KWA NINI TUNAHITAJI USHIRIKI WA MWNAMKE KATIKA KATIBA MPYA?
Kwa kuwa tunahitaji katiba itakayokidhi matakwa ya mwanamke na mwanaume ,hivyo ushiriki wa makundi yote haya kwa uwiano sawa ni muhimu ili kuleta mabadiliko ya kweli na kupata katiba itakayosimamia usawa, haki ,utu na heshima ya wananchi wake bila kujali jinsia.
Kutokana na changamoto hii na kwakuzingatia idadi ya watanzania inayoonyesha kuwa wanawake wana idadi kubwa ikilinganishwa na idadi ya wanaume katika sensa iliyopita inayoonyesha wanawake ni asilimia hamsini na moja ( 51% )ya watanzania wote ,Hivyo wanawake tunalojukumu la kuwahamasisha wanawake wenzetu walioko pembezoni ili wajue umuhimu wa katiba ya nchi na waweze kujitokeza kushiriki katika mchakato wa kuandaa katiba mpya kwa kuchangia / kutoa maoni yao.
Ibitekerezo (5)