Envaya

Dhahabu Arts Group ni taasisi ya kijamii isiyolenga kupata faida binafsi yenye lengo la kuona siku moja jamii ya kitanzania inakuwa bora katika sekta za Afya, Elimu, Uchumi na Utamaduni.

Ili kutimiza malengo haya, Dhahabu hufanya kazi na wabia mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Kwa sasa inafanya kazi zaidi na The Foundation for Civil Society.

Mapema mwaka huu Dhahabu itakuwa inatekeleza Mradi wa mpango wa Kuwajengea uwezo Jamii na Wadau Sekta ya Elimu kuhusu Maboresho ya Sekta ya Elimu na wajibu wao katika usimamizi wa Rasilimali za Umma za Sekta ya elimu ngazi ya Kata kupitia mradi wa Social Accountability Monitoring (SAM) katika Kata zote 34 za Manispaa ya Kinondoni. Mradi huu ambao umefadhiliwa na Taasisi ya The Foundation for civili Society ni wa miaka mitatu na unaanza mwaka huu wa 2011 na utamalizika Septemba 2013.

 

Ni kwa muktadha huu, na kwa kuzingatia ukweli kwamba ni vigumu kufikia mafanikio ya mradi ambayo ni kuongeza Ufanisi katika Sekta ya Elimu pasipo ushirikiano toka kwako, kwa maana hii kama una kitu unaweza kuchangia katika kufanikisha mradi huu usisite kuwasiliana nasi.

Kwa kipindi cha January – Machi mwaka huu tutakuwa na mafunzo ya siku nne ya watu 162 kutoka katika kata zote Manispaa ya Kionondoni. Mafunzo yanatarajiwa kuanza tarehe 10/1/2011 katika ukumbi tutakaoutangaza baadae.

 

 (Baadhi ya wasanii wa Dhahabu wakiiwezesha jamii kufanya ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za umma kwa kutumia Sanaa Shirikishi hadhira katika viwanja vya TGNP Mabibo Mei 2010

 

5 Januari, 2011
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.