TANGAZO.
CHAMA CHA MICHEZO CHA VIZIWI TANGA-CHAMIVITA.
CHAMIVITA-TANGA kinaomba ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuinua ari ya michezo kwa walemavu viziwi katika jiji la Tanga
CHAMA CHA MICHEZO CHA VIZIWI TANGA (CHAMIVITA) TANGA ASSOCIATION OF SPORTS FOR THE DEAF (T.A.S.D) S.L.P 5106-TANGATANZANIA,EMAIL: deafssports@yahoo.com |
Kumb no. CMVT/TNG/VOL ,12/12 03/05/2012
KWA WADAU WOTE WA WA MICHEZO
POPOTE TANZANIA.
KK
AFISA UTAMADUNI,
HALMASHURI YA JIJI LA TANGA,
S.L.P 178
TANGA
Ndugu,
YAH: OMBI LA MSAADA WA NAULI KWA AJILI YA KUSHIRIKI TAMASHA LA MICHEZO ZANZIBAR.
Somo la hapo juu lahusika sana.
Chama cha michezo cha viziwi Tanga-(CHAMIVITA) kinaandika barua hii kwako kwa ajili ya kupatiwa msaada wa Nauli kwa ajili ya kutuwezesha kushiriki TAMASHA LA MICHEZO KWA VIZIWI litakalofanyika Zanzibar mwezi july 23 hadi 6 Agost 2012 mwaka huu.
Kwa sasa CHAMIVITA kipo katika kutafuta na kukuza ARI ya michezo kwa walemavu viziwi wa mkoa wa Tanga, kwa mujibu wa waandaaji wa TAMASHA hilo kwa CHAMIVITA TANGA tunatakiwa kujigharamia kwa mahitaji ya nauli ya kwenda na kurudi Tanga,usafiri wa ndani ya Zanzibar.kwa wachezaji 20 na viongozi 3 Aidha chakula na malazi vitatolewa na wandaaji/wenyeji ZFA na CHAMIVIZA(CHAMA CHA MICHEZO CHA VIZIWI ZANZIBAR) Mahitaji yetu ni kama ifuatavyo:-
(i) Usafiri wa Tanga to Dar es salaam watu 23@11,000x2x23= Tsh 506,000.00
(ii) Usafiri wa dar es salaam to Zanzibar watu 23@20,000x2x23 =Tsh 920,000.00
(iii) Usafiri wa ndani ya Zanzibar kwa wiki mbili =Tsh 300,000.00
(iv) Dharura na matibabu =Tsh 200,000;00
JUMLA 1,926.000,00
Kwa mahitaji hayo hapo juu tunaomba muangalie ni jinsi gani mnaweza kutusaidia kadri ya uwezo wako ili tuweze kufanikisha Azma yetu ya kuendeleza michezo kwa walemavu viziwi wa mkoa wa Tanga.
Tunatanguliza shukrani za dhati kwako.
Wasaalam,
________________
ALLY NASSORO
KATIBU MKUU SIMU +225713 733 114 TUMA SMS TU.
________________________________________________________________________
N.B: Endapo msaada wenu utakuwa katika hundi iandikwe: JUMUIYA YA MICHEZO YA VIZIWI TANZANIA A/C NO 41 72 50 87 86 NATIONAL MICROFINANCE BANK(NMB) MADARAKA BRANCH TANGA