .Serikali kwa kujali ustawi wa wananchi wake imetenga eneo la kuwahifadhi wahanga wa mafuriko hayo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam maarufu kama Mabwebande.
Maeneo yaliyoathirika sana kwa mafuriko hayo ni kimara,ubungo,mburahati,hananasifu,bonde la msimbazi na jangwani kwa kutaja machache.Bonde la mto mzinga liko mbagala misheni kando ya barabara ya kilwa.Mto huu ni moja kati ya maeneo yaliyoathirika vibaya kutokana na mafuriko hayo,lakini kwa bahati mbaya hakuna taarifa zozote zinazoonesha kuwepo kwa hatua za dharura za kuwasaidia wakazi wa eneo hilo.
Hali ya maisha ya wakazi wa eneo hili yako hatarini kwa kuwa nyumba nyingi ziko karibu na mto huu.Licha ya ukaaribu wa mto huu,vile vile,kiwanda cha nguo cha KTM [karibu textile mill]ni tatizo jingine linaloongeza hatari kwa maisha ya wakazi katika eneo hilo.Kiwanda hicho kinatiririsha maji machafu kupitia makazi ya watu,hali ambayo ni hatari kwa afya zao.
Mifumo ya maji na miundo mbinu yake hili hakuna hali ambayo inapelekea wakazi wake kutumia maji ya mto huo kwa shughuli za kijamii kama vile kufulia,kuogea na kulishia mifugo.Eneo la mto mzinga linachukua mitaa ya ngadu,kizinga,bughudadi,mashine ya maji namba tano na misheni,lakini maeneo yote hayajatambuliwa kama maeneo yaliyoathiriwa kwa mafuriko .Baadhi ya nyumba ziko karibu kabisa na mkondo wa maji wa mto huo,hivyo kuongeza uwezekano wa kutokea kwa madhara zaidi pindi mvua za masika zitakapoanza hapo mwezi machi
Tatizo lingine linaloweza kuwakumba wakazi wa eneo hili ni kupata magonjwa ya ngozi kutokana ukweli kwamba maji yanayotoka kiwandani yana kemikali zinazoweza kumdhuru mwanadamu kirahisi.Kemikali hizo ni zile zinazotupwa kutoka kiwandani bila mpangilio maalumu.Wakazi wanaoishi upande wa mashariki mwa mto huo,wapo ndani kabisa ya mkondo wa bahari ya hindi.
Kiujumla eneo hili halifai kuishi kutokana na kuwa katika mfumo wa mkondo wa maji yanayo enda kasi na ardhi yenye kichanga,ambayo ni rahisi kumegeka na kuleta madhara makubwa kwa binadamu na mali zake.Jeanmedia huwa tunaamini kuwa kinga ni bora kuliko tiba,na kutokana na ukweli huo,tungependa kuwaomba wote wenye mamlaka na bonde hili wachukue hatua za haraka za kuwaondoa wakazi wote katika mto huu ama kwa kuwapatia viwanja vya kujenga au kuwapatia fedha ambazo zitawasaidia kutafuta makazi mapya.
Pamoja na eneo hili kuwa hatari kwa maisha ya binadamu,vile vile limesheheni miti aina ya mikoko ambayo inahitaji matunzo ya pekee ili kuifanya izidi kuwepo kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji ya bahari ya hindi na viumbe vingine vilivyomo ndani yake.Lakini tukumbushane kuwa mdharau mwiba mguu huota tende,leo tumeona na tumejua hatari iliopo mbele yetu,hebu tuchukue hatua ili baadae tusimputupie MUNGU lawama .
Chini utaweza kuona picha mbalimbali za mto,nyumba na mshine ambayo hutumika kuchujia maji na kuyapeleka kiwandani na mashine hiyo imekuwa ni chanzo kelele kwa wakazi wa eneo hilo na hutoa moshi mchafu ambao una madhara kwa afya za binadamu.
ANTON KITERERI
UCHUNGUZI ZAIDI WA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MAFURIKO UNAHITAJIKA.
