Log in
ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA)

ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA)

Bunda, Tanzania

KWANINI VIJANA WANAJIHUSISHA NA VITENDO VYA UOVU?

ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA)
June 2, 2014 at 10:01 PM EAT

CHANZO CHA VIJANA KUJIHUSISHA NA VIKUNDI MBALIMBALI VYA UHALIFU KATIKA JAMII

Imekuwa ni kawaida ya vijana kuanzisha vikundi mbalimbali vya uhalifu katika jamii suala ambalo jamii kiujumla haiwezi kulistahimili kwani vijana hawa wamekuwa ni vijana wanyang’anyi na pengine hata kudhuru maisha ya watu.

Hivi juzi tu, tumeshuhudia ama kushuhudiwa katika vyombo vya habari ama kwa kuona kwa macho yetu jiji Dar-es-salaamu vikundi vya vijana mbalimbali vijijihusisha na unyang’anyi kwa kutumia nguvu tena hadharani na sehemu nyingine mbalimbali za nchi hii siyo hali ya kuvumilia katika jamii kwani inahatarisha uhuru na uhai wa taifa kiujumla. Pamoja na jitihada mbalimbali kuchukuliwa na serikali ili kudhibiti tatizo hili katika jamii lakini sisi wana AUVITA kiukweli tunaliona tatizo hili kwa jicho tofauti ambapo serikali na asasi zingine tunaweza kushiliki kwa kutatua changamoto zifuatazo kwa vijana ili kuwaepusha na vitendo visivyo salama katika usitawi wa jamii.

Sababu za vijana kuunda vikundi vya kutenda maovu

Ukosefu wa ajira kwa vijana, kumekuwa na ongezeko kubwa kwa vijana katika jamii ambao hawana ajira suala hili linaendana sambamba na kutokuwa na sifa za kupata ajira hivyo vijana wengi hukosa kazi ya kufanya na kujiandaa rasimi kwa kuishi kwa kutumia nguvu za uporaji kwa kuunda vikundi mabalimbali kama tuonavyo leo.

Ukosefu wa elimu ya ujasiliamali kwa vijana, imekuwa ni kawaida ya vijana kutoka vijijini na kukimbilia mijini kwa kujitafutia kipato lakini wafikapo mijini huyakuta maisha ni magumu kupita kiasi kwa vile vijana hawa huwa hawajajiandaa rasimi kujishugulisha na biashara ndogondogo za kijiingizia kipato basi matokeo yake huwa ni kuvuta madawa ya kulevya na kundaa vijikundi vya uhalifu.

Ukosefu wa mitaji, pamoja na kuwa vijana hawa baadhi yao hupata mafunzo ya ujasiliamali ama kwa wenzao au asasi za kijamii lakini bado changamoto kubwa kwao huwa ni mitaji ya kuwawezesha kuanzisha biashara ndogondogo, kutokopesheka kwenye taasisi mbalimbali za kifedha, na kutijituma kujitafutia wenyewe mitaji.

Nini cha kufanya

Serikali iamzishe mafunzo ya ujasiliamali mashuleni na vyuoni kama somo na liwe la lazima kwa kila mtanzania kusoma.

Vijana wahamasishwe kijihusisha na shughuli za kilimo vijijini badala ya kukimbilia mijini ambako hkoswakazi ya kufanya na kujiingiza katika vikundi vya uhalifu.

Asilimia 10 ya mapato ya halimashauri zote nchni kutengewa vijana na akinamama itiliwe mkazo na serikali kwa kushirikiana na asasi za kijamii waelimishe vijana na kuwawezesha ili wajijengee misingi bora ya maisha.

Taasisi za kifedha ziwekeze kwa vijana kwa kuwaelimisha juu ya mbinu za kibiashara na jinsi wanavyoweza kunufaika na huduma za kifedaha kwa kuwekeza hasa katika kilimo ambacho hakiitaji ujuzi wa elimu ya juu sana, tukiwajengea uwezo vijana na taasisi zikifungua milango ya mikopo kwa vijana watajikwamua kiuchumi.

Asasi za kijamii zinazohusika na vijana zitumie muda mwingi kuongea na vijana na kuwaelimisha juu ya shughuli mbalimbali ambazo zinaweza kurahisisha maisha yao kilahisi.

