Injira
African Heritage Foundation

African Heritage Foundation

Dar es Salaam, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

UZINDUZI WA KITUO MAALUM CHA ELIMU.


Shirika la African Heritage Foundation inchini Tanzania limezindua kituo maalum cha elimu kiitwacho(Talented Brothers Academy).Uzinduzi huo ulifanywa na Bwana Moses Katega  aliyekua mgeni rasmi ambaye ni katibu mtendaji wa shirika hili nchini Uingereza majira ya saa 01:45 mchana.Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wajumbe kutoka jumuiya ya Watganzania wanaoishia Italia pamoja na viongozi wa kituo hicho waalimu na wanafunzi.Hafla hiyo ilifuatiwa na muhadhara mfupi ulioongozwa na Bwana Katega uliohusu Historia ya mwanadamu ambayo ilikua ni changamoto kubwa kwa waalimu na wanafunzi.Pia mratibu wa elimu wa shirika Bwana Christopher Kauno alieleza kua kituo hicho kitakua ni msaada mkubwa kwa jamii inayowazunguka.Pichani juu wa kwanza kushoto ni Bwana Katega Bitegeko katibu wa shirika hilo Uingereza,wa pili ni Mratibu wa elimu wa shirika bwana Christopher Kauno na watatu ni Bwana Albert.T.Msafiri mkurugenzi wa shirika hilo Tanzania wakijiandaa kuzindua kituo.Pichani chini ni Bi.Sauda Mapondela mwakilishi wa wanafunzi akitoa risala katika hafla hiyo.Picha zinazofuata ni matukio mbalimbali katika hafla hiyo na mwisho ni picha za majeng ya kituo hicho.

25 Kanama, 2010
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.