Baada ya mafuriko yaliyotokea tarehe 20/12/2011 kuacha familia zaidi ya 1800 zikiwa hazina makazi,upotevu wa mali na vifo vya watu zaidi ya 41,imebainika kuwa kuna haja ya kufanya uchunguzi akinifu ili kubaini madhara zaidi yaliyopatikana kutokana na ukweli kuwa kuna watu na nyumba zaidi ziliharibika lakini hazikubainika.
Uchunguzi uliofanywa na jeanmedia umebaini kuwa maeneo mengi yaliathirika na mafuriko hayo hayakuweza kubainishwa katika zoezi la kubaini maeneo yaliyoathirika,hali ambayo imepelekea malalamiko kwa viongozi wa ngazi za chini hususani wenyeviti wa mitaa,watendaji na madiwani,kwa kutokufuatilia nyumba zilizo pata madhara kutokana na mafuriko hayo.
Wakazi hao kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wamesema kuwa nyumba zao pamoja na mali zao zilisombwa na maji lakini cha ajabu huduma ikatolewa kwa baadhi ya wananchi.Wameeleza kuwa mpaka sasa hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyejaribu kwenda kuwapa hata pole ya maneno hali ambayo inaonesha kutokujaliwa wanapopata matatizo,isipokuwa wakati wa uchaguzi tu ndio wanaonekana wana wajali.
Wananchi hao wa maeneo ya kimara kilungule,ubungo rombo,gide, kibangu na msewe wamezidi kueleza kuwa karibu maeneo yote yaliyopitiwa na mifereji ya maji yalipata madhara ya kubomokewa kwa nyumba na kupotea kwa vyombo vya ndani.Kutokana na hali hiyo,wameiomba serikali kufanya tathimini upya ili kubaini maeneo ambayo yamepata madhara ili kupunguza usumbufu unaoweza kujitokeza siku za mbeleni.
Ni vema tukaamini kuwa lisemwalo lipo na kama halipo basi laja,hivyo basi kabla madhara zaidi hayajatokea inabidi hatua za makusudi zichukuliwe kuhakikisha kuwa makazi ya watu na mali zao zinakuwa salama.Elimu ya utunzaji wa mazingira inabidi ipewe kipaumbele,hususani katika maeneo ambayo yanakaliwa na wakazi waliokaribu na mifereji ya kupitisha maji ili kuepuka utupaji wa taka ovyo katika mifereji hiyo hali ambayo hupelekea izibe na kuleta harufu mbaya na mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu,kuhara na ugonjwa wa matumbo.Tuendelee kupeana hekima za kiafrika kwa kusema tunza mazingira ili yakutunze.
ANTON MWITA KITERERI
MAISHA MAPYA MABWEPANDE BAADA YA MAFURIKO.
Ni mji mpya kwa sasa,unaopatikana km 37 kutoka jijini Dar es salaam na upo upande wa kusini magharibi mwa jiji hilo,unaotegemewa kukaliwa na familia zipatazo 1800,baada ya makazi yao kuharibiwa kwa mafuriko ya tarehe 20/12/2011.
Jumapili ya tarehe 22/01/2012,msururu wa magari ya jeshi la wananchi wa Tanzania ukiambatana na viongozi wengine wa mkoa wa Dar es salaam,waliwasili katika eneo la Mabwepande tayari kuwakabidhi nyumba wahanga wa mafuriko.Eneo hilo linatarajiwa kuwa na familia zipatazo 1800,lakini mpaka sasa ni familia 300,ndizo zitakazo anza kuishi eneo hilo wakati ukarabati wa nyumba nyingine ukiendelea.
Diwani wa kata ya Mabwepande bwana Clement Boko,anaeleza kwa ufupi changamoto ambazo zinategemewa kuwepo katika kipindi hiki ambacho wakazi hawa wanahamia katika kata yake.Pamoja na kushukru ujenzi uliowezeshwa na shirika la msalaba mwekundu,kwa kuweka mifumo ya maji,bafu na vyoo,lakini anasema bado kuna umuhimu wa kuweka mifumo ya maji taka kwa kuwa haipo kabisa,hali ambao inaweza kuibua tatizo la magonjwa ya kuhara,kipindu pindu na ugonjwa wa matumbo.