Mwisho

Jamii yetu ni vijana wetu tuwaelimishe, tuwawezeshe na kuwajengea misingi bora ya maisha kwa maendeleo ya taifa letu.

NOMBA MICHANGO YENU ILI KUTATUA TATIZO HILI.

Neatness Msemo (Dar es salaam)
June 11, 2014 at 3:36 PM EAT (edited June 11, 2014 at 4:07 PM EAT)

Kwanza kabisa namshukuru Mungu pia nawashukuru Envaya kwa kutuunganisha na kwa kujenga Network kubwa hapa nchini hii pia ni hazina tosha.Pia nawashukuru wenye kuleta mada hii (AUVITA)kwani wamemaliza yote ambayo ndani ya moyo wangu ningetamani nihutubie taifa na kuwaeleza ni nini kilio cha watanzania wengi hususan vijana.Mimi kama mmoja wa wenye Asasi hizi za kiraia au mwanachama hai kwenye Asasi ya Africa Upendo Group(AUG)Asasi ambayo kwa sehemu kubwa inashughulika na vijana na kiasi kikubwa kilio chetu kinafanana kwani tunapoteza nguvu kazi ya nchi kwa kukosa tu maarifa.Labda niweke michango yangu kwa namna hii hapa:

  • Haya tunayoyaona yote ni matokeo ya yale ambayo kwa kiasi kukibwa tumeyazembea.
  • Vijana wenyewe kama watajitambua na kujithamini haya yote tunayoyazungumza yatakuwa hayapo kwani kila mtu atajua jukumu na wajibu wake wa kufanya.
  • Pamoja na elimu ni muhimu sasa serikali ikapangilia mitaala yake na tangia mwanzo wa kuanza elimu ya msingi masomo kadhaa (soft skills)yakiwemo ya ujasiriamali yakaanzwa kufundishwa na kusimamiwa kivitendo na wanafunzi wakafanya mitihani ya vitendo kama ilivyo practical exams kwenye masomo ya sayansi.
  • Kama kulivyo na vyuo mbalimbali vya ufundi basi mkazo uwepo pia na kuwe na vyuo maalum na shule za michepuo wa kibiashara,kilimo na ufugaji na kuwepo na mitihani na wanafunzi wafanye mitihani kama inavyofanyika sasa na badala ya wanafunzi kusoma nadharia tena ya masomo ambayo hayana faida kwao wanapomaliza ni vizuri sasa serikali ikajikita zaidi kwenye masomo yenye kuleta tija kwetu yaani taifa kwa ujumla.mtu asome ambayo baadaye atayafanyia kazi kama madaktari.Lakini leo mtu anasomeshwa mavitu mengi na akienda mtaani au kazini hakuna hata uhusiano.Graduate anaajiriwa hajui afanye nini ni hadi aanze kupitishwa tena kwa miaka ndipo apate uzoefu.inachosha.Utashaangaa mtu ambaye hajasoma anachapa kazi kuliko ndio maana hivi sasa ofisi nyingi ambazo sio za serikali haziangalii tu kisomo pia utendaji kazi.
  • Sasa hivi ni kweli vijana wengi hawana kazi lakini pia vijana wengi hawako tayari kujitolea na katika kujitolea ndipo mtu anapopata uzoefu na kama vijana waliomaliza udaktari wanapelekwa internship(mazoezi katika hospital mbalimbali)ifanyike hivyo hata kwa fani nyingine.Watu wasiajiriwe moja kwa moja kwanza wapimwe na kupata uzoefu kazini ili aajiriwe mtu ambaye anastahili na sio anayejulikana.Leo watoto wa wa kubwa ndio wenye kila kitu baba zao wakistaafu wao nao wapo kwenye nafasi zao au mashirika na taasisi nyeti wakati hawajui kitu.wenzetu huko majuu system zao angalau wanajitahidi sana.kwao mwanafunzi anapitia kwenye mafunzo ya kujitolea na anajua wajibu wake na hata akipewa taasisi anatumika ipasavyo na haweki fedha mbele bali anaweka maslahi ya wateja wake au wananchi mbele.Aanajua kabisa kuwa wao ndio waliomwanjiri.
