Njia rahisi ya kuongeza hati kama za Microsoft Word kwenye tovuti yako ya Envaya ni kwa njia ya kunakili na kuhamisha. Hata hivyo, njia hii haifanyi kazi wakati wote, kwa sababu picha na mpangilio wa hati yako inaweza kupotea wakati wa kuhamishia kwenye tovuti yako ya Envaya.
Njia mbadala ya kuchapisha nyaraka zako juu ya Envaya ni kwa kutumia batani hii . Hii inakuwezesha kuchapisha nyaraka kutoka Microsoft Word, pamoja na PowerPoint, Excel, na PDF.
Kuongeza hati juu ya ukurasa au habari mpya unayoihariri, ponyeza kwenye kiboksi kama hapa chini:
Kwenye boksi itakayojifungua ponyeza peleleza kuchagua hati kutoka katika kompyuta yako:
Tafuta hati au picha au faili ya picha, na kisha bonyeza Fungua. Hati yako itahamishiwa kwenye sehemu husika ya Envaya. Inaweza kuchukua dakika chache kulingana na kasi ya mtandao wako.
Kitufi cha hati yako kitaonekana kwenye ukurasa unaohariri. Unaweza kuendelea kuhariri ukurasa wako. Unapomaliza, bonyeza batani ya bluu chini ya ukurasa kuchapisha hati kwenye tovuti yako.
Hati itakapochapishwa kwenye tovuti yako itaonekana kama hivi:
Mtu yeyote atakayetembelea tovuti yako atakuwa na uwezo wakuona hati yako kwa urahisi bila kuhitaji kufungua programu ngingine.