Shirika letu kwa sasa tumeweza kuwasaidia watoto 45 wanaoishi katika mazingira hatarishi wa vijiji vya Lusanga, Kwadoli na Dihinda kupunguza makali ya maisha kwa kuwapatia chakula,nguo na vifaa vya kusomea.
Pia upande wa VVU/UKIMWI shirika limeweza kuendesha zoezi la kupima kwa hiari katika kijiji cha Lusanga ili kubaini maambukizi mapya hapo mwaka 2009 na 2010 na kubaini waathirika 18 ambao wanapata huduma ya dawa za kurefusha maisha sasa.
ELIMU:Shirika limeendelea kutoa elimu ya tekinolojia kwa vijana na watu wazima chini ya mradi wake wa ongeza maarifa ya tekinohama(omayate), mpaka sasa vijana 17 na watu wazima 10 wamepata elimu ya tekinohama,mradi huu ulianza mwezi wa July 2010 na ni mradi endelevu.
Shirika linakusudia kuendesha mradi wa kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika Tarafa 2 za Turiani na Mvomero hapo ifikapo June 2011 kama tutapata ufadhili mapema.
Comments (1)