  • Leo tumeajiri wasomi kwenye sekta mbalimbali lakini nikujipitisha tu hakuna kitu kinachofanyika wengi hawajui wala hawana uchungu na nchi wakati wote anawaza atapataje gari la kifahari na nyumba aoe na kuolewa na kutanua basi hajui kuwa hao wananchi ndio wamemweka katika nafasi hiyo.Ndio maana kuna mikataba feki waliopewa dhamana wanalindana tu watu wakisema ukweli wanakasirika na hata watoa maamuzi nao wamekuwa hivyo hivyo hakuna tena mwenye uchungu na nchi hadi unashangaa na kujiuliza je hawa kweli ni watanzania wenzetu?.Kwa misingi hiyo hakuna sera wala taratibu ambazo watu wamejiwekea zinazofuatwa bali wengi hulindana tu.Hii ni shida ndio maana leo wenye kutengeneza mitaala hawana macho ya kuona Alama za nyakati kwamba kinachotakiwa ni nini kwa kizazi cha sasa.Wao wanasema hayo ndio maamuzi ya serikali.Serikali isiyosikia wala kuona je ni kweli ni serikali au ni watendaji wabovu?
  • Hapa nimeongelea zaidi vijana wasomi lakini kwa vile tulishapotea njia ndio maana nimesema tujitathimini kama serikali/wadau/wananchi tuanze upya na kwa hawa ambao ni product mbovu serikali ikisaidiana na wadau mbalimbali kama sisi NGO'S Tuweze kuwa na mipango endelevu ambayo kama tutawaza ni namna gani ya kumkomboa kijana badala ya kulalamika kwani serikali inalalamika NGO nazo zinalalamika na wananchi nao wanalalamika sasa nani amsaidie yupi.Tukae pamoja na kwa pamoja tuje na mikakati  mbalimbali ambayo ni mikakati inayotekelezeka.Mfano kule Mtwara kule Mwanza,Kule Kilimanjaro kule Mbeya n.k hebu tuangalie tunayo ardhi safi ambayo ni kubwa sana na haijalimwa.Hebu vijana tujiunge pamoja na labda kama kuna NGO, halmashauri mbalimbali wawe na mikakati na vijana na makundi pia mengine.Tutumie ardhi tulipewa na Mungu tuna maji mengi sana kila mahali mfano nakumbuka zamani sisi huko kwetu tulikuwa na kitu kinaitwa misaragambo watu wanatoka na kuchimba mifereji kila mtu anapata maji ya kumwagilia shambani mwake na kama tulivyo na maji na ardhi kweli hatuwezi kuwa na kilimo cha kumwagilia?je hatuwezi kuwa na mabwawa ya samaki na mambo mengi kadha wa kadha .Mengine ni kujitolea tu sio lazima kila kitu kianze na hela hela ni matokeo.Lakini sasa hivi kila kitu ni lazima Proposal na tusipopata hela hatufanyi lolote hili nalo ni tatizo lingine.kwani sio kila jambo linataka hela ya mfadhili jamani tuonyeshe mfano ndipo tutafute pesa.Leo ukipewa milioni mia utaifanyia nini?hela sio jambo la kwanza ni matokeo ya mipango kazi yako.vijana tuamke tujiunge pamoja ndipo serikali inaweza kufanya kazi nasi serikali haiwezi kufanya kazi na mtu mmoja mmoja.
  • Maamuzi yote ya serikali ambayo hutolewa ama bungeni ama kwenye vikao vyao yatendewe kazi na hela yote iliyotengwa kwa ajili ya jamii hususana vijana itumiwe kama ilivyopangwa na vijana wafikiwe na sio wajanja wachahe tu wanatumia hila na kuitumia hela ile na hakuna hatua zinazochukuliwa zidi yao.Jeshi la polisi na taasisi za serikali -taasisi ya  kuzuia Rushwa(PCB) ipewe meno makali waweze kudhibiti wachache hawa ambao hawana uchungu na wananchi bali wameendekeza starehe na kujinufaisha wenyewe.Kesi za watu kama hawa ziwe hadharani na watu hawa waandikwe kwenye vyombo vya dola na habari ili wengine wasiige mifano yao mibovu ikibainika wamekula hela za wanyonge.

