- UTUME WA CHAVITA-MISSION
“CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya viziwi ina maisha bora, inayojijengea uwezo wa kujiamini, kujithamini, kujiendeleza, kukuza lugha ya alama ya Tanzania na kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kimaendeleo, kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na serikali na taasisi nyingine.”
- DIRA YA CHAVITA-VISION
CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya watanzania inawatambua, inawakubali, inawathamini, inawashirikisha viziwi na kuhakikisha hawasumbuliwi na umasikini, unyanyasaji, ubaguzi na ukandamizaji wa aina yoyote”
- MALENGO YA CHAVITA
Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha hili kwa:
- Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapa Tanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
- Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
- Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama ya Tanzania.
- Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
- Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
- Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
- Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
- Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.
Latest Updates
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA DODOMA MJINI updated its History page.
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) ni chama kilichoanzishwa na Viziwi wenyewe mwaka 1983 na kusajiliwa rasmi na Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 04/09/1984 na kupewa no so. 6466 na baaada ya kupitishwa kwa sheria ya Uanzishwaji wa vyama vya kiraia ya mwaka 2002, CHAVITA ilipata hati namba NGO 1878 tarehe 21/04/2006. ... Read more
December 7, 2012

CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA DODOMA MJINI updated its Projects page.
Mradi wa Lugha ya Alama uliofadhiliwa na shirika la The Foundation Civil for Society ya Dar es salaam hapa wageni wakuu wa idara za Serikali,Kaimu Afisa Ustawi wa Manispaa na Bibi Hawa Mtui Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wakifungua Mradi wa Mafunzo ya Lugha ya Alama kwa kata 4 za wilaya Ya Dodoma Mjini,Kikombo,Hombolo,Zuzu na... Read more
December 7, 2012

CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA DODOMA MJINI added 2 News updates.
Lugha ya alama nini? – Lugha ya alama tanzania ni chombo cha mawasiliano ambacho humuwezesha mzungumzaji kufikisha ujumbe kwa jamii kwa adhira iliyokusudiwa na jamii husika. – ( L.A.T) – Lugha ya alama ni lugha ambayo imekamilika... Read more
December 7, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA DODOMA MJINI created a Home page.
UTUME WA CHAVITA-MISSION
– “CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya viziwi ina maisha bora, inayojijengea uwezo wa kujiamini, kujithamini, kujiendeleza, kukuza lugha ya alama ya Tanzania na kushiriki kikamilifu katika... Read more
December 7, 2012
Sectors
Location
DODOMA, Dodoma, Tanzania
See nearby organizations
See nearby organizations