Aidha bwana Boko anaeleza kuwa kuna umuhimu wa huduma ya shule ya msingi na sekondari kuandaliwa mapema kwa kuwa watoto ni wengi sana na hakuna shule zilizo karibu na eneo hilo.Pamoja na kuwepo kwa vyoo,bado inaonesha kuwa si vya muda mrefu hivyo kuna kila sababu ya kujenga vyoo vya muda mrefu na miundo mbinu inayopitisha maji taka.Vile vile kituo cha afya ni muhimu kiweke katika eneo hilo kwa ajili ya kuwatibu wagonjwa.
Katika siku ya kuwasili kwao,shirikisho la vyuo vikuu vipatavyo 27 ambalo ni vijana wa Chama Cha
Mapinduzi,kutoka mkoa wa Dar es salaam chini ya mwenyekiti wao bi Aisha Suruu wametoa misaada ya magodoro,maji,juisi,nguo na viatu kwa ajili ya wahanga hao.Kwa kuwa eneo hilo ni jipya na ndio maisha yanaanza upya kuna changamoto mbalimbali ambazo zinatarajiwa kutokea.
Changamoto hizo ni pamoja na maisha kuwa magumu zaidi kwa wahanga,mama Bakri ambaye ni mjane asiye na mme wala mtoto anasimulia, naishukuru serikali kwa kutupatia makazi haya,lakini bado hali ni ngumu kwa upande wetu,hatuna pa kuanzia maana kila kitu kilisombwa na maji,hivyo tunaomba misaada zaidi mpaka pale tutakapo kuwa na uwezo wa kujitegemea,mwisho wa kunukuu.
Katika eneo hilo hakuna huduma yoyote inayopatikana ,kwa maana kwamba maduka,soko na huduma nyingine za kijamii kitu ambacho kinaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi hao.Misaada mbalimbali ya kibinadamu inahitajika kwa haraka sana ili kuwasaidia wahanga hao.Chakula,nguo,dawa ya kutibu maji,dawa za chooni,misaada kwa ajili ya watoto wa shule kwa maana kwamba,sare,viatu,nguo,madaftari na peni za kuandikia ni muhimu sana.Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik anawaomba wadau wazidi kuwasaidia wahanga mpaka watakapokuwa tayari kujitegemea,huku bwana Aidan David wa msalaba mwenyekundu akitoa wito wa aina hiyo hiyo kwa wadau wote kusaidia jamii hiyo.
Kwa upande wa malazi,magodoro,shuka,na hata vitanda ni vitu vya muhimu sana kwa ajili ya wahanga hao.Serikali ya mkoa,wadau na mashirika yana wajibu wa kuhakikisha kuwa mazingira katika eneo hilo yanalindwa ili liendelee kuwa eneo salama la kuishi kwa kila mwanajamii husika.
NINI KIFANYIKE ?
Jeanmedia ni taasisi iliyojikita katika kulinda,kutunza,na kuhifadhi mazingira, inao wataalamu ambao wamebobea katika masuala ya elimu ya mazingira,hii ni timu ambayo ina uzoefu na ujuzi wa kutoa elimu ya mazingira na namna ya kujilinda na maradhi.Kwa mantiki hiyo wadau,mashirika,idara na watu binafsi tunaomba muiunge mkono katika kuhakikisha kuwa adhima ya kutoa elimu hii kwa wahusika inafikiwa kwa kiwango kinachotakikana na kwa muda mwafaka.
Daima tukumbuke ule msemo usemao,kinga ni bora kuliko tiba.
Hapo chini unaweza kuangalia picha mbalimbali za maisha yalivyoanza huko Mabwepande.
ANTON MWITA KITERERI
HALI HALISI YA MAISHA BAADA YA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM
kama umebahatika kutembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko katika jiji hili,hali ni mbaya sana kwa wakazi wa maeneo hayo.Nyumba nyingi ziko kwenye tope zito huku tope hilo likiwa limechanganyika na kinyesi cha binadamu.
hali ya maisha kwa ujumla imekuwa ngumu sana kiasi kwamba wengine wamekata tamaa ya kuishi.Wapo wazazi ambao wana watoto wa shule,lakini tangu shule zinafunguliwa hawajaenda shule kutokana na kutokuwa na sare za shule na vifaa vingine vya shule.