Sisi kama asasi (Africa Upendo Group)tunatoa mafunzo mengi sana kwa vijana mbalimbali kuanzia waliomaliza vyuo vikuu hadi chini.Tuna program ambayo tunaiita FikraPlus kwa kushirikiana na HAIBA Tanzania tumewafikia vijana wengi sana na pale ofisini kwetu tumefungua Change Mind Clinic.Tunadhani na tunaamini kuwa tatizo kubwa la watu mbalimbali awe ni kiongozi,mfanyakazi,mwanafunzi na kijana wa rika lolote lile kama ni Mbunge au Waziri tatizo lipo katika MIND. Ukibadilisha mtazamo wako kutoka hasi kwenda chanya na ukajitambua kuwa wewe ni nani ukoje na unatakiwa uweje bila shaka maisha yako yatabadilika.Tatizo sio serikali wala kijana wala mzazi tatizo ni MIND zetu.

Hebu leo tuanze na sisi wenyewe kuwa sisi ndio tunaweza kuwafanya vijana wakabadilisha mitazamo yao.Wakajitambua na kujithamini kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa.Badala ya wao kukimbilia mijini hebu tushirikiane tuwape elimu.pale ulipo ndipo unapoanzia.haihitaji hela labda kama unataka kuja Dar au mimi nataka kwenda Mtwara ,mbeya, kilimanjaron.k .Waalike hapo wewe ulipo anza kuwajengea uwezo kama utahitaji masomo tunaweza kuyatuma au hata kuyaweka kwenye account yetu na ukawafundisha vijana na hata viongozi.Sisi tuliwafundisha vijana ambao tunaishi nao na kwa sababu hapa wapo vijana wanasoma UDSM na wale waliomaliza vyuo mbalimbali kama UDOM,SAUTI,TUMAINI,IFM,n.k tumewatumia sana nao wamekwenda kule kata ya WAZO na kuwafundisha kuanzia kata nzima viongozi wote hadi wajumbe wa nyumba kumikumi sasa tupo kwa vikundi mbalimbali tunawaelimisha umuhimu wa kujithamini kujitambua na jinsi ya kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa sasa hata wakiwaita watu wa taasisi za fedha n.k wanajua kwa nini wapewe hela na watazifanyia nini na sio lazima ukope.Wengine tumewafundisha ufugaji wa kuku wa kienyeji jinsi ya kuwafuga kwa njia ya kupata lishe na kipato wameanza sana na wanafankiwa kwani karibu kila mtu ana kuku lakini hakujua kumbe kwa kuku mmoja anaweza kupata milion moja na laki nane kwa mwaka 1,800,000.00 je akiwa na kuku kumi au mia sio tajiri kwani huyu anataka mtaji?si kuelimishwa tu.Haya tunayo maji kibao Tanzania nzima je Samaki si pia ni chakula yaani lishe bora lakini pia ni kipato kizuri sana hakihitaji hela hata ni elimu tu na unaweza ukawa tajiri hapo hapo kijijini sio lazima uje mjini.

Kwa hiyo mimi nasema hebu tubadilishe mitazamo yetu na tuwasaidie vijana kama serikali NGO na taasisi zingine mfano SACCOS zao zinafanya  nini huko kijijini au VIKOBA au umoja walionao kwanini wanachangishana sana, lakini ni kwa ajili ya tumbo tu.si semi kuchangishana ni vibaya lakini kama tunaweza kuchangishana kwa ajili ya kula harusi je ni vibaya sasa tukabalisha mitazamo yetu na tuklachangishana kwa ajili ya mambo yaletayo tija kama kuchanga ili watoto kumi wenye vipaji wakasoma baadaye wakawa msaada kwa taifa?au tukamleta mtaalamu mmoja akatufundisha na kutusimamia ili tutoke katika hali tuliyo nayo nadhani ni wakati muafaka wa kujitathim ni tena na kuona kama tuko katika mstari ulionyooka au la kama watanzania.Tuamke tutoke katika usingizi mzito na Mungu atusaidie tufanye yale ambayo tulikuwa hatuwezi kuyafanya kwa ajili ya watoto wetu na taifa kwa ujumla.

