HATIMAE ASASI ZA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI, ZAKUBALIANA MPANGO WA KUFANYA KAZI KAMA TIMU ILI KUFANISI HUDUMA ZITOLEWAZO KWA JAMII NA KUFIKIA MALENGO.
Hakuna Matata Charity Organization kanda ya Magharibi ofisi kuu KIGOMA, yazindua programu ya maalumu itakayo ziwezesha Asasi mbalimbali Mkoani Kigoma kufanya kazi kama timu ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mfumo mmoja wa uratibu wa shughuli zinazo tekelezwa na CSO katika Manispaa ya kigoma. Katika kufanikisha hilo Asasi ya Hakuna Matata kanda ya magharibi Kigoma kwa kushirikiana na Mtandao wa KIGOMA UJIJI NGO NETWORK (KIUNGONET) Kwa pamoja wamefanikisha kufanyika kwa mkutano ulio zileta pamoja Asasi zaidi ya kumi, zinazo shughulika na Watu wenye ulemavu,Wazee,Vijana,Watoto waishio katika mazingira hatarishi,Mazingira pamoja na zile zinazohudumia watu wenye matatizo ya ngozi(Albino) Kikao hicho kilifanyikia katika Ofisi ya Hakuna Matata Charity-Kigoma. Siku ya Jumamosi saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, tarehe 18/05/2013.
Wajumbe waliohudhuria kikao hicho waliwakilisha Asasi za, Mwenyeji wa Mkutano HAKUNA MATATA CHARITY ORGANIZATION-KIGOMA, CHAWATA-KIGOMA,LATAPEDO,WDS,CAYODE,TAS-KIGOMA,KALLE-CBO,SHIVAWATA-KIGOMA,KDSG,SHIMAUTITA,YECAPA,KIUNGONET,NA YAAPA.
MADA ZILIZO JADILIWA:
MADA YA KWANZA:
Uwasilishaji wa kazi za Asasi washiriki ikiwa ni pamoja na uainishaji wa shughuli za kila Asasi,maeneo inayo fanyia kazi, Dira,Dhamira na Madhumuni ya kila Asasi ilioshiriki Mkutano huo.
Kila Asasi iliwasilisha kazi zake mbele ya wadau, ambapo baada ya uwasilishaji wa kazi za Asasi kufanyika.
Ulifuata wakati wa uchambuzi wa kimantiki baina ya Dira,Dhamira na Madhumuni ya kila Asasi. katika kipengele hiki mwezeshaji wa Mkutano ndugu Adam Kiyunzuguru ambae ni (Country Executive Director wa Hakuna Matata)
Alifafanua kwa kina, juu ya umuhimu wa kila Asasi kurejea upya katika kuhakikisha kuwa Dira,Dhamira na Madhumuni ya Asasi vinakuwa na Uhusiano wa Kimantiki, kwa kuongoze alisema.
"Mtiririko mzuri baina ya Dira,Dhamira na Madhumuni ya Asasi ndiyo muhimili mkuu wa kuitambulisha Asasi katika jamii,wadau na Wahisani" kwa kuongeza alisema, kama Asasi haitakuwa na Mpangilio mzuri, inakuwa vigumu Asasi kujitabua uwepo wake, na wajibu wake.
Ufafanuzi huo ulitengeneza wingi wa maswali miongoni wa washiriki "wengi wao walikiri kuwepo na udhaifu wa kimantiki baina ya Dira,Dhamira na Madhumuni yaliyoko katika Asasi zao hali inayo pelekea wengi wao kushindwa kufikia vigezo vya kupata ufadhiri kutaka vyanzo mbalimbali zaidi ya THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY Ambae ndie mfadhili mkuu wa Asasi zilizoshiriki Mkutano huu"
MAAZIMIO: "Asasi washiriki wa mkutano walikubaliana kurejea na kufanya mapitio ya Dira,Dhamira na Madhumuni ya Asasi ili kuona kama kuna ulinganifu wa kimantiki".
MADA YA PILI:
Mtoa mada. Ndugu Adam Kiyunzuguru ambae ni (Country Executive Director wa Hakuna Matata)
Mada ya pili ilihusu uchambuzi wa mfumo wa kiutawala wa kidemokrasia unao pendekezwa kutumikia katika Asasi.
kama Asasi inayo zingatia kanuni za utawala bora ni vema kupitia mfumo wa kiutawa wake kuona kama ina mihimili ifuatayo ndani ya Asasi yake.
1. MKUTANO MKUU
Mkutano Mkuu wa wanachama wote, kuwa chombo chenye sauti ya mwisho ya maamuzi katika mambo yote yanayo husu mustakabali wa Asasi.
2. BODI YA WAKURUGENZI.
kam Asasi inayo jitambua ni vema kuwa na Bodi ya wakurugenzi iliyo thabiti na inayo jitambua, bodi ya wakurugenzi inaundwa na baadhi wa wanachama walio chaguliwa kupitia mkutano mkuu wa wanachama wote, kwa lengo la kuwa wasimamiziwakuu wa shughuli zinazo tekelezwa na Sekretariati ya Asasi, na hawa ndio wanaobeba dhamana usimamizi kwa niaba ya Wanachama wa Asasi, ikumbukwa kuwa Bodi ya inawajibika kwa Mkutano Mkuu wa wanachama wote.