hili ni tatizo jingine ambalo linaweza kuwakumba wakazi wa maeneo haya ya bondeni.Ugonjwa wa kipindu pindu uko karibu sana kulipuka kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.Chakula,maji,kulala,na hata kucheza kwa watoto ni katika mazingira machafu sana ambayo hayamfai mwanadamu aliye hai kuishi.
nyumba za wakazi hawa wa bondeni,ukijaribu kuzitazama kwa umakini utadhani ni mabanda ya kuku au mbuzi,hakika inahuzunisha sana.Jamii yote ya kitanzania inalojukumu la kuwasaidia waathirika hawa ili kuhakikisha kuwa maisha yao yanazidi kusonga mbele kama ilivyo kuwa hapo mwanzo.
katika maeneo haya misaada ya haraka inayohitajika ni kama vile nguo hususani kwa watoto wa shule,dawa kwa ajili ya kuulia mazalia ya mbu,vyandarua,dawa za kutibu maji,vifaa vya kufanyia usafi kama vile jembe,vyekeo,dastibini,na mifagio mikubwa.
mitaro ya kupitisha maji machafu katika nyumba za wakazi hawa imeziba,hali ambayo inaongeza uwezekana wa kuleta maradhi zaidi katika maeneo hayo.Pamoja na tatizo lillilojitokeza,kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya mazingira kwa wakazi hao ili kuwakinga na maradhi yanayoweza kuwakabili muda wowote.
zoezi la kuwasaidia waathirika wa mafuriko kuweza kuhama kutoka katika maeneo hayo linaonekana kwenda pole pole sana,hali ambayo inachangiwa na uwezo mdogo wa serikali kuwahudumia waathirika wote kwa pamoja.Kutokana na hali hiyo wito kwa mashirika ya kiraia,taasisi za dini na watu binafsi,washiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wanatoa misaada kwa wahanga hawa wa mafuriko.
Kuendelea kufumbia macho watu wanao endelea kukaa bondeni ni kuwachimbia kaburi wakati wakiwa hai,hii ni kutokana na ukweli kuwa hata kabla ya mafuriko hali za wakazi hao ni mbaya sana kuanzia makazi na mazingira wanayoishi.Wito kwa wadau na watanzania wote wakazi wa bondeni ni ndugu zetu,tuwasaidie ili waweze kuondokana na hali waliyonayo kwa sasa.Waafrika tumezoea kusema 'kutoa ni moyo',usambe si utajiri.Saidia ili ibarikiwe.
PICHA MBALI MBALI ZA ATHARI ZA MAFURIKO JIJINI DAR-ES-SALAAM
Maji machafu karibu ya makazi ya watu na nyumba zizilojengwa kwenye maeneo hatarishi,
endapo mvua kubwa zitatokea tena
Hali ikiendelea kubazi namna hii kuna hatari kubwa ya Magonjwa ya milipuko. Kazi kubwa inatakiwa kufanywa kuhamasisha jamii ili tuweze mazingira yawe safi na salama kwa binaadam.
Dar es Salaam Flooding Community Survey
Before flooding: saa 1 | Now: saa 2 na zaidi,hii ni kutokana na kuvunjika kwa madaraja |
ELIMU YA STASDI ZA MAISHA.
Mimba za utotoni na utumiaji wa dawa za kulevya nchini Tanzania limekuwa ni tatizo linalokuwa siku hadi siku.Takwimu zinaonesha kuwa watoto wenye umri kuanzia miaka 9-25,ndio wanaoathirika kwa kiwango kikubwa na tatizo hili.
Mwaka 2008 katika shule ya msingi Ilagala mkoani Kigoma binti wa miaka tisa alionekana kuwa na ujauzito ,hali ambayo ilihatarisha maisha yake na kiumbe kilichokuwa tumboni.Mwaka 2006 wanafunzi 64 wa kike walioanza shule ya sekondari katika shule ya sekondari Ilagala,ni wanafunzi 4 tu waliobahatika kuhitimu kidato cha nne.Hapo unaweza kuona namna tatizo hili lilivyo kubwa.
Asasi za kiraia na wadau wengine wa afya wanalojukumu la kutoa elimu kwa vijana wa shule za msingi,sekondari na wale walioko mitaani kwa lengo la kuwajengea stadi za kujitambua,kujiamini,kujithamini,na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika makuzi yao.