Uhalifu utapungua au kwisha kama vijana watatambua wajibu wao kwa taifa na kama wapo ambao watakuwa wanaendelea hatimaye wataacha kama kila mtu atajitambua na kuwa busy na hao wahalifu wakija watagundulika mapema sana.na hatimaye uhalifu utakuwa hauna mashiko.Hata zamani ulaya watu walikuwa kama sisi lakini walipojitambua na kuchapa kazi leo angalia wachina ,wajapan,n.k ulaya watu wanaiba lakini sio kama huku hata kama ukiacha kitu chako hapo utakikuta,ukiingia supermarket huwezi kuiba ukienda kwenye mitaa husikii wizi kama huku kila mahali ni amani tupu labda wizi ule mkubwa wa kutumia mitandao n.k sio wizi kama wetu hao wanaoiba wamesoma na kubobea wanajaribu kuibia marais na wakubwa wenye pesa lakini sisi hadi inashangaza hata mtalii akija ameshaonywa kwamba hapafai .Uhalifu wenu ni wa tofauti sana wetu wengi ni vibaka wanakwapua pochi za walala hoi n.k hadi wanaitwa Panya Road

mfano wale vijana wanatumia madawa ya kulevya wakijitambua wataacha na kufanya kazi kama wengi leo walivyo kwenye bodaboda n.k wale wauzaji watakosa soko wataacha kuingiza yale madawa na dawa za kulevya hazitakuwa na soko tena hapa kwetu lakini kwa vile matajiri wauza unga wamekumbatiwa na kikundi kidogo kisicho kuwa na maadili kinasababisha kundi kubwa la vijana kuangamia.

Wakiwa tayari hawana maadili wanaingia katika makundi maovu na kufanya uhalifu lakini kama hawa watakuwa na njia mbadala kama kilimo basi uhalifu utakwisha kwani mtu akiwa ni mkulima au yuko busy sana anachoka hatimaye analala lakini kama haan kazi ya kufanya atakuwa tu kwenye makundi kucheza pool n.k

Asasi hii kama yenu tuungane pamoja tufanye yale tunayoweza kufanya naamin wapo wengi watatuunga mkono na polepole kila kitu kitakuwa shwari.Haya ni maoni yangu binafsi hayana uhusiano na mtu ama kikundi chochote na wala sina nia ya kumchafua mtu bali nimeona nitoe yaliyo moyoni mwangu.Asanteni.

 

Asasi ya ukombozi wa vijana AUVITA (via email)
June 13, 2014 at 10:16 PM EAT
Nashukuru kwa ujumbe wako mzuri ambao kwa kiwango kikubwa umenifunza mengi
na kunionesha njia. Nikweli kabisa tatizo la vijana katika nchi yetu
halitotatuliwa kwa propaganda za kisiasa ama maneno matupu bali linahitaji
kujitoa mhanga na kuonesha moyo wa kipekee wa uzalendo wa
kuwafunza/kuwaelimisha vijana na kuibadili mitazamo hasi ambayo ni mitazamo
funge ya fikra na kupandikiza mitazamo chanya ambayo inazaa matunda ya heri
na fanaka. Vijana wa tanzania wanahitaji msaada wa kifikra ambao utawaondoa
pangoni na kuwaleta kwenye mwanga, tunahitaji kujitolea kwa hili na
kuonesha ushirikiano na jamiii itatufuata baada ya kuona mafanikio. Sisi
wana AUVITA tuko tiari kabisa kushiriki nanyi katika ukombozi huu wa vijana
kwani ndiyo dhamira yetu kuanzisha asasi hii hivyo kwa hili tuko pamoja na
wala hatutarudi nyuma. Pia umesema kuwa mumeshafanya mafunzo mbalimbali na
matini munayo naomba utusaidie matini hayo ili tuyatumie pia kuwakomboa
vijana wa mtwara ambao kweli dunia inaonesha kuwatupa mkono maana hofu
waliyonayo vijana inahitaji jitihada kuwakomboa kifkra.

Wako,

Simba Mramba.


2014-06-11 15:36 GMT+03:00 Envaya :
Africa Upendo Group
June 24, 2014 at 3:18 PM EAT

nitumie email yako binafsi  yangu pia ukitualika tunakuja kukuonyesha njia utakayoweza kufanya maajabu.

