Fungua
AGENCY FOR BETTER HOPE AND SOCIAL UNITY[ABHASU]

AGENCY FOR BETTER HOPE AND SOCIAL UNITY[ABHASU]

MBEYA, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

ABHASU kupitia  mradi wake wa SOCIAL PROTECTION FUND PROJECT (SPF)yatoa msaada wa majanga kwa wanachama.

Familia mbili za wanachama wa Agency for Better Hope and Social Unity hivi karibuni wamenufaika na kuwepo kwa shirika hili kwa kupata msaada wa kijamii wa kukabiliana na misiba. ABHASU imetoa jumla ya Tsh 700,000( laki saba tu) kama rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Wanachama wa ABHASU pia walishiriki kwa hali na mali katika shughuli mbalimbali kwenye misiba hiyo na kuwafariji wanajamii waliopatwa na misiba hiyo.

 

Clifford Majani

Katibu

RafikiElimu Foundation wazindua mradi wa MAFUNZO YA UJASIRIAMALI BILA MALIPO

 

Mwalimu wa ujasiriamali wa rafikiElimu akiwa anafundisha

Taasisi hii hutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kati ya miaka 15-45 bila malipo yoyote, tafadhari itumie fursa hii kujikwamua.

Kwa mawasiliano na RafikiElimu foundation piga simu 0763 976548 au 0782405936

au tembelea tovuti yao http://www.rafikielimu.blogspot.com

au waandikie kwa barua pepe: rafikielimutanzania@gmail.com

Na Clifford B. Majani

Katibu Mkuu

Agency for Better Hope and Social Unity

 

 

FOMU YA KUOMBEA UANACHAMA

KUJIUNGA NA ABHASU

Kwa mtu yeyote anayetaka kujiunga na shirika hili anakaribishwa kutuma maombi kwa mwenyekiti wa shirika ambaye atampatia fomu ya kujaza. Fomu hii italipiwa Tsh 1000/- [elfu moja tu]. Hakikisha umeisoma katiba na kuelewa madhumuni,malengo na faida ya uanachama kwanza. Nakala ya katiba imeeambatanishwa hapa chini.

Wenu Katibu Mkuu

ABHASU

The E-mail of ABHASU is : abhasuinfo@yahoo.com

Anuani ya barua pepe ya ABHASU ni : abhasuinfo@yahoo.com

Anuani hii inaweza kutumiwa na mwanachama au mtu yeyote kwa ajili ya mawasiliano na asasi yetu.

Website yetu ni : https://envaya.org/abhasu

Tunawashukuru sana ENVAYA kwa kutuwezesha kupata wavuti huu.

Imeandikwa na

Clifford Majani[ Mwenyekiti wa ABHASU]