Lugha ya alama nini?
Lugha ya alama tanzania ni chombo cha mawasiliano ambacho humuwezesha mzungumzaji kufikisha ujumbe kwa jamii kwa adhira iliyokusudiwa na jamii husika.
( L.A.T)
Lugha ya alama ni lugha ambayo imekamilika kuliko lugha yeyote ambayo inazungumziwa na watu wote ulimwenguni kwa maana lugha ya alama ina mpangilio mzuri wa sarufi inayojitegemea kwa kutolea mfano: kiswahili , Naomba maji ya kunywa tafadhali. Hapa unakuwa bado kuidhinisha ni maji gani unayotaka wewe na kitu gani kitumike kuchotea maji hayo unayotaka wewe. Ila lugha ya alama inabainisha kila kitu tena hatua kwa hatua mpaka zoezi zima linatimia japo inaenda taratibu kuliko lugha ya kiswahili au kiingereza.
2. Rejea alifabeti za alama tanzani kwa mfano herufi ,A, C,D,Z,na Y. Hii ni moja ya mifano hai yenye kutumia umbo kamili la lugha ya alama. Pia kuna vitu kama samaki, gari, simu, na karibu vitu vyote vinatumia umbo au tendo linalojirudiarudia wakati wa kutumia vitu hivyo baadhi ni kama baiskel, pikipiki, cherehani n.k.
3. lugha ya alama imegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni:
A) lugha ya asili tanzania. (A.A.T)
B)lugha ya alama tanzania.(L.A.T) ambayo ndio lugha ya taifa.
4.Kwa utaratibu maalumu wa matumizi ya lugha ya alama lazima baadhi ya viungo vya mwili vitumike ili kuonesha ni kitu gani kina taka kuzungumziwa, baadhi ya viungo hivyo ni mikono, Uso, Kichwa, mdomo, na macho na sio kutumia miguu maana lugha ya alama inaishia usawa wa kitovu kwenda juu nakutoka kichwani ni sm kumi kwenda juu. Pia kila kiungo kitakapohusisha uonesha huwasilishaji wa ujumbe huo uko namna gani kama ni hali ya furaha au huzuni. Mfano uso mara nyingi huonesha kalipio au furaha zaidi.
5. Vikwazo katika mawasiliano ya lugha ya alama kuna vikwazo kama vile msongamano wa watu maeneo ya ofisini, mikutano, kuta za majengo, miti, magari pia mwanga hasa hali ya giza ndio huathiri mawasiliano kwa kiwango kikubwa sana kwani viziwi wanatumia macho na si masikio kwa maana macho yanatumika kuona kila alama na masikio yanatumika kusikia kila aina ya sauti.
6. Kiziwi ni binadamu wa kawaida mwenye utamaduni wa aina mbili ukiwemo wa kutumia lugha ya alama kama chombo chake cha mawasiliano na akitumia lugha ya taifa lake kwani lugha ndio kitambulisho cha utamaduni wa jamii ya eneo fulani. Viziwi hawakubaliani kabisa na neno la kuitwa bubu. Ni Lugha mbaya na tena ni udhalilishaji mkubwa.