Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
Asasi ya kijamii "COLD" limeadhimisha siku ya mwanamke kwa kutoa mafunzo ya namna ya kutengeneza jiko la maajabu kwa wanawake wa kikundi cha Mwamko wa kata ya Igoma, jijini Mwanza. Jiko hili hutumia kuni au mkaa kidogo sana Lengo la mafunzo hayo ni kupunguza mzigo kwa wanawake waliokuwa wakilazimika kutumia muda mwingi kutafuta kuni milimani. Mafunzo hayo yameendeshwa na raisi ambaye pia ni afisa mtendaji mkuu wa asasi hii bwana Kisumva Mathew Maziku. Wakati hayo yakiendelea Mwanza, huko Dar, makamu wa raisi wa shirika hili bi Esther Mbedule aliliwakilisha katika maadhimisho hayo kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Donate us
Community Organization for Life and Development "COLD" is asking wellwishers to make their donation to one or for all from the following programs. 1. Sponsor a child. Children sponsorship is an amazement way to bring hope and to a child living in difficult circumstances. 669 children identified and we sponsor 66 (orphans, vulnerable, rural poor and disadvantaged) children to school. Your financial contribution can enable us to buy exercise book and text, school uniforms, shoes and school bag. By paying the school fees for one of the children, you help the child to get quality education. In return, you will be kept up-to-date about the progress of your sponsor child. The sponsorship is automatically terminated after one year unless you indicate that you that you wish to continue. 2. HIV/AIDS awareness program in rural communities. 3. Run the job skills training related to the needs of the community. 4. Provide lunch at school for 669 vulnerabled children in primary school of Bugarama ward, Kahama, Tanzania. MAKE YOUR DONATIONS TO THE FOLLOWING BANK ACCOUNT. Account holder: Community Organization for Life and Development "COLD" Bank name: NMB Kahama branch. Account number: 3062300949. Donate by POST: Alternatively, if you wish to make a one-off donation by cheque, you can use the followin address below:- COLD BOX 150 KAHAMA.
Kupitia mradi wake wa 'TEGEMEZA' inaendesha kampeni juu ya kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI, katika programu hii COLD imedhamiria kueneza ufahamu wa jinsi ya kujikinga ili kupunguza maambukizi mapya nchini Tanzania. Mpango huu unalenga kuondoa imani potofu kuhusu VVU/UKIMWI na kuhakikisha kuwa jamii ina habari sahihi zitakazowasaidia kufanya maamuzi sahihi. Mpango huu umekusudia:- 1. Kuhamasisha jamii kufikiri kuhusu mapenzi na kuwaruhusu kutathmini madhara yatokanayo na aina yoyote ya mapenzi. 2. Kuwafundisha watu jinsi ya kupunguza madhara ya maambukizi kwa kuwahamasisha kuacha ngono, kuchelewa kujiingiza katika vitendo vya ngono, kutumia kondomu na kupunguza idadi ya wenzi wao. 3. Kuwapa watu ujasiri na silaha ili waweze kujadiliana na wenzi wao kuhusu suala la mapenzi. 4. Kuwasaidia watu kuelewa madhara ya kuwa muathirika na kuhamasisha kutunza afya zao kwa kadri iwezekanavyo ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa. 5. Kuwapa ufahamu walezi namna ya kuwahudumia waathirika wa VVU/UKIMWI walio majumbani.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
Community Organization for Life and Development "COLD" imeshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo yameadhimishwa kimkoa katika kata ya Bugarama wilaya ya Kahama, ambapo mgeni rasmi amekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Brigedia Jenerali mstaafu, Dk. Yohana Balele. COLD imetoa msaada wa sare za shule na madaftari hamsini na tano kwa watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu kumi na mmoja, wavulana watano na wasichana sita wanaosoma katika shule ya msingi Bugarama ambazo wamekabidhiwa na mgeni rasmi. Mgeni rasmi amelipongeza sana shirika hili kwa juhudi zake na kuahidi kuwa yuko tayari kulisaidia kistadi na kiushauri. Pia mgeni rasmi amekabidhi hundi ya shilingi mia tano elfu kwa mkurugenzi mtendaji wa COLD Bw. Kisumva Mathew Maziku ukiwa ni msaada wa kuunga mkono jitihada za shirika kutoka halmashauri ya wilaya ya Kahama.
Community Organization for Life and Development "COLD" imealikwa kushiriki katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, yatakayofanyika kimkoa katika kata ya Bugarama, kwenye eneo la utekelezaji wa shughuli zake. Siku hiyo asasi hii imekusudia kutoa sare za shule, madaftari na kalamu kwa watoto 11 walio katika mazingira magumu wanaosoma katika shule ya msingi Bugarama. Kwa kufanya hivyo COLD itakuwa inatimiza kauli mbiu ya mwaka isemayo "TUUNGANE PAMOJA KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA KUSAIDIA WATOTO WA MITAANI"
Tawi jipya
Community Organization for Life and Development "COLD" imefungua tawi jipya katika kijiji cha Bugalagala, wilaya ya Bukombe. Tawi hilo litafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu zinazoiongoza COLD na si vinginevyo. Watendaji wa tawi hili watawajibika kwa uongozi wa asasi katika makao makuu ya asasi.Mgeni rasmi,afisa maendeleo ya jamii kata ya Bugarama, wanachama wa COLD na wageni waalikwa wakielekea kuzindua ofisi ya shirika hili.
Wazazi/walezi wakiwa na watoto wao baada ya kupewa msaada wa sare za shule na asasi ya COLD.