Envaya

Envaya

Kuongeza Mashirika ya Ubia kwenye Mtandao wako

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri
Msaada : Kuhariri Tovuti Yako

Kuongeza Mashirika ya Ubia kwenye Mtandao wako

Katika tovuti yako ya Envaya, unaweza kuunda ukurasa wa mawasiliano, ambapo unaweza kuorodesha mashirika ambayo unashirikiana nayo na kueleza jinsi unavyofanya nayo kazi.

Mashirika haya ni pamoja na mashirika yanayokudhamini, au yanayofanya kazi na wewe, pamoja na mitandao ambapo asasi yako ni wanachama. Unaweza kuongeza mashirika ya Mtandao katika ukurasa wako hata kama hayajasajiliwa kwenye Envaya.

Kuunda ukurasa wa majadilianao, ingia kwenye Envaya nenda kwenye hariri ukurasa ( ). Nenda chini katika sehemu hariri ukurasa, na bonyeza majadiliano.

Kuongeza shirika la ubia, bonyeza Ongeza Shirika. Kisha, ingiza jina la shirika, na mawasiliano ya shirikia hilo, kisha bonyeza kitufe ya Ongeza Shirika.

Envaya itatafuta mashirika ambayo yameshajiunga kwenye Envaya kwa kutumia jina na mawasiliano la shirkia hilo. Ikiwa shirika hilo ni mtumiaji wa Envaya, bonyeza Ongeza ili kuwaongeza kwenye ukurasa wa Mtandao wako.

Kama shirikia halipo kwenye Envaya, bado unaweza kuwaongeza. Kama wana anwani ya barua pepe, unaweza kuwaalika kujiunga Envaya.

Baada ya kuongeza shirika la ubia, bonyeza Ongeza maelezo kuongeza habari zaidi kuhusu uhusiano wa asasi yako na hilo shirika.

bonyeza Ona Ukurasa kuona jinsi ukurasa wa mtandao unavyoonekana kwenye tovuti ya asasi yako. Juu ya ukurasa utaona orodha ya mashirika ya ubia, na viunganishi vya tovuti zao. Chini ni muhtasari wa taarifa za mabadiliko au habari mpya kutoka kwa mashirika yako ya ubia walio kwenye Envaya.