UTEUZI WA MSHAURI WA MASWALA YA AFYA WA SHIRIKA.
Mkurugenzi wa shirika la AHF nchini Tanzania bwana Albert.T.Msafiri amemteua rasmi Dr Oswad Lyapa kuwa mshauri wa shirika hilo katika maswala ya afya, uteuzi huo umethibitishwa na Dr. Frank Mukiza ambae ni mkurugenzi wa shirika hilo nchini Uingereza. Pia Dr Oswad atakua na jukumu la kuongoza timu ya madaktari na wauguzi watakao jitolea kutoa huduma za afya sehemu mbalimbali ndani na nje ya inchi.Dr. Oswad ambaye kwa sasa yupo katika hospitali ya mwananyamala jijini Dar es salaam amepoke kwa furaha kubwa uteuzi huo na kuaidi kutekeleza wajibu wake kwa bidii na ufanisi mkubwa.
Pichani ni Dr Oswad Lyapa
15 Desemba, 2010
Maoni (2)