Shirika la Christian Education and Development Organization CEDO, limezidua mpango mkakati wa uchechemuzi (Advocacy) wa lishe na ustawi wa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Mpango huu umezinduliwa tarehe 31/01/2015, na Mhe. Naomi Mwakyoma na ulishirikisha asasi za kiraia, Madiwani, Baadhi ya viongozi wa Serikali za mitaa, Wananchi wa kawaida, Sekta binafsi,na wataalamu.
Lengo kuu la mpango huu ni kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, kuboresha maisha, afya na ustawi wa wote, wanawake na makundi yaliyohatarini kwa kuinua uelewa wa jamii ili kuchangia na kuendeleza juhudi za kuokoa maisha ya mama na mtoto.
February 6, 2015
Comments (1)
“Afya njema kwa kila mtu afya njema kwa watu wote”
“Lishe Bora ni msingi wa Maendeleo ya Taifa, timiza wajibu wako”