Tovuti ya asasi yako inaweza kuandikwa kwa lugha yoyote unayotaka. Hata hivyo, watu wengi zaidi wataweza kusoma tovuti yako kama imetafsiriwa kwa lugha yao.
Kupitia Envaya, ni rahisi kutafsiri ukurasa wowote wa tovuti yako kwa lugha nyingine.
Baada ya kuchapisha ukurasa ambao umeandikwa kwa lugha moja, chagua lugha nyingine ya Envaya kwa kutumia menyu ya Lugha juu ya ukurasa. Halafu, bonyeza Hariri tafsiri au Edit translations, kama hapo chini:
Ikiwa kuna zaidi ya tafsiri moja katika ukurasa huo, Envaya itaorodhesha maandiko yoyote ambayo yataweza kutafsiriwa katika ukurasa huo, pamoja na tafsiri ya sasa. Bonyeza tafsiri ambayo unataka kuihariri.
Halafu, unaweza kuhariri tafsiri kwa lugha nyingine. Bonyeza kitufe cha Toa tafsiri au Submit translation wakati ambapo umemaliza ili kuchapisha tafsiri kwenye tovuti yako.
Watu wengine wanaotembelea tovuti yako wanaweza pia kusaidia kutafsiri tovuti yako kwa lugha mbalimbali. Hata hivyo, tafsiri yoyote iliyowasilishwa na watu wengine inahitaji kukubaliwa nawe au na msimamizi kabla ya kuchapishwa na kuonekana katika tovuti yako.