Katika makuzi ya vijana,wamejikuta wakikabiliwa na shinikizo rika,hali ambayo imewaingiza baadhi yao katika matatizo.Miongoni mwa matatizo ambayo yanawakabili vijana kutokana na shinikizo rika ni pamoja na mimba za utotoni,utumiaji wa dawa za kulevya,ushoga,uchokoraa,na utumikishwaji katika biashara ya ngono.
Somo la stadi za maisha limeonesha uwezo mkubwa wa kuwasaidia vijana wengi kukabiliana na changamoto zinazowakabili.Vijana wengi ambao walishaanza kutumia dawa za kulenvya na kujiingiza katika vitendo vya ngono katika umri mdogo,walijiondoa baada ya kupatiwa elimu ya stadi za maisha.
Kwa wale ambao walikuwa hawajanza vitendo hivyo,baada ya kupatiwa elimu hiyo wamekuwa ni waelimishaji wazuri kwa wenzao,hali ambayo imesaidia kukuza uelewa wao kuhusiana na afya ya miili yao.Stadi za maisha ni mbinu au njia anazo tumia mtu katika kukabiliana na mazingira yanayomzunguka hatimaye abaki salama kimwili,kiroho na kiakili.
Kwa kawaida stadi za maisha husaidia vijana kujiamini,kujithamini,kujiheshimu,kujitambua na kuwajenga uwezo wa kupambanua jambo baya na zuri na kufanya maamuzi sahihi pindi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali.
Katika stadi za maisha tunawafundisha vijana kutatua matatizo kwa kutumia T3.Hii ina maana kuwa
T1-----------tatizo
T2-----------tatuzi
T3----------tokeo
Katika kupata tokeo la tatizo,kuna uwezekano tokeo likawa chanya au hasi.Kwa kutumia T3 kijana anaweza kutatua matatizo kimantiki zaidi,tofauti na ambaye hana elimu ya stadi hiyo,ambapo wengi wakabiliwapo na matatizo magumu hufikia hatua ya kujiua kwa kuamini kuwa matatizo kama hayo hayana utatuzi,hususani baada ya kufukuzwa nyumbani au kukataliwa na wenzi wao.
Mada zifuatazo huwasaidia vijana kujitambua vizuri sana katika makuzi yao.
- Ø Madhara ya dawa za kulevya
- Ø Madhara ya mimba za utotoni
- Ø Uthubuti wa kusema hapana yenye kumaanisha
- Ø Kuepuka makundi rika
- Ø Namna ya kuchagua rafiki mwema
- Ø Njia za kuepuka maeneo hatarishi.
- Ø Mbinu za kuepuka ushawishi wa zawadi,lifti na pesa
- Ø Namna ya kujitunza wakati wa balehe na kuvunja ungo
Vijana hupata habari nyingi ambazo nyingine ni potofu kwao.Kutokana na hilo ni vema wakapewa habari sahihi zinazohusu miili ya na makuzi yao.Mfano vijana wengi wa kike na wa kiume wanapata taarifa kuwa wasipofanya ngono mapema watapata matatizo wakiwa wakubwa,habari ambazo kwa hakika si sahihi na zinapotosha.
Vilevile vijana hupenda kujaribu baadhi ya mambo ili kuona matokeo ama wanayo yasikia au kuona nini kitatokeo ya kufanya jambo fulani.Kutokana na hali hiyo wazazi,walezi,asasi za kiraia,azaki,na wadau wengine wanalojukumu la kutoa elimu kwao ili kuwaepusha na majaribio ambayo mwisho wake ni matatizo kwao.
Jeanmedia imeliona hili na itashiriki kikamilifu kuhakikisha kuwa inawaandaa vijana bora kwa ajili ya kuwa viongozi mahiri wa kesho.Kwa kutambua ukubwa na ugumu wa tatizo hili,jeanmedia inawaomba wadau wote kuunga mkono juhudi hizi kwa kuiwezesha kwa hali na mali ili iweze kuwafikia vijana wengi wa mjini na vijijini.
