Kufungua Akaunti yako ya Envaya
Ukijiandikisha Envaya unaingia moja kwa moja kwenye akaunti yako mpya. Lakini wakati mwingine unaweza kurudi envaya.org, huenda ukawa umefungiwa nje na unahitaji kuingia tena kuhariri tovuti yako.
Ili kuhariri tovuti yako, nenda http://envaya.org katika web browser yako na bonyeza Ingia, kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
Kisha andika jina la mtumiaji la shirika lako na neno la siri yaani password, ambazo ulizichaguwa wakati wa kusajili asasi yako, na bonyeza batani ya bluu kuingia ndani
Kama umekosea kwenye kuandika jina la mtumiaji au neno la siri, ujumbe mwekundu utajitokeza. Jaribu kuandika jina na neno la siri lako tena, na kuhakikisha kuwa unaliingiza neno la siri kwa kutumia herufi zilezile ulizotumia ulipofungua akunti yako, kama ni herufi kubwa au ndogo, kisha bonyeza batani ya bluu tena.
Kubadilisha Neno la Siri
Kama huwezi kuingia kwenye akaunti yako ya Envaya, unaweza kubadilisha neno la siri ya akaunti yako.
Kama asasi yako limesajili anwani ya barua pepe na Envaya,fuata hatua zifautazo:
- Bonyeza "Umesahau neno la siri?"
- Ingiza jina la mtumiaji la shirika yako au anwani ya barua pepe, na bonyeza batani ya bluu
- Ingia kwenye akaunti ya barua pepe la shirika lako na subiri ujumbe kutoka Envaya
- Bonyeza link itakautumwa na Envaya
- Kuchagua password mpya ya shirika lako, na bonyeza batani ya bluu kuingia ndani
Kama asasi yako haina anwani ya barua pepe, au kama huwezi kubadilisha neno la siri kutumia hatua ya juu, nenda http://envaya.org/envaya/contact na tutumie mawasiliano yako ili tuweze kuthibitisha kama wanapaswa kuingia kwenye akaunti hiyo.