3.SEKRETARIETI.
Inapendekwezwa kuwa Mkuu wa Sekretarieti ya Asasi ni Mkurugenzi Mtendaji, ambae yaweza kuwa ameteuliwa au ameajiriwa na bodi ya Wakurugenzi. Na huyu ndiye atakuwa mwajiri wa wafanyakazi wote wa Asasi, kwa kukuzingatia mahitaji ya Asasi na uwezo wa kifedha lakini yote shariti yafanyike kwa njia shirikishi baina ya mtendaji Mkuu wa Asasi na Bodi.
katika hali hii, Mtendaji Mkuu wa Asasi anawajibika kwa bodi na bodi inayo mamlaka ya kumuonya,kumsimamisha au kumuachisha kazi endapo kama itabainika kuwa anaendesha Asasi kinyume na taratibu za zilizo kusudiwa.
baada ya mada kuwasilishwa kilifuata kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa washiriki wa Mkutano, kama inavyo onekena katika picha.
Baada ya kipindi ch maswali na majibu kukamilika washiriki wote walikubaliana kurudi katika taasisi zao kwa ajili ya majadiliano ya kina wanachama wa asasi wanazotoka, ili kupitia upya mufumo wa kiutawala na kiutendaji ndani ya Asasi.
MJUMUISHO WA MKUTANO.
Mwezashaji wa Mkutano, Ndugu Adam Kiyunzuguru ambae ni (Country Executive Director wa Hakuna Matata). Alichukua fursa hii kuwa elezea washiriki wa mkutano juu ya Dira,Dhamira na Madhumuni ya Asasi ya Hakuna Matata Charity Organization.
Alinukuu Dira,Dhamira na Madhumuni ya Asasi yaliyo andikwa kwa lugha ya Kingereza kama inavyo someka hapa chini:-
DIRA YA ASASI.
Society free from Stigma and discrimination on marginalize groups and gender identity rights.
DHAMIRA YA ASASI.
Hakuna Matata Charity Organization is an NGO aiming at improving the capacities of Marginalize groups, community,CSOs,CBO,FBO,SCHOOLs and local governments’ leaders to deliver friendly services through training, networking, policy analysis, lobbying and advocacy.
MADHUMUNI YA ASASI.
1. To promote community awareness on issues of marginalize groups and gender identity rights.
2. To start exploring District level responses, priorities, opportunities and risk on marginalize groups and gender identity on their basic rights.
3. To develop, programme, objectives, outputs, outcomes and agree on strategies to reach the expected changes on marginalize groups and gender identity on their basic rights.
4. To comprehensive knowledge among marginalize groups and SOGI, on HIV/AIDS-TB and Malaria Transmission, Treatment, prevention and Care support.
13.5. To Educate Community, religious leaders and politician on Health reproduction adhere to people with disability and MSM.
Baada ya uwasilishaji huo kuihusu Asasi ya Hakuna Matata Charity Organization.
Ndugu Adam,aliwaelezea washiriki Wanaasasi katika mkutano huo, kuwa Asasi ya HMCO katika kutambuba kuwa ili iweze kufikia malengo yake ya kiutendaji inategemea sana ushirikiano baina yake na Asasi nyingine zinazo toa huduma za kijamii kwa makundi tofauti. katika kuhitimisha Asasi zote washiriki walikubaliana kwa pamoja kuunganisha nguvu zao ili kuwa na mfumo mmoja wa utambuzi na utoaji huduma kwa jamii kwanjia ya kuwaunganisha walengwa katika makundi ya kimtandao. Ambapo ilishauriwa kuwa Asasi zile zinazofanya kazi zinazo fanana ni vizuri zikawa na utaratibu unaofanana na maeneo yanayo eleweka ili kuhakikisha kuwa panakuwepo mfumo ulio wazi wa kuitendaji na ubadirishanaji taarifa juu ya mafanikio na changamoto na kuwekea mikakati ya kukabiliana na mazingira yanayo jitokeza.
MAAZIMIO YA JUMLA YA KIKAO:
Mwisho wa Mkutano, Asasi ya Hakuna Matata Charity Organization ilitambulisha programu yake ya " utekelezaji kupitia wahusika" katika programu hiyo Hakuna matata itaendesha program na miradi ya kuwajengea uwezo watu wa makundi maalumu yaani watu wenye ulemavu wa aina zote,Wazee,Watoto na Wamama wajane. programu hiyo itakelezwa kupitia makundi na Asasi zao, lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kuwaunganisha katika vikundi vya mtandao na Asasi na kuwajengea uelewa juu ya haki zao na jinsi ya kuzidai na kutumia umoja wao kama spika ya kufikisha sauti yao kwa umma. programu hiyo itawafanya watu wa makundi maalumu kushiriki michakato ya kuzidai haki zao katika maswala Kisiasa,Sera,Utawala,Elimu,Ajira na Afya.
kupitia programu hiyo Asasi washiriki walikubaliana kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kama timu sambamba na kuwashirikisha walegwa katika kila hatua tangu uibuaji wa miradi na utekelezaji wake ili kutekeleza hasa kile ambacho walengwa wanakihitaji kiuharisia.