Nguvu kazi ya taifa lolote duniani ni vijana,hivyo wasipoandaliwa vizuri leo,kesho watakuwa bomu ambalo litakapolipuka litaangamiza taifa lote.Waafrika wanayo methali isemayo “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”,hivyo kama tunahitaji kuwa na kizazi bora chenye maadili,uzalendo na uwajibikaji tuanze kuwaandaa vijana sasa kisaikolojia,kimaadili,kifikra na kimtazamo.
ANTON MWITA KITERERI
ilikuwa ni tarehe 20/12/201, usiku na kuamkia tarehe 21/12/2011 wananchi wa jiji la Dar es salaam walijikuta katika wakati mgumu mara baada ya kukumbwa na mafuriko,ambayo yaliwaacha baadhi ya wakazi wa jiji hili wakiwa hawana makazi ya kuishi huku wengine wapatao 41 wakipoteza maisha.
Kutokana na hali hiyo,serikali,taasisi,mashirika na watu binafsi walijitoa kwa hali na mali kuhakikisha kuwa wahanga wa mafuriko wanasaidiwa,kwa kupatiwa malazi,mavazi na chakula.Maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na mafuriko hayo ni pamoja na kimara,mbezi,tabata,msewe na jangwani.
Nyumba,miundo mbinu ya barabara na madaraja,viliharibiwa kabisa hali iliyopelekea kukatika kwa mawasiliano kati ya eneo moja na lingine. Kutokana na kuharibiwa kwa miundo mbinu hiyo,baadhi ya maeneo ya kazi yalikosa ufanisi,kutokana na ama wafanya kazi kuchelewa kufika kazini au kutofika kabisa.
Athari ya mafuriko itaendelea kuwa kubwa iwapo hatua za makusudi hazitachuliwa hasa kwa wananchi wanaoishi sehemu za bondeni kwa kuwa idara ya hali ya hewa nchini imeelezea kuendelea kuwepo kwa mvua kubwa kati ya mwezi Februari na Machi.Baada ya mvua kusimama kwa muda baadhi ya changamoto mbalimbali zimeonekana kujitokeza.Moja ya changamoto hizo ni pamoja na uwezekano wa kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara,kipindu pindu na magonjwa ya tumbo.
Hali hii inatokana na uchafu uliokithiri katika maeneo hayo ya bondeni.Baadhi ya maeneo yameonekana kuwa na vinyesi ambavyo vilitapishwa wakati mvua ilipokuwa inanyesha.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine,wana jukumu la kuhakikisha kuwa elimu ya mazingira inatolewa ili kuepuka madhara ambayo yatatoke baadae,iwapo hatua za makusudi hazitachuliwa kudhitibiti hali hiyo.Daima kinga ni bora kuliko tiba,ni vema utaratibu wa kudhitibi matatizo uzingatiwe kabla ya kutokea kwa tatizo,hali ambayo itasaidia kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.
Pamoja na serikali kuwataka wananchi wanaoishi sehemu za bondeni kuhama na kutafuta maeneo yaliyosalama kwa maisha na mali zao,bado uchunguzi unaonesha kuwa itakuwa ni vigumu kwa baadhi yao kuhama kutokana na ukweli kwamba,wananchi wengi hali zao za kimaisha ni duni sana.Mfano mkazi mmoja wa jangwani B amenukuliwa akisema kuwa yuko tayari kufia bondeni na hawezi kuhama kwa kuwa hana uwezo wa kufanya hivyo.
wananchi hao ambao wengi wao huendesha maisha yao kwa kuokota makopo na kuyauza,inaonesha itakuwa ni vigumu kuwaondoa maeneo hayo kwa kuwa hawana njia nyingine mbadala ya kuwafanya wajikimu kimaisha.
Katika kipindi hiki cha mpito,serikali,mashirika na watu binafsi wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma za afya unazingatiwa,kwa kutoa dawa za kutibu maji,vyandarua,sabuni pamoja na vyombo vya kupikia pale itakapobidi.
Daima umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,hivyo wadau kwa pamoja tuungane ili kuhakikisha kuwa tatizo lililojitokeza linakabiliwa.
ANTON MWITA KITERERI.
ATHARI ZA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM
Kutokana na mafuriko yaliyolikumba jiji la Dar es salaam,tarehe 20/12/2011 wananchi wengi mpaka sasa hawana makazi ya kudumu na huduma za afya zimezidi kuzorota kwa kiwango kikubwa.
