Log in
UVIKITWE GROUP

UVIKITWE GROUP

Dar es salaam, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Mradi wa elimu ya kina kuhusu uwezo kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa wafanya biashara za ngono na watumiaji wa dawa za kulevya katika maeneo ya machimbo ya Dar-pori, Masuguru, Mpepo na Lukarasi yalioko katika wilaya ya Mbinga - mkoa wa Ruvuma. Mradi huu umeweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwa wlengwa wa moja kwa moja, baada ya kupewa elimu ya stadi za maisha na kuweza kuwajengea uwezo wa kujitambua na kutambua mahitaji yao ya msingi, pia mradi huu umeweza kuleta mabadiliko ya shughuli za kiuchumi hasa kwa akina dada wanaojiuza kwenye maeneo ya ya machimbo baaday kuwa kufikia uamuzi wa kubadilisha kazi ya kujiuza kama njia ya kijipatia riziki ya kilasiku, na kuanzisha biashara zingine kwa mtaji wa sh millioni 25 ( TZS 25,000,000) kama ruzuku kwa njia ya vikundi. vikundi vilivyoanzishwa na kusajiliwa rasimi na serikali ni vikundi 12, kumi vikiwa ni vya akina dada na viwili ni vya akina kaka wanaotumia dawa za kulevya. Lengo la uvikitwe ni kuweza kutumia fursa zilizopo ili kuweza kuiokoa jamii ya kitanzania hasa iliokuwa masikini zaidi, kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi, kiutamaduni na kisikolojia.

November 21, 2011
« Previous Next »

Comments (2)

RAMADHANI MGAYA (DAR ES SALAAM) said:
HONGERA KWA KAZI NZURI.MSIISHIE HAPO TU
January 9, 2012
Uvikitwe Group (via email) said:
Ushauri wako tunauheshimu na kuuthamini sana tusaidiane kiushauri ili tuweze kuboresha shughuli hizi za jamii.
January 9, 2012

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.