Asasi ya ukombozi wa vijana AUVITA (via email)
June 25, 2014 at 3:15 PM EAT
Email yangu binafsi ni, tiganize@gmail.com au mrambasimba@yahoo.com
Emmanuel Mihambo (Mwanza,Nyamagana)
December 6, 2015 at 1:30 PM EAT
Mimi ni mwenyekiti Wa kikundi cha umoja name ushirikiano Wa vijana ninaomba ushauli jinsi ya kuendeleza kikundi hiki ilikikue na tunufaike sisi kama vijana Wa taifa hili
Denize Theonest (Dar es salaam)
January 22, 2016 at 3:41 PM EAT

@ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA): 

Adam Kheri Famao (Dar es Salaam)
February 29, 2016 at 5:22 AM EAT

@Neatness Msemo (Dar es salaam): 

Adam Kheri Famao (Dar es Salaam)
February 29, 2016 at 5:25 AM EAT
Samahani...Mimi ni mwanachuo nipo UDOM...nilikuwa naomba kujua jinsi ya kuanzisha kikundi cha vijana kwa ajili ya kufanya shughuli za kimaendeleo na hatua za kufuata
Adam Kheri Famao (Dar es Salaam)
February 29, 2016 at 5:39 AM EAT
Naomba majibu kupitia email yangu adamfamao@gmail.com
Kisota Laizer (Arusha)
July 8, 2016 at 5:00 PM EAT

E mail yangu ni llonyori@yahoo.com

STEVEN SYLIVESTER DUGUZA (KAGERA)
February 1, 2017 at 2:53 PM EAT

 Mimi ni kijana umri miaka 25 ni Mwanachuo chuo cha SAUT MWANZA nasoma bachelor degreee in Economics and Geography ninaomba kujua jinsi gani ya kuanzisha kikundi cha vijana cha ujasiriamali nimepata elimu ya kutosha kuhusiana na ujasiliamali.

Mawasiliano:-

Phone no: 0757388737

denizetheo (via email)
February 10, 2017 at 6:08 PM EAT
Habari? Wewe kama we unajihusisha na ujasiliamali upi?
[message deleted]
BONIPHACE GERVAS (KIGOMA)
February 12, 2017 at 6:52 PM EAT (edited February 12, 2017 at 6:53 PM EAT)

Hakika nimefarijika kukuta page inayozungumzia changamoto za vijana hakika mmegusa nyanja nzuri nliiyo ipenda nakufikiri nami kama kijana napataje fulsa .Tafazari naomba nipewe elimu jinsi gani ya kuanzisha kikundi cha vijana na namna gani ya kupata mtaji pia niombe kupewa elimu juu ya ujasiliamali. 

Nipo UDOM boniphace gervas.

mawasiliano.0766206631

        Boniphacegervas@gmail.com

DENIZE THEONEST (via email)
February 12, 2017 at 7:21 PM EAT
0715383318
philimon thomas (chato,geita)
May 18, 2017 at 3:49 PM EAT

Nimejifunza mengi ktk asasi yenu ,nashukuru kwa ujumbe wenu mzuri kwan kwa kila kijana atakayeupata na kuusoma akaufanyia kazi naamin utaleta mafanikio kwake na kwa jamii kiujumla.

[message deleted]
evaline (dareslaam)
May 22, 2017 at 12:51 PM EAT

@Neatness Msemo (Dar es salaam): Asante sana Neatness Msemo nimeona challenges nyingi na nimejifunza kitu kwenye post yako pia ninakubaliana na wewe tatizo ni MIND wala hamna kingne.What you are doing kwenye company yenu ni kitu kizuri sana Mungu awabariki.

hamza jabir (samora avenue)
November 6, 2017 at 2:44 PM EAT

@ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA): 

am proud of you; its amazing work that your doing. am trainer also via Ashoka Product from USA. am a Coach, Mentor, facilitator, and Consultant for Civil Society, and dealing with youth, on enterprenur, Community Leader, and Culture of Volunteerism in Tanzania, we have the new Unit in Tanzania. you can find me via jabilihamza@yahoo.com


Add New Message

Invite people to participate