Takwimu zinaonesha kuwa watu wapatao 41 wamefariki dunia kutokana na mafuriko hayo,wakati wengine mamia wamepoteza makazi na mali zao.Baada ya tukio hilo kutokea serikali na wadau wengine walishirikiana kuhakikisha kuwa misaada ya hali na mali inapatikana kwa ajili ya wahanga wa tukio hilo.
Hali ya maisha kwa wahanga imekuwa ngumu zaidi kutokana na kukabiliwa na mafuriko hayo,hususani kwa wale waliokuwa wanaishi maeneo ya bondeni.Pamoja na sababu za kisayansi zilizoainisha kuchangia kutokea kwa mafuriko hayo,bado kuna kila sababu ya kuamini kuwa uchafu uliokithiri katika maeneo mengi ya jiji na miundo mbinu mibovu imechangia kuongeza ukubwa wa tatizo.
Utupaji wa taka ovyo katika mifumo ya kupitishia maji,ulipelekea mikondo ya maji kubadili uelekeo wake kutokana na kukosa uelekeo ulio sahihi.Mkazi mmoja wa kimara kilungule aliyejulikana kama baba Jesca,alieleza kuwa uchafu uliokithiri katika mitaro ya maji ndio sababu iliyochangi kwa kiasi kikubwa maji kubadili uelekeo wake na kuingia katika nyumba,baada ya kukosa uelekeo wa moja kwa moja.
Wakati mwingine kutokana na mitaro kuziba ilibidi maji yakose uelekeo na hivyo kuharibu maeneo menginie,hasa ikichukuliwa kuwa sehemu nyingi za jiji la Dar es salaam zina udongo wa kichanga,hali ambayo ni rahisi kwa maji kujipenyeza mahala popote hasa pale yanapokutana na ukinzani.
Maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam yamejaa taka taka,hali ambayo ni hatari kwa afya za wakazi wa maeneo husika na mkoa kwa ujumla.Ukibahatika kupita maeneo ya jangwani,kimara baruti,ubungo kibangu,ubungo msewe,bonde la msimbazi na maeneo mengine ya tabata,mburahati,mbezi na hata katikati ya jiji kwa kutaja baadhi hali ya mazingira ni mbaya sana.Hali hiyo inapelekea kuwepo kwa mlipuko wa magonjwa ya mara kwa mara,kama vile kipindu pindu ,kuhara na ugonjwa matumbo.
Hali ni mbaya zaidi kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko,kutokana na maeneo hayo kuendelea kuwa na uchafu uliochanganyikana na kinyesi cha binadamu.Iwapo hatua za haraka hazitachuliwa,madhara yake yatakuwa makubwa sana,hali ambayo itaiingiza serikali katika gharama nyingine.
Nyumba nyingi bado zimejaa tope zenye vinyesi hali ambayo ni hatari kwa afya za binadamu,hususani watoto wadogo ambao hawajui madhara yoyote wanapokuwa wanacheza katika tope hizo.Miundo mbinu ya maji nayo imechafuliwa sana na mafuriko hayo,hivyo hali hiyo inaleta wasiwas zaidi ya watu kunywa maji yenye maji yenye uchafu na yasiyo salama kwa afya zao.
Jitihada za makusudi inabidi zichukuliwe kuhakikisha kuwa mazingira na maeneo yaliyoathiriwa yanakuwa safi na salama kwa watu kuishi.Elimu ya mazingira ni muhim,hasa katika kuondoa tope kwenye nyumba,kufukia madimbwi ya maji machafu,kuchimba mashimo ya taka,kusafisha mitaa yote ili kuiweka katika hali ya usafi na salama zaidi.
Suala la kuyaweka mazingira katika hali ya usafi ni la wadau wote.Jeanmedia ikitambua umuhimu wa afya kwa binadamu imelenga kutoa elimu ya mazingira kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam,kwa lengo la kulifanya jiji hili kuvutia kimadhari.
Kwa kuwa jeanmedia imeonesha njia kwenye suala hili,ni vema ikaungwa mkono na wadau wengine ili kufikia lengo la kuyahifadhi mazingira yetu.Wakazi walioathirika kwa mafuriko wanahitaji kupewa elimu ya mazingira kwa kuyaweka katika hali ya usafi,kuchemsha maji ya kunywa,dawa za kutibu maji na dawa na kuulia wadudu.
