Kushiriki katika kampeni ya kuiwezesha jamii iweze kuchukua hatua ili kupunguza/kuzuia vifo vya akina mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Singida na Mara.
Kutengeneza filamu inayoelezea mbinu mbadala za kupambana na ukimwi na kuulinda utamaduni iitwayo Mwanahiti
Kutengeneza filamu inayohimiza uadilifu katika maisha ya ndoa iitwayo Msamaha.
Kutengeneza matangazo ya redio (jungle) kuhusu Ukatili wa kijinsia majumbani, udhulimati wa mirathi na upatikanaji wa misaada ya kisheria kwa kushirikiana na WIL-DAF.
Kuwawezesha vijana wa makambi (camps) wa wilaya za Kinondoni ili waachane na matumizi ya madawa ya kulevya na waweze kujiajiri kulingana na fursa walizonazo (kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society)
2008
kusimamia unzishwaji wa Mtandao wa vijana walio katika makambi (Camps) wa Dar es salaam Camps Network (DACANE) kwa ajili ya kuwawezesha vijana kujiajiri kulingana na fursa walizonazo.
kutengeneza filamu inayoelezea umuhimu wa kuandika wosia iitwayo Siku isiyo na jina.
Kuandaa utaratibu wa kuendesha mijadala ya kijamii ya kila mwezi ili kujadili mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika kata na wilaya yetu.
2009
kutekeleza Mradi (pets) wa kuboresha Elimu Manispaa ya Kinondoni.
Kukamilisha Studio ya taasisi na kuandaa vipindi televisheni vya kijamii vyenye lengo la kuendelea kuifanya jamii kuwa bora katika kila sekta ili kutimiza lengo letu.
2010
Kutoa elimu ya Mpiga kura katika Kata sita za Manispaa ya Kinondoni.
2011 -2013
Kuijengea uwezo jamii kuweza kusimamia rasilimali za umma za Sekta ya Elimu (Social Accountability Monitoring - SAM) katika Kata 34 za Manispaa ya Kinondoni.