Wapo wakazi walio hamishiwa eneo la mabwepande,kama sehemu ya makazi yao mapya,kuna kila sababu ya wakazi hawa kupewa elimu ya kuhifadhi mazingira kutokana na huduma nyingi za kijamii kutopatikana.Huduma za maji,vyoo,dawa na vifaa vya kufanyia usafi nai moja kati ya vitu muhimu vinavyohitajika kwa wahanga hawa katika kipindi hiki wanachoanza maisha upya.
Jeanmedia inaamini kuwa ustawi bora wa maisha ya mwanadamu hutegemea ubora wa mazingira anayoishi,na kinga ni bora kuliko tiba,hivyo elimu inayotegemewa kutolewa na jeanmedia ni kinga kwa maradhi ya mlipuko.
Kusubiri tatizo litokee ndio tuanze kutumia gharama katika kuliondoa au kulidhibiti,tunazalisha matatizo zaidi,maana tatizo linapotokea tayari linakuwa limeisha acha madhara ya kifo au uharibifu wa mali na makazi ya watu.
Kutoa elimu ya mazingira itasaidia kupunguza gharama zisizokuwa na sababu kwa mwananchi.Mfano badala ya kusubiri mwananchi augue kipindu pindu ndio apatiwe matibabu ni vema akapewa elimu ya kujikinga na maradhi hayo,ili gharama ambazo zingetumika kwenye matibabu zitumike kwenye huduma nyingine za kimaendeleo.
Ikumbukwe kuwa hata mabadiliko ya tabia nchi yamechangiwa kwa kiwango kikubwa na shughuli za kibinadamu na harakati zake kuyatawala mazingira.Kutokana na ukweli huo,elimu pekee ndio njia mbadala ya kuhifadhi mazingira na kuyafanya kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Taarifa zilizokuwa zinatolewa na idara ya hali ya hewa kama zingezingatiwa na kutiliwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kupunguza ukubwa wa tatizo au kulidhibiti kabisa.Mali pamoja na maisha ya watu yangeokolewa iwapo serikali na wadau wengine wangechukua jukumu la kuwaondoa la kuwaondoa wakazi wa bondeni kama ilivyofanyika hivi sasa.
Vile vile jeanmedia inaamini kuwa huu ni wakati mwafaka wa kutoa elimu ya mazingira ili kupunguza baadhi ya matatizo yasiyo ya lazima kutokea.Suala la mazingira ni la mtambuko,linahitaji uhamasishaji kwa kila mdau kutambua umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi,kuepuka kutupa taka katika vyanzo vya maji,kuepuka kuchoma misitu,ujenzi holela usiofuata taratibu bora za ujenzi kama ilivyo miji mingi nchini,kuepuka kuchoma takataka zenye kimekali katika maeneo yenye makazi ya watu.
Ikiwa wewe ni mtu binafsi,shirika,taasisi,kikundi cha watu iunge mkono jeanmedia katika kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo lake la kutoa elimu hii kwa jamii.Waafrika tunao msemo methali isemayo,ngoja ngoja yaumiza tumbo,hivyo linalowezekana leo lisingoje kesho.
ANTON MWITA KITERERI
Skill sharing- Basic Interviewing Skills
Hallo there!
I would like to share with you some basic Interviewing Skills:
- Know what your story is-in other words why you are doing the interview?
- Know what role this person is playing in your programme.
- Brief yourself-find out as much background on the story as possible.
- Decide on your angle. What line are you going to take?
- Keep your questions brief and simple.
- Decide when you are going to use open/closed questions.
- Try not to write down the questions-use key words to jog your memory.
- Tell your interviewee what you are going to talk about. But do not spell out each question to him/her.
- Don’t let them tell you their best stories in the chat. They’ll never repeat them in the same way and they will use “as I said earlier”.
- Remember to give them the context of the interview. Which programme and why.
- Remember body language is most important for you and for the interviewee.
- Don’t let interviewees pull rank. This is your interview and you are finding answers for your audience.
- Keep eye contact.
- On the phone SMILE and soften the voice.
